Nimedokezwa: MOU 30 alizosaini Rais Dubai zikiwekwa hadharani, waTanganyika wote tutalala uchi barabarani

Nimedokezwa: MOU 30 alizosaini Rais Dubai zikiwekwa hadharani, waTanganyika wote tutalala uchi barabarani

If you really believe what you have just written..., Pole Sana is all I can Say; Lakini kama unajua unachoandika sicho ila basi tu unaamua kupotosha ili unufaike kwa lipi I do not know..., lakini I doubt if what you are getting is a price worth of selling your soul (unless hata conscious hauna tena)

By the way nikukumbushe tu madudu aliyoyavumbua CAG ya upotevu wa mapesa ya UMMA lukuki hivi recently, ilikuwa ni AWAMU gani ?!!
CAG ameanza lini kuvumbua madudu kwa uwazi?. Tangu awamu ya nne yupo na uwazi huu na madudu anayavumbua kila kukicha.

Na upo uwezekano mpaka sisi tunaondoka duniani atakuwa anavumbua tu madudu, ni mentality tunayo ya kitaifa.

DPW anakuja kuongeza ufanisi wa bandari yetu. Sijui kama unafurahi kusikia meli moja inachukua siku mbili au tatu ikisubiri pale nje ya bandari. Sijui kama unafanya biashara yoyote yenye kukuweka karibu na bandari ukajua ni changamoto zipi zenye kuhitaji utatuzi wa haraka.

Tumuache SSH apige kazi.
 
Muda sio mrefu inakwenda kuandikwa mikataba ya kibiashara kati ya DPW na serikali ya Tanzania na nyinyi pingapinga mtakuwa wa kwanza kufaidika na urahisishwaji wa shughuli za bandari.
Nimefuatilia hoja kwenye huu uzi, nimeiridhisha, japo una ufahamu kinachoendelea kuhusu uwekezaji bandarini, hujajikita kwenye hoja zinazopinga baadhi ya vifungu vya "Makubaliano" hayo.

Wote wanaoutetea wanadai nchi itafaidika (rejea maelezo yako rangi nyekundu) kwa uwekezaji huo kana kwamba ndio uwekezaji wa kwanza nchini km kwenye uchimbaji wa vito na madini, tena yenye thamani kubwa (almasi, dhahabu), nchi imefaidika nini hadi leo? Tatizo liko kwenye mikataba. Angalau hayo makubaliano yamevuja tukajua mbivu na mbichi.

Kama makubaliano hayo ndio msingi wa kutengeneza mikataba ya utekelezaji, hakuna shaka kuwa matokeo yatakuwa ni yale yale ya uchimbaji madini na ukodishaji mbuga za wanyama. Bado tu ardhi kukodishwa, kwa kile kitachotetewa kuwa imekaa bure, na waTanzania kufanywa vibarua mashambani humo.

Swali: Tunakopa na kuomba misaada, kwa nini tusifanye hivyo kwa bandari zetu, tukatafuta na kumlipa mwenye uwezo wa kuendesha, hata kama ni huyo DPW?
 
CAG ameanza lini kuvumbua madudu kwa uwazi?. Tangu awamu ya nne yupo na uwazi huu na madudu anayavumbua kila kukicha.
Mkuu unajua hata logic wewe ndio umesema zamani kulikuwa na wizi sasa hivi mambo yamebadilika hence mikataba itakwenda sawa sawia sababu sasa hivi kila kitu ni Kosher....

Ndio nikakuuliza sasa hivi ambapo kila kitu ni Kosher mbona CAG anagundua madudu (au hio suggestion kwamba tusihofu sasa hivi kila kitu ni sawa inaishia wapi)?
Na upo uwezekano mpaka sisi tunaondoka duniani atakuwa anavumbua tu madudu, ni mentality tunayo ya kitaifa.
Kwahio hayo madudu upigaji unaishia wapi ? Huku kwenye mikataba / Makubaliano hakuna madudu
DPW anakuja kuongeza ufanisi wa bandari yetu. Sijui kama unafurahi kusikia meli moja inachukua siku mbili au tatu ikisubiri pale nje ya bandari. Sijui kama unafanya biashara yoyote yenye kukuweka karibu na bandari ukajua ni changamoto zipi zenye kuhitaji utatuzi wa haraka.

