Nimegundua Wanaume wengi huku JF ni Wapweke Mno na Wamekosa Utulivu

Hizo Zina kuaga ni genye...wala sio upweke.
Kuna watu wakiona hayo matrako hapo profile wanadhani ni real wanawaza kufokoa tuu.
 
Watu mko serious sana na JF 😹😹😹

Humu ingia kuchangamsha genge ukimaliza log off kaendelee na maisha yako mengine, yani upate sonona kwa fake IDs??

Afu umesema marafiki nini?
Utafute marafiki JF?? 😹😹
Naona unatafuta kudhalilishwa, kuna wenzio walikutana na watu humu wakaletwa na picha zao.
Hivyo wanavyokukataa ndo vizuri tena inatakiwa wakuogope kabisaa..!!
 
Shida yenu mnajionaga mnajua sana kulinda privacy zenu sijui. Kalaga baho namba zangu nawekaga hadharani na vigoli vimenitafutaga fresh tu. Jf hii mishangaz ndo mingi, miaka 10 mbele asilimia 75 ya wote wataanza kula mafao. Nisikilize mm
Mimi nishaanza kula mafao karibu shem 😹😹
 
πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚ Nimecheka
 
Uko sahihi,mtu anachati Hadi saa 6 usiku na saa kumi Yuko macho.

Hata hivyo jf kwangu ni sehemu ya burudani sihitaji watu physical kupata burudani.
 
Jf kwangu ni jumba la kujichotea maarifa na kurelax nikiwa free, muingiliano na watu haujawahi kuwa zaidi ya hapa jukwaani na lengo ni kuchangamsha genge na si vinginevyo.

Ukiwa na mipaka na ukaiheshimu na kuilinda mipaka yako ni raha sana, humu kuna baadhi sio wema kwahiyo ukijichanganya tu lazima ujute.

Humu ndio kuna wanaothibitisha ile methali ya umzaniaye ndiye kumbe sie. Kuweni makini na watu mnaojihusisha nao hasa mitandaoni.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…