Nina milioni 25, naweza kuwekeza kwenye nini ili nipate pesa nzuri kwa muda mfupi?

Nina milioni 25, naweza kuwekeza kwenye nini ili nipate pesa nzuri kwa muda mfupi?

Yaani watu walivyowasumbufu kwenye kulipa,sijui wakopeshaji wanatumia mbinu gani kupata faida..mikopo ya kukatwa juu kwa juu ndo atleast aisee
Inabidi hii biashara usali sana sana...Ila STONE katibua kinoma, hali haikuwa hivi[emoji848]

Ila ni biashara nzuri ukipata watu waaminifu
 
Naomba uielezee hii mkuu
Yanakua ni kifusi kikubwa sana mfano wa hata nyumba,wanakua wanayauza unacho Fanya unachukua sample kwenye rundo linalo uzwa unaenda kulipima kwa mkemia mkuu kujua lime contains kiwango gani cha madini,majibu yanayo toka yanaonyesha kiwango cha copper,silver na gold kilichopo ndani ya rudio,na majibu unaweza kadiria utapata gold kiasi gani,unanunua marudio unayasomba na maroli unapeleka illusion (plant) yanaenda kuozeshwa na carbon (electrolysis process) extraction of gold

Unapata Mali yako pure gold,unaingia sokoni,kama una mtaji..Illusion inatumia wiki mbili hadi NNE kuozesha inategemea na kiasi cha wingi ya marudio yako na kwa hii process ni ngumu sana kupoteza hela..Makadirio ya chini milioni 7 kila wiki mbili so itakua mil 14 kwa mwezi makadirio ya chini ila unaweza pata hadi mil 30 kama marundo yanasoma vizuri....
 

Attachments

  • VID-20210326-WA0010.mp4
    5.1 MB
Anzisha kampuni ya kujenga makaburi, utatengeneza pesa hadi uchanganyikiwe, hutaamini macho yako; yaani watu kwenye kujengea makaburi huwa hawataki hata kubargain bei, Ukimwambia kaburi milion 6 anakwambia nipe account namba. Mfano waliojenga kaburi la JPM, wale washakuwa matajiri tayari, kwa ile kazi moja tu. Nenda Instagram uone watu wanavyopiga mpunga kimasikhara
Haaa na jamaa yangu alikua mojawapo ya walio piga hiyo kazi walio faidi ni wakubwa tu ova
 
kwahyo unamjua atakae lipa na asie lipa kwa kumuangalia usoni??

Ni hivi, namkopesha mtu ninaefahamiana nae vizuri na ninamjua mzunguko wake wa pesa vizuri, pia kwenye kikoba watu wakitaka kuchukua mikopo na hawana hisa mimi nawakopesha wakichukua mikopo nakata hela yangu.

Kingine kwa mtu nisiemfahamu kama kaletwa na mtu mimi simuandiki jina yule mteja namuandika yule aliemleta so nitamdai aliemleta.

tatu sikopeshi zaidi ya milioni mbili kwa mtu mmoja na siruhusu mtu kutop up mkopo.

unaruhusiwa kulipa riba mwezi mmoja tu, siruhusu mtu kukaa na hela zaidi ya miezi miwili.

Toka nianze ni miezi 11 sasa na sijawahi dhulumiwa na mtaji wangu usharudi zamani.

Nadhani nimejitahidi kukujibu
 
Ndugu yangu aliuza nyumba ya urithi Mikocheni, akaenda kununua nyumba Sinza, akafungua studio ya kurekodi muziki, Hadi leo sijawahi kusikia redioni wimbo kutoka studio yake, sijui zinapigwa kwenye space station anga za mbali?!?!¿‽‽[emoji848][emoji848][emoji848]
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Fanya biashara bubu ya kukopesha Ila wateja wawe waaminifu .
Naona watu wengi mnamshauri hivi..yan ukitaka kufanya biashara ya kukopesha unatakiwa uwe Mchawi au Mcha Mungu sana la sivyo wakopeshaji watakusahaulisha madeni yao.
 
Back
Top Bottom