Nimeona clip ya Mtanzania mwenzetu Joshua Mollel anauawa na Hamas. Inatia hasira kuona tulipiga kura kuwaunga mkono
Ikirushwa humu video inayoonyesha alivyouwawa Ben Saanane basi wote hum mtabak vinywa wazi.

Tunapowashutum Hamas huku tukiwachekea wakina Makonda inashangaza.

Kama kuuliwa kikatili basi hakuna anayemfikia marehem Daud Mwangosi.
 
Upstairs uko sawa kweli? Magaidi wa Hamas wanachafuliwaje?

Hebu tueleze nini kilichotokea October 7?
Ile scanario ya kutekwa wengi wanadai palikuwa na Tamasha mambo ya show na hapo palikuwa na raia wa kigeni kibao .

Hata rocket za Hamas ziliua watu wachache na inakadiriwa mateka 200 na kitu walichuliwa ni kutokana na yule dogo aliyetoa ushuhuda ni Mtanzania ..

Inakuwaje pawe na special treatment wote wachukuliwa vizuri halafu huyu wamammalize na mwili wake waondoke nao ,mpaka sasa wanasema mwili upo kwa Hamas sasa ngoja tuone?

Kumbuka HAMAS walisharelease mateka kweny batch ya kwanza ,sasa iwejw wabaki na maiti!?
 
Kabisa, chupi itakuwa ilimponza, kiarabu sikijui ila nasikia neno elshabaab yaani ewe kijana!
Ni kweli, ile chupi ya kijeshi ilimponza sana. Vijana tuache kujifanya wajeda. Kibaya hata kama angewaeleza shida hamas wameumizwa mno tena sana na mashushushu wa mosad.
 
Unawajua Waisrael wewe au unaropoka umeona hiyo boxer ya kijeshi umejilizq kaavaa kwa makusudi haraffu Watanzania wengi wanafiki sana watoto 8000 waliouliwa Gaza hawana thamani zaidi ya Joshua? Au wale watoto ni Hamas hawana haki ya kuishi? Serikali inajua kila kitu ndiyo maaana imekaa kimya.
Yale ni magaidi. Kitoto cha miaka 3 kinafundishwa kuchinja hayo ni magaidi na yanastahili kuuawa ili amani iwepo. Mtu mwenye akili timamu hawezi kufundishwa kuvaa mabomu.
 
Nasikitika sana naungana na wazazi wa Joshua Mollel kuhusiana na kifo cha mtanzania mwenzetu..

Yapo maswali na sintofahamu nyingi na utata kuhusiana na taarifa za kifo cha Joshua ambapo si vibaya sisi kama watanzania tukahoji ingawa marehemu hatorudi lakini tusiwe ni kizazi cha kupokea tu bila kuhoji tutakuwa wajinga. Yapo mambo mawili ambayo yanahitaji ufafanuzi hapa.

Mosi huyu mtanzania mwenzetu tulipata taarifa kuwa amechukuliwa mateka na Hamas huko Gaza lakini leo tumeoneshwa hapa kuwa aliuwawa na Hamas nadhani tarehe 7.10.2923 ndani ya mipaka ya israeli.

Pili kama aliuwawa tangu tarehe 7.10.2023 kwanini serikali ya Israeli haikutoa taarifa ya kuuwawa kwake hadi leo walipotuletea hii clip?

Mwisho kabisa hii clip imekuja baada ya balozi wa palestina hapa nchini kuhojiwa na kituo cha radio cha clouds FM je kuna nini nyuma ya pazia? Naomba tujadili bila jazba wa mihemko.

Natoa Pole za dhati sana kwa familia ya Joshua Miller na watanzania wote kwa pamoja kwa kumpoteza Mtanzania mwenzetu.
Maswali kuhusu mateka wa Tanzania yapo mengi kuliko hayo na mengine serikali yenyewe ingepaswa kuyatolea ufafanuzi
.Hawa watanzania walikwenda kusoma au walikwenda kufanya kazi mashambani au kazi nyengine za usafi majumbani .Kama walikwenda kusoma walipelekwa chuo gani cha kilimo.
Siku ya tarehe 7 oktoba walikuwa maeneo gani ya Israel.Isijekuwa walikamatwa ndani ya kambi za jeshi za Israel na hivyo Hamas wakawachukulia ni askari wa kawaida wa Israel.Kwa sababu kama hawakwenda kusoma yawezekana walikuwa ndani ya kambi wakifanya kazi nyengine.
Maswali hayo serikali inaweza kujibu kwa kushirikiana na balozi wa Tanzania nchini Israel au na balozi wa Israel nchini Tanzania.
 
Habari wazalendo wa kitanzania. Video hii nimeipata IG kiukweli nina mixed emotions. Nina hasira na masikitiko makubwa kupita kiasi. Ewe mtanzania mzalendo wa nchi tuweke mbali udini etc ni kitu kilichoniumzia roho mno. Hii video inamuonyesha Joshua Mollel akitekwa na Hamas. All the deniers sijui nawasaidia vipi. Huyu alikuwa ndugu yetu. RIP Joshua. My heart bleeds kwa hii familia

View attachment 2845298
Msijizime data,


Kumbukeni hiyo ni vita na vita hii ina historia ya muda mrefu

Kwenye uwanja wa vita lolote linaweza kutokea, hata hao palestina wengi tu wameuliwa hata kabla ya vita iliyoanza karibuni, hivyo hapo hamna kuaminiana

Ndio maana unakuta hadi waandishi wa habari wengi wanauliwa tu.


Mimi sidhani kama kuna mtu ambaye anafurahia mauaji kama haya, ila napinga watu kuchukulia hamasa za kidini na kuona kundi fulani ni magaidi na kundi lingine ni wema.



Hao jamaa na waisraeli wote ni magaidi na wanachokifanya hakikubaliki.


Shida kubwa inakuja watu wengi wanaketa hamasa za kidini kwenye jambo serious kama hili.
 
Maswali kuhusu mateka wa Tanzania yapo mengi kuliko hayo na mengine serikali yenyewe ingepaswa kuyatolea ufafanuzi
.Hawa watanzania walikwenda kusoma au walikwenda kufanya kazi mashambani au kazi nyengine za usafi majumbani .Kama walikwenda kusoma walipelekwa chuo gani cha kilimo.
Siku ya tarehe 7 oktoba walikuwa maeneo gani ya Israel.Isijekuwa walikamatwa ndani ya kambi za jeshi za Israel na hivyo Hamas wakawachukulia ni askari wa kawaida wa Israel.Kwa sababu kama hawakwenda kusoma yawezekana walikuwa ndani ya kambi wakifanya kazi nyengine.
Maswali hayo serikali inaweza kujibu kwa kushirikiana na balozi wa Tanzania nchini Israel au na balozi wa Israel nchini Tanzania.
Serikali yetu imeshindwa kuchukua hatua za uhakika juu ya watu wetu.pia nathubutu kusema hata kama tungekua na mateka wengi huko israeli naamini wangekufa tusingeweza kuwakomboa . Tumekua ni serikali ya kupokea kila tunachoambiwa badala ya ku demand.
 
Yale ni magaidi. Kitoto cha miaka 3 kinafundishwa kuchinja hayo ni magaidi na yanastahili kuuawa ili amani iwepo. Mtu mwenye akili timamu hawezi kufundishwa kuvaa mabomu.
Na hawa hapa mabawana zako?
 

Attachments

  • IMG_8244.jpeg
    IMG_8244.jpeg
    70.7 KB · Views: 3
  • IMG_8243.jpeg
    IMG_8243.jpeg
    48.9 KB · Views: 3
  • IMG_8245.jpeg
    IMG_8245.jpeg
    74.7 KB · Views: 1
Back
Top Bottom