Tumuache SSH apige kazi.
Kwahio unadhani makubaliano yakiwa na tija zaidi kwetu ufanisi utaondoka ? Jaribu kutofautisha Makubaliano mazuri kwa manufaa ya wote, Utendaji mzuri / Mbovu na Makubaliano Mazuri na Utendaji mzuri..., Haimaanishi kupata makubaliano mazuri kunaondoa ufanisi (Yaani ufanisi lazima uendane na makubaliano mabaya - TICTS Makubaliano yalikuwa mabaya na Utendaji Mbaya - Haimaanishi tuingie makubaliano mabaya kwa ajili ya Utendaji Mzuri why not Vyote ?)
 
Usidhani mpaka kufikia hatua ya serikali kuutaka uwekezaji wa DPW hakuna utafiti wa kina uliofanyika, usijidanganye kuhusu hilo.

Wengi tunaopiga kelele kuupinga huu uwekezaji hatuna hata biashara ndogo tu zinazotuweka karibu na bandari kuweza kujua ni ugumu gani unaozuia ufanisi wa shughuli za kila siku mahali pale. Tupo kishabiki zaidi.

Muda sio mrefu inakwenda kuandikwa mikataba ya kibiashara kati ya DPW na serikali ya Tanzania na nyinyi pingapinga mtakuwa wa kwanza kufaidika na urahisishwaji wa shughuli za bandari.

Mmeshazoeleka nyinyi wazee wa kupinga kila kitu, mlipinga hata matumizi ya usafiri wa mwendo kasi katika jiji la Dar na leo mnaamka saa kumi na mbili asubuhi kuuwahi ili mfike mapema katika shughuli zenu.
Hakunaanaekataa uwekezaji ili kuongeza ufanisi, kwani ufanisi huo haiwezi kupatikana bila kuuza nchi , watu wake, na Sovereignity yetu? Hoja ni kukataa vipengele vya kimangungo, sio uwekezaji, hatukatai uwekezaji
 
Kujiingiza utumwani ni tatizo binafsi la akili ya mtu. Hakuna wa kukufanya mtumwa katika karne ya sasa. Ni ulimwengu wa biashara na uwekezaji wa kisasa.

Serikali imeangalia ni mwekezaji yupi mwenye vifaa vya kisasa atakayeongeza tija pale bandarini. Na taasisi za wafanyabiashara zimemuelewa vyema nini anataka kufanya rais wa awamu ya sita.
Vipengele vya mkataba vinatuingiza utumwani kwa kuuza nchi, watu wake na Sovereignity yetu, hoja ni hiyo
 
Makubaliano [agreement] mkataba [contract]. Makubaliano huanza kwanza kisha mkataba hufuatia.

Kilichopelekwa bungeni ni makubaliano na kinachokwenda kusainiwa na kuingia katika hatua za utendaji ni kuandikwa kwa mikataba kulingana na maslahi ya pande mbili ambazo ni serikali ya Dubai na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Wapotoshaji wanakuja na hoja kwamba kilichopelekwa bungeni ni mkataba wakati ukweli ni kuwa yale ni makubaliano yanayowezesha mikataba kuja kuandikwa. Ndio wanaita IGA ambazo zinabariki kuandikwa kwa HGA na pande mbili zinazoingia katika hatua za utekelezaji wa huo uwekezaji.
Kwahiyo nikisaini mkataba leo halafu kesho ukafuatia mkataba mwingine, automatically uke mkataba wa mwanzo unabadilika na kuwa makubaliano, si ndio?

Kwamba mlichosaini na kupitisha bungeni ni mkataba, ila mkijankisaini mkataba mwingine ndio huu utabadilika na kuwa makubaliano, sivyo?
 
Kunataarifa zindai kwamba kuna hati za maelewano zipatazo 30 zilisainiwa na Rais katika ziara yake ya Dubai.

Pia inadaiwa, huu mkataba wa Bandari ni moja tu kati ya vilivyomo kwenye maelewano hayo. Pia kuna sekta zingine kama posta nk.

Inasemekana kwamba, MOU hizo zote zikiwekwa wazi, basi waTanganyika wote mtalala uchi barabarani mkigalagala na kulia.

Ombi, MOU hizo zote 30 alizosaini, ziwekwe wazi.
Wa kusikia🙌
 
Makubaliano [agreement] mkataba [contract]. Makubaliano huanza kwanza kisha mkataba hufuatia.
Ok sawa...so what!
Kilichopelekwa bungeni ni makubaliano
Huu uongo unautoa wapi. Hebu msikilize msaliti Tulia alikiitaje kilichopelekwa bungeni siku ya kwanza ya mjadala wa kuridhia mkataba wa DP!

Wapotoshaji wanakuja na hoja kwamba kilichopelekwa bungeni ni mkataba wakati ukweli ni kuwa yale ni makubaliano yanayowezesha mikataba kuja kuandikwa. aji.
Baada ya serikali kushtukia ilivyoshukiwa na wananchi kuhusu huo mkataba wa hovyo ndipo katika kuhaha wakaja na na maelezo hayo ya kucheza na maneno.
 
Amesaini kwa jina la JMT tukiachana na Zbr tukabaki Tg tunawasambaratisha
Hujasoma makubaliano yote. Soma article 19 'If the sate party is replaced or succeeded by one or more states.................... Any successor state shall be considered as party to this agreement........'
Kwa hiyo hata ukibaki Tanganyika, huchomoki kwenye makubaliano hayo.
Someni someni
 
Mama yupo kazini😂😂😂 mama anaupiga mwingi mama anaifungua nchi. Hivi wale chawa wa mama wako wapi skuhizi sioni nyuzi zao kabisa
 
Ok sawa...so what!

Huu uongo unautoa wapi. Hebu msikilize msaliti Tulia alikiitaje kilichopelekwa bungeni siku ya kwanza ya mjadala wa kuridhia mkataba wa DP!

Baada ya serikali kushtukia ilivyoshukiwa na wananchi kuhusu huo mkataba wa hovyo ndipo katika kuhaha wakaja na na maelezo hayo ya kucheza na maneno.

Hizi ni conspiracy theories za kawaida, ni siasa za kuyashuku maamuzi ya kiserikali na ndio uhuru wenyewe wa habari, ndio demokrasia yenyewe hii.
 
Ok sawa...so what!

Huu uongo unautoa wapi. Hebu msikilize msaliti Tulia alikiitaje kilichopelekwa bungeni siku ya kwanza ya mjadala wa kuridhia mkataba wa DP!

Baada ya serikali kushtukia ilivyoshukiwa na wananchi kuhusu huo mkataba wa hovyo ndipo katika kuhaha wakaja na na maelezo hayo ya kucheza na maneno.

Azimio la bunge kuhusu pendekezo la kuridhiwa mkataba. Maana yake hicho kilichopo hapo ni agreement ya IGA, mikataba halisi inatengenezwa kwa makubaliano ya pande mbili, DP na wadau wa bandarini kuhusu biashara husika inayotajwa kwenye hiyo IGA.
 
Ninyi ndio wale sifia sifia hata ktk mambo ya kijinga yaliolitesa taifa hili kwa miongo mingi hata sasa...sitaki kuamini kama hauna ufahamu wa kile kinacholalamikiwa na watanzania ktk sakata hili...unataka kutuaminisha kuwa wote walioukosoa mkataba huu ni wanaharakati na watu wasiopenda wawekezaji...!
Wengi ni wapiga kelele na baadhi ni bendera hufuata upepo. Hakuna mkataba wa kibiashara uliosainiwa mpaka dakika hii.

Itakuja kusainiwa muda sio mrefu kwani mkataba unahusisha biashara fulani maalum pale bandarini. Kilichokwenda bungeni ni agreement ya IGA, ni sawa na skeleton tu, mtu mwenyewe ataundwa kwa makubaliano kati ya mwekezaji na mzalendo.

Hapa ndipo wanasheria na wasomi wengi wanapoziteka akili za kivivu zetu watanzania kwa kutuaminisha kuwa kile kilichokwenda bungeni kina nguvu kuliko kile kitakachoziongoza biashara za uwekezaji zitakazofanyika pale TPA.

Watu wameingizwa chaka na hawa wanasheria kina Mwabukusi na kwa sababu ya uvivu wetu wa kutafuta maarifa tumeingizwa chaka mazima.
 
Vipengele vya mkataba vinatuingiza utumwani kwa kuuza nchi, watu wake na Sovereignity yetu, hoja ni hiyo
Mkataba upi wenye vipengele vinavyotuingiza utumwani?. Hiyo ndiyo kazi haramu inayofanywa na wanasheria kina Rugemeleza na Mwabukusi, kuwadanganya watu wakiwa na nia ovu kwa bandari na maslahi yake mapana.

Hakuna mkataba wowote uliosainiwa kwani mikataba ya kibiashara inatokana na makubaliano yaliyopitishwa na bunge. Azimio lililopita bungeni halina nguvu kulingana na kile kinachokwenda kuandikwa kwenye mikataba ya biashara inayokubalika na pande zote mbili na kuwa mwongozo wa biashara ya hapo TPA.
 
Kwahiyo nikisaini mkataba leo halafu kesho ukafuatia mkataba mwingine, automatically uke mkataba wa mwanzo unabadilika na kuwa makubaliano, si ndio?

Kwamba mlichosaini na kupitisha bungeni ni mkataba, ila mkijankisaini mkataba mwingine ndio huu utabadilika na kuwa makubaliano, sivyo?
Kilichosainiwa bungeni sio mkataba ni azimio la makubaliano ya kufanyika biashara ya pamoja kati ya DP na Tanzania.

Mikataba itakwenda kuandikwa na kusainiwa baadae, ni baada ya majadiliano ya kina kuhusiana na uwekezaji utakaofanyika hapo bandarini.

Kilichopelekwa bungeni ni IGA, kinachosainiwa kwa ajili ya kufanyika kwa biashara kinaitwa HGA, ni vitu viwili tofauti.
 
Mkuu unajua hata logic wewe ndio umesema zamani kulikuwa na wizi sasa hivi mambo yamebadilika hence mikataba itakwenda sawa sawia sababu sasa hivi kila kitu ni Kosher....

Ndio nikakuuliza sasa hivi ambapo kila kitu ni Kosher mbona CAG anagundua madudu (au hio suggestion kwamba tusihofu sasa hivi kila kitu ni sawa inaishia wapi)?

Kwahio hayo madudu upigaji unaishia wapi ? Huku kwenye mikataba / Makubaliano hakuna madudu

Kwahio unadhani makubaliano yakiwa na tija zaidi kwetu ufanisi utaondoka ? Jaribu kutofautisha Makubaliano mazuri kwa manufaa ya wote, Utendaji mzuri / Mbovu na Makubaliano Mazuri na Utendaji mzuri..., Haimaanishi kupata makubaliano mazuri kunaondoa ufanisi (Yaani ufanisi lazima uendane na makubaliano mabaya - TICTS Makubaliano yalikuwa mabaya na Utendaji Mbaya - Haimaanishi tuingie makubaliano mabaya kwa ajili ya Utendaji Mzuri why not Vyote ?)
Ondoa wasiwasi na mashaka, amini nchi yako ipo katika mikono salama.

Wizi upo dunia nzima, hakuna serikali isiyo na ufisadi ndani yake kuanzia zile kubwa kina USA, Russia na sisi huku Tanzania.
 
Ondoa wasiwasi na mashaka, amini nchi yako ipo katika mikono salama.

Wizi upo dunia nzima, hakuna serikali isiyo na ufisadi ndani yake kuanzia zile kubwa kina USA, Russia na sisi huku Tanzania.
Kwamba wewe una uelewa wa sheria kuliko Shivji?Muda utaongea.
Uzuri pia tumeweka risiti ya hili.
 
Back
Top Bottom