Nimeangusha pesa ya rambirambi 300,000/= cash mchana huu

Mkuu kama ni suala la kupewa pole, basi ipokee ya dhati kutoka kwa wana JF. Lakini hakikisha kuwa pesa ya itokanayo na michango ya wadau unaiwakilisha ktk ukamilifu wake wote.

Nawasikitikia sana kwa kuwa bado mpo ktk mfumo wa kupokea fedha taslimu, mfumo ambao una changamoto nyingi sana ikiwemo suala ambalo limekusibu. Ktk masuala ya menejimenti ya fedha, watu wengi hupendelea miamala ifanyike kupitia njia ktk njia za kidijikali. Jambo hili hufanyika ili uwepo wa uwazi ktk kufanikisha masuala ya mihamala husika na kumbukumbu zake.

Mkuu huna ujanja zaidi ya kulipa fedha za watu. Ila unalo jambo la kujifunza, nalo si lingine zaidi ya kuepuka kupokea fedha taslimu za michango ya watu. Unapaswa kubadilika ili nawe uwe sehemu muhimu ya matumizi ya uhakika ya teknolojia ya sasa yenye uwezo mkubwa wa kuthibiti miamala ya fedha inayotumika.
 
Nashauri upelekwe kituo cha polisi kilichopo karibu nawe ili ukaongee unachokijua kuhusu ulipopeleka hizo pesa.Na hukohuko ndipo utabadilishwa kutoka infantry soldier kuwa jeshi la akiba la ccm
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…