Nimeacha pombe na sigara lakini napata taabu sana, sipati usingizi hadi usiku wa manane

Hongera hakuna kitu kinashindikana kuacha ukijizatiti na kuwa na msimamo.
 
Amen mkuu sitak artificial medication mkuu watanipa methadon hao🤣🤣 sema ntatoboa
 
Hapana mkuu nilishindwa kuacha taratibu nilikua nikivuta muda tu unaenda huku nikijiapiza kuacha na kulaumu nikilud tena
Sema utaacha tu kwa sababu ushaweka Nia. Kikubwa kua serious na jitahidi kuyapitia Mara kwa Mara madhara yanayosababishwa na sigara pamoja na pombe hiyo pia itakupa msukumo wa kuacha.
 
Anavyokosa usingizi maana yake hajaacha pombe..bado anashawishika kugida.

Labda tuambie ulikuwa unapiga bia au vikali
Vyote na sigala mkuu isipokuwa vile vya ovyo kama visungura na wenzake
 
Sema utaacha tu kwa sababu ushaweka Nia. Kikubwa kua serious na jitahidi kuyapitia Mara kwa Mara madhara yanayosababishwa na sigara pamoja na pombe hiyo pia itakupa msukumo wa kuacha.
Amen mkuu
 
Amina mkuu miez 3 itaisha tu na hakika na kuendelea ntafanya yote uliyo niambia
 
Nilijitahidi kuacha pombe lkn nashindwa.

Nilianza kuacha kunywea bar. Nimeshinda sasa nanywea home.

Home nilijitahidi kuacha kwa kuanz kunywa bia chache hadi moja, bado ninehamia kula sprit. Yaani kwa sasa nakuwa kama popo.

Ushauri wa kwenda kwa daktari nikafanyiwe detoxification napata ubaridi maana niknikama kwend kufanyiwa ile kusFisha figo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…