Nimesikitika baada ya kuona Nigeria ina GDP karibu mara tano ya Tanzania

Nchi gani Afrika inayoongoza kwa GDP per capita?
GDP per capital haileti maendeleo kwa wananchi wake, haileti miundombinu bora, haileti ajira, haileti heshima, haijengi uchumi wa nchi.

GDP per capita inaleta heshima kwa mtu mmoja mmoja tena ni kama fake average, tumia akili wewe, matajiri maia moja wa Dar wana neutralize umaskini wa watu milion 5 wa Dar na wote wanaonekana kama wanakipato cha wastani kumbe matajiri wakubwa wachache wameficha umaskini wa watu milioni 5, nakuonaga una mantiki muda mwingine kumbe huna unalojua.
 
Ili uwe na per Capita kubwa ambayo in turn ita define welfare lazima ukuze GDP ni lazima sio ombi.

So Nigeria imetuzidi GDP na per Capita
Wafundishe hao, naona wanakomalia vitu vya ovyo, China ana GDP per capita ndogo sana lakini kwanini anahesabika kama taifa namba mbili lenye uchumi mkubwa na ana miundombinu bora na viwanda vilivyotukuka, tukuze GDP tuache porojo tutumie vema rasilimali zetu zituinue kiuchumi.
 
Mbona hujanitajia nchi zinazoongiza kwa GDP per capita barani Afrika?
 
Mbona hujanitajia nchi zinazoongiza kwa GDP per capita barani Afrika?
Siwezi kukutajia vinchi vidogo vidogo hivyo venye watu milioni moja au laki tano huto ni sawa na wilaya uyui, unataka kulinganisha baba anayelisha familia ya watoto 50 na baba mwenye familia ya mtoto mmoja.
 
Unasikitikia GDP? are you seven serious? Ebu angalia GDP ya Belarus na Mauritius. Na hizo nchi kwenye Human Index Development wametuzidi wote, sio Nigeria, sio Tanzania.

Mauritius ni ya kwanza Afrika.
 
Mbona Kenya Ina IDADI ya watu ndogo kuliko tanzania.

Ila Kenya Ina uchumi imara Africa mashariki nzima.


Kwanini Tanzania yenye IDADI kubwa ya watu isiwe na uchumi mkubwa kuliko Kenya
 
Naam,

Na hata hiyo GDP per capita nayo, hesabu zake ni za average.

Average zinaficha umasikini wa wengi kutokana na utajiri wa wachache.

Twende kwa namba.

Aliko Dangote anakadiriwa kuwa na utajiri wa dola za Kimarekani 10.1 bilioni.

GDP per capita ya Nigeria ni dola za Kimarekani 2066 per 2021 figures.

Ukifanya $ 10,100,000,000 divide by 2066, to see how many people Aliko Dangote alone pulls from zero dollar to 2066 dollars, unapata watu 4,888,673 wa 4,888,674 akiwa Aliko Dangote mwenyewe.

Utajiri wa Aliko Dangote peke yake, unawainua watu wa Nigeria almost 4.9 million kutoka 0 US dollar per capita GDP to $ 2066 per capita GDP.

Na Nigeria kuna mabilionea kadhaa na mamilionea wa US dollar wa kumwaga.

Maana yake nini?

Maana yake hata hiyo GDP per capita ambayo ni average, inakuwa si realistic, watu wachache wanaibeba inakuwa juu sana, wakati watu wengi wanaishi uchumi wa dola mbili kwa siku.

Aliko Dangote peke yake anainyanyua takriban asilimia 2.3 ya nchi nzima ya Nigeria kutoka GDP per capita ya 0 mpaka $2066 !
 
Kumbe nchi yetu imezidiwa kiasi hiki na nchi yenye boko haram? Yaani kweli wao wanakaribia gdp ya bilioni 400 usd wakati sisi tupo kwenye bilioni 80s usd?
HV shule ulikwenda kusomeaa ujinga nn

HV kwa akili zako za kawida unafikiri wale jamaa Wana akili Kama za Huku

Kwa kutazama tu wako watu milion 220 Ni lzm wakuzid uchumi na gdp yako [emoji1787] Tena unaambiwa Nigeria ndio taifa lenye watu kila pembe za dunia kuzaka fursa
 
Wingi wa watu unapoleta kugombea maliasili chache ni lazima akili zifanye kazi ili mkono uende kinywani, kule kugombea kidogo kinachokuwepo kunatengeneza mfumo rafiki wa kubadili hali za kimaisha za watu.

Mfumo wa elimu unabadilika Tanzania, kwa sababu ya wingi wa watu na wengi wao ni masikini. Mifumo ya kushughulika na afya na yenyewe inabadilika kulingana na ukweli kuwa idadi ya watu inaongezeka.

Kilimo kinakwenda kuwa cha kisasa na cha kisayansi, sababu ni changamoto ya uongezeko la watu.

Tupo milioni 64 mwaka huu, mwaka 1985 tulikuwa milioni 20 tu, mengi yanaendelea kubadilika kwenye mifumo yetu ya kimaisha na hii ni changamoto isiyokwepeka.

Nakataa kwamba hakuna kinachofanywa na serikali licha ya wingi wa watu kuongezeka mahitaji yao ya kila siku.
 
Hoja ni Ukubwa wa GDP na sio impacts ya GDP kwenye uchumi.

Uchumi wa Nigeria ni mkubwa mara 6 ya Tanzania.
Ukubwa wa uchumi si hoja, uchumi unaweza kuwa mkubwa lakini una watu wengi wanagawana, hauna ufanisi na nchi ni masikini, wakati pengine pana uchumi mdogo, watu wachache, wenye ufanisi na nchi ni tajiri.

Ugali wa kilo moja unaogawanywa kwa watu 100 kiasi kila mtu ale tonge moja tu ukaisha haushibishi kuliko ugali wa robo kilo anaokula mtu mmoja akashiba na kuuacha.

Sasa hesabu za kuangalia ukubwa wa ugali bila kuangalia watu wanaokula huo ugali zinaweza kukufanya uone ule ugali wa kilo moja kwa kuwa ni mkubwa, ndio mzuri zaidi kushibisha, ukaenda huko, ukakuta unakula tonge moja tu.
 
Nigeria imetuzidi vyote
 
[emoji3][emoji3][emoji3]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…