Nipo tayari kutoa milioni 5 kwa mtu atakayenionyesha hili andiko

Ubatizo ulikuwa unakuuganisha na mauti aliyopitia Yesu msalabani ila haikufanyi uzaliwe upya kama inavyofundishwa ila shida na mateso aliyopitia Yesu utapitia maana umeunganishwa na mauti yake.
 
Amina..Ubarikiwe sana
 
Kama haukubaliani na mitume. Nenda kwenye biblia yako unayoiamini, ondoa vitabu vyote vilivyoandikwa na mitume ubakiwe na Yesu tuu mkuu. Siwezi kujibu maelezo yako uliyomezeshwa mkuu
Huwezi kujibu kwa sababu ni ukweli usiopingika. Mitume hawana ubavu wa kubadili agizo la aliyewatuma.
Yohana 13:16
Amin, amin, nawaambia ninyi, Mtumwa si mkuu kuliko bwana wake; wala mtume si mkuu kuliko yeye aliyemtuma.
Kama hukubaliani na agizo la Yesu, nenda kwenye biblia yako unayoiamini, ondoa Maandiko yote aliyonena Yesu ubakiwe na ya mitume tuu, mkuu, halafu subiri siku ya mwisho uone kama Yesu hatakuambia maneno haya:
Lk 13:27
Naye atasema, Nawaambia, Siwajui mtokako; ondokeni kwangu ninyi nyote mlio wafanyaji wa udhalimu.
 
Sawa
 
Hakuna katika biblia nzima mahali mtu amebatizwa hivyo..... batizo zote ni kwa Jina la Bwana Yesu Kristo
 
Siyo kila kitu kipo kwenye Biblia. Mambo mengine yameanza baada ya Biblia kuandikwa
 
Sawa, hebu useme ni kwanini Mtume Petro na wengine wote walibatiza kwa Jina Yesu Kristo?
 
Kama haukubaliani na mitume. Nenda kwenye biblia yako unayoiamini, ondoa vitabu vyote vilivyoandikwa na mitume ubakiwe na Yesu tuu mkuu. Siwezi kujibu maelezo yako uliyomezeshwa mkuu
Mt 28:19 (SUV)
Basi, enendeni, mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi, mkiwabatiza kwa jina la Baba, na Mwana, na Roho Mtakatifu; na kuwafundisha kuyashika yote niliyowaamuru ninyi; na tazama, mimi nipo pamoja nanyi siku zote, hata ukamilifu wa dahari.

Agizo la kubatiza kwa jina la Baba, na Mwana, na Roho Mtakatifu linaendana na agizo la kuwafundisha wanafunzi(mataifa yote) kuyashika YOTE aliyoyaamuru Yesu. Wewe ni nani unayetaka tuache kuyashika aliyoyaamuru Yesu, badala yake tufuate ya mitume?
 
Ongeza Ela nkuonueshe mkuu,
Million 5 Ni pesa ndogo sn kunipekulisha biblia
 
Vipi kakupa 5M yako
 
Kwahiyo mitume wakaona wachague kwa jina la Yesu nawakati boss wao aliwaambia kwa jina la Baba, Mwana na Roho. Asante kwa kushiriki mkuu
Walifanya Kama vile “jamhuri ya muungano wa Tanzania … kazi iendelee”… kibwagizo hