Nimeibiwa kuku wa nyama

Nimeibiwa kuku wa nyama

Mbona kama ulivyoeleza ni simple kuwabaini. Kwani wanakuchanganyia wapi?
Atakuwa aliwaruhusu kuingia bandani kuchagua kuku mkuu hawa professional yao ni wizi kuna namna wanawakata wawili wawili kwa kasi ya ajabu kukuchanganya. Mm niliwahi kuona kwa mama yangu mdogo yaan alichukua kuku 40 ila nikaona mbona Banda kuku wamepungua sana tukapiga tanchi Tenga zitoke zihesabiwe upya alianzisha utata wa ajabu uzuri pale tulikuwaga vijana jirani wakaja pale tukakiamsha akadai atafidiwa muda wake anaopotezewa tukasema sawa huku tenga linafunguliwa tulikuta kuku 60 badala ya 40. Akadai tulikuwa tunahesabu ss yy alikuwa haesabu kuku anatoa tu
 
Asanteni 🙏🏽🙏🏽

Yan total waliyoniibia ni kuku 208
208x6500=1,352,000
Kiulainiiii kmmm


Yan wale wanatumia dawa plus kukuzubaisha kila mtu anakuongelesha huyu anakushauri hivi huyu hivi yani maneno mengi
Pole sana mkuu dah wakija wamejipanga na wamefanya survey
 
Asubuhi ya leo nimeibiwa kuku wa nyama 200+ na wababa wa tano tena wana nguvu zao tu jamani😭😭😭

Alikuja mmoja na boda akasema nataka kuku 100, kaja saa12 alfajir akasema ngoja nikachukue tenga

Kurudi kaja na wababa 4 wana pickup nyeupe😭😭😭😭😭😭😭😭😭

Wezi wenyewe hao hapo
Mbona hujui kujieleza umendiaka niini saa 9 za usiku alafu tena saa12 ?
 
Tulikua wawili

Wana mbinu plus madawa sijui imekuwaje yani😭😭😭😭
Pole sana...hakuna madawa, ni mbinu tu...........inahitaji uzoefu kujua michezo hiyo........wakati nafanya hiyo biashara, mimi au kijana wangu ni lazima kukaa kwenye mlango wa banda na kuhesabu kila kuku anayetolewa nje......
 
Hapo unatakiwa kuhesabu mwenyewe unampa kuku mmoja mmoja akiwa mita Tano nje ya banda.ukimruhusu kuingia bandani utaibiwa na kuleta magonjwa kwenye Banda lako
ni kweli ila huyu mtoa mada aliwaruhusu wote au zaidi ya wawili kuingia bandani akawa anawahesabu wakiwa mikononi mwao..
 
Pole aisee,matukio ya namna hii yanakatisha tamaa.Jivike ujasiri.Naamini haitatokea uibiwe kwa style hii .
 
Kwa uzoefu wangu wa kesi aina yako hao Watu wamekutaperi...!
Uliamini kiia walichokua wanakwambia, ila unaweza kuwakamata vile picha unazo, ila SIo kazi Ndogo.
 
Back
Top Bottom