Nimedokezwa: MOU 30 alizosaini Rais Dubai zikiwekwa hadharani, waTanganyika wote tutalala uchi barabarani

CAG ameanza lini kuvumbua madudu kwa uwazi?. Tangu awamu ya nne yupo na uwazi huu na madudu anayavumbua kila kukicha.

Na upo uwezekano mpaka sisi tunaondoka duniani atakuwa anavumbua tu madudu, ni mentality tunayo ya kitaifa.

DPW anakuja kuongeza ufanisi wa bandari yetu. Sijui kama unafurahi kusikia meli moja inachukua siku mbili au tatu ikisubiri pale nje ya bandari. Sijui kama unafanya biashara yoyote yenye kukuweka karibu na bandari ukajua ni changamoto zipi zenye kuhitaji utatuzi wa haraka.

Tumuache SSH apige kazi.
 
 
CAG ameanza lini kuvumbua madudu kwa uwazi?. Tangu awamu ya nne yupo na uwazi huu na madudu anayavumbua kila kukicha.
Mkuu unajua hata logic wewe ndio umesema zamani kulikuwa na wizi sasa hivi mambo yamebadilika hence mikataba itakwenda sawa sawia sababu sasa hivi kila kitu ni Kosher....

Ndio nikakuuliza sasa hivi ambapo kila kitu ni Kosher mbona CAG anagundua madudu (au hio suggestion kwamba tusihofu sasa hivi kila kitu ni sawa inaishia wapi)?
Na upo uwezekano mpaka sisi tunaondoka duniani atakuwa anavumbua tu madudu, ni mentality tunayo ya kitaifa.
Kwahio hayo madudu upigaji unaishia wapi ? Huku kwenye mikataba / Makubaliano hakuna madudu
Kwahio unadhani makubaliano yakiwa na tija zaidi kwetu ufanisi utaondoka ? Jaribu kutofautisha Makubaliano mazuri kwa manufaa ya wote, Utendaji mzuri / Mbovu na Makubaliano Mazuri na Utendaji mzuri..., Haimaanishi kupata makubaliano mazuri kunaondoa ufanisi (Yaani ufanisi lazima uendane na makubaliano mabaya - TICTS Makubaliano yalikuwa mabaya na Utendaji Mbaya - Haimaanishi tuingie makubaliano mabaya kwa ajili ya Utendaji Mzuri why not Vyote ?)
 
Hakunaanaekataa uwekezaji ili kuongeza ufanisi, kwani ufanisi huo haiwezi kupatikana bila kuuza nchi , watu wake, na Sovereignity yetu? Hoja ni kukataa vipengele vya kimangungo, sio uwekezaji, hatukatai uwekezaji
 
Vipengele vya mkataba vinatuingiza utumwani kwa kuuza nchi, watu wake na Sovereignity yetu, hoja ni hiyo
 
Kwahiyo nikisaini mkataba leo halafu kesho ukafuatia mkataba mwingine, automatically uke mkataba wa mwanzo unabadilika na kuwa makubaliano, si ndio?

Kwamba mlichosaini na kupitisha bungeni ni mkataba, ila mkijankisaini mkataba mwingine ndio huu utabadilika na kuwa makubaliano, sivyo?
 
Wa kusikia🙌
 
Makubaliano [agreement] mkataba [contract]. Makubaliano huanza kwanza kisha mkataba hufuatia.
Ok sawa...so what!
Kilichopelekwa bungeni ni makubaliano
Huu uongo unautoa wapi. Hebu msikilize msaliti Tulia alikiitaje kilichopelekwa bungeni siku ya kwanza ya mjadala wa kuridhia mkataba wa DP!

Wapotoshaji wanakuja na hoja kwamba kilichopelekwa bungeni ni mkataba wakati ukweli ni kuwa yale ni makubaliano yanayowezesha mikataba kuja kuandikwa. aji.
Baada ya serikali kushtukia ilivyoshukiwa na wananchi kuhusu huo mkataba wa hovyo ndipo katika kuhaha wakaja na na maelezo hayo ya kucheza na maneno.
 
Amesaini kwa jina la JMT tukiachana na Zbr tukabaki Tg tunawasambaratisha
Hujasoma makubaliano yote. Soma article 19 'If the sate party is replaced or succeeded by one or more states.................... Any successor state shall be considered as party to this agreement........'
Kwa hiyo hata ukibaki Tanganyika, huchomoki kwenye makubaliano hayo.
Someni someni
 
Mama yupo kazini😂😂😂 mama anaupiga mwingi mama anaifungua nchi. Hivi wale chawa wa mama wako wapi skuhizi sioni nyuzi zao kabisa
 
Hizi ni conspiracy theories za kawaida, ni siasa za kuyashuku maamuzi ya kiserikali na ndio uhuru wenyewe wa habari, ndio demokrasia yenyewe hii.
 
Azimio la bunge kuhusu pendekezo la kuridhiwa mkataba. Maana yake hicho kilichopo hapo ni agreement ya IGA, mikataba halisi inatengenezwa kwa makubaliano ya pande mbili, DP na wadau wa bandarini kuhusu biashara husika inayotajwa kwenye hiyo IGA.
 
Wengi ni wapiga kelele na baadhi ni bendera hufuata upepo. Hakuna mkataba wa kibiashara uliosainiwa mpaka dakika hii.

Itakuja kusainiwa muda sio mrefu kwani mkataba unahusisha biashara fulani maalum pale bandarini. Kilichokwenda bungeni ni agreement ya IGA, ni sawa na skeleton tu, mtu mwenyewe ataundwa kwa makubaliano kati ya mwekezaji na mzalendo.

Hapa ndipo wanasheria na wasomi wengi wanapoziteka akili za kivivu zetu watanzania kwa kutuaminisha kuwa kile kilichokwenda bungeni kina nguvu kuliko kile kitakachoziongoza biashara za uwekezaji zitakazofanyika pale TPA.

Watu wameingizwa chaka na hawa wanasheria kina Mwabukusi na kwa sababu ya uvivu wetu wa kutafuta maarifa tumeingizwa chaka mazima.
 
Vipengele vya mkataba vinatuingiza utumwani kwa kuuza nchi, watu wake na Sovereignity yetu, hoja ni hiyo
Mkataba upi wenye vipengele vinavyotuingiza utumwani?. Hiyo ndiyo kazi haramu inayofanywa na wanasheria kina Rugemeleza na Mwabukusi, kuwadanganya watu wakiwa na nia ovu kwa bandari na maslahi yake mapana.

Hakuna mkataba wowote uliosainiwa kwani mikataba ya kibiashara inatokana na makubaliano yaliyopitishwa na bunge. Azimio lililopita bungeni halina nguvu kulingana na kile kinachokwenda kuandikwa kwenye mikataba ya biashara inayokubalika na pande zote mbili na kuwa mwongozo wa biashara ya hapo TPA.
 
Kilichosainiwa bungeni sio mkataba ni azimio la makubaliano ya kufanyika biashara ya pamoja kati ya DP na Tanzania.

Mikataba itakwenda kuandikwa na kusainiwa baadae, ni baada ya majadiliano ya kina kuhusiana na uwekezaji utakaofanyika hapo bandarini.

Kilichopelekwa bungeni ni IGA, kinachosainiwa kwa ajili ya kufanyika kwa biashara kinaitwa HGA, ni vitu viwili tofauti.
 
Ondoa wasiwasi na mashaka, amini nchi yako ipo katika mikono salama.

Wizi upo dunia nzima, hakuna serikali isiyo na ufisadi ndani yake kuanzia zile kubwa kina USA, Russia na sisi huku Tanzania.
 
Ondoa wasiwasi na mashaka, amini nchi yako ipo katika mikono salama.

Wizi upo dunia nzima, hakuna serikali isiyo na ufisadi ndani yake kuanzia zile kubwa kina USA, Russia na sisi huku Tanzania.
Kwamba wewe una uelewa wa sheria kuliko Shivji?Muda utaongea.
Uzuri pia tumeweka risiti ya hili.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…