Nimepata mtoto wa kiume usiku huu, baada ya kuwa kwenye ndoa kwa zaidi ya miaka 7

Endelea kubarikiwa
 
Amina.
Hongera sana.
 
Kweli dunia vurugu. Wewe unafurahia wakati hapa mimi nimevurugwwa wife hazioni siku zake week ya pili sasa.
Nahis kuvurugwa kwel kwel yan
Shuda ni kwamba kwa umri wangu wa 35 years sasa nilisha plan sitaki tena mtoto.
NB
nasisitiza ni wife, mke wangu wa miaka 14 sasa na tuna watoto wa 4.
 
Mkuu ushauri wote uchukue ila masuala ya kupima DNA ya puuze kabisa utatengeneza tatizo kubwa la kudumu kati yako na mke wako, la kutoaminiana tena upendo utaondoka.
Kawaida tu, hata bila DNA maisha ya sasa tatizo la kuaminiana ni kubwa sana. Na hata hivyo hupaswi kumuamini mwenza wako 100%
 

Kufanya DNA ni kupoteza muda tu. Hata kama mtoto si wake, ataambiwa ni wa kwake.

Atulie na amlee huyo malaika.
 
Hongera sana kwa Zawadi ya mtoto, hongera pia kutambua uwepo wa Mungu katika kupata kwako mtoto. BWANA amtunze mwanao, akue vyema, awe na afya njema.
 
yani watu hawakwepeshi🤣🤣ni huzuni kwakwel
Bora ukwel unao huzunisha kuliko kujifurahisha kwa uongo. Hii hua ni suala la kitambo kifupi.

Shida hajaeleza tatizo hasa lilikuaje before walitumia njia gani kukabiliana nalo, nani kati yao alikua na changamoto na changamoto hiyo ilikua ipi?
Wakachukua hatua gani mpaka kufikia hitimisho la matokeo ya mimba.

Anaweza akaona sio muhim ila alipaswa kuandika humu maana angesaidia wengi ambao mpaka sasa huenda wana shida kama aliokua nayo yeye
 
Dah, Una wivu
Sitakujibu mengi isipokuwa jibu Moja tu.

Anza wewe kunionyesha majibu ya DNA aliyopima baba Ako kujihakikishia kuwa wewe ni mwanae mzazi.

Kama hayapo basi pongezi Kwa mama yako kukaa na Siri hiyo Kwa miaka mingi.
Tafiti nyingi sana zinaonyesha kwamba kiini au chanzo cha Migogoro mingi sana pamoja na vyanzo vya ugomvi au Mauaji kwa wanandoa wengi sana hapa duniani ni wivu wa mapenzi, kukosa uaminifu katika ndoa (infidelity) au Wanaume kubambikiwa watoto ambao kimsingi sio watoto wao halisi wa kuwazaa (not biological Fathers). Visa vingi sana vya Mauaji ya wanandoa hususani kwa akina mama na watoto wao huwa vinahusiana na suala la hili la Wanaume kubambikiwa watoto, mambo yanapokuja kujulikana hadharani wakati tayari mwanaume ameshaingia gharama kubwa katika malezi ya watoto ambao baadaye inakuja kuthibitika kuwa siyo wake matokeo yake huwa ni mabaya Sana kupita kiasi.
Hivyo basi, njia pekee ya kuweza kuepukana na dhahama au mabalaa kama hayo ya Mauaji kwa wanandoa ni kuchukua tahadhari kubwa katika hatua za mapema, yaani kuwapima DNA watoto wanaozaliwa, Kama matokeo yatakuja tofauti kabisa na matarajii, basi mwanaume atakuwa na nafasi ya kuweza kujiepusha na gharama zisizomhusu za malezi ya watoto ambao siyo wake. Aidha, mtoto husika ataweza kupata malezi kutoka kwa baba yake halisi. Na mwisho kabisa, kupima DNA Mapema pia itasaidia Wanandoa kuwaepusha na janga kubwa la Migogoro ya hatari kati yao ambayo mara nyingi sana husababisha madhara makubwa sana yasiyorekebishika ktk siku za usoni, ikiwamo na mifarakano mikubwa na Vifo.

Kinga ni Bora kuliko Tiba, Kupanga ni Kuchagua!
The choice is yours.
 
Hongera sana mkuu.
Ningekua karibu ningekuja kuchukua baraka za huyo mtoto.
 
Aaaah wajameni mwacheni mwenzenu afurahi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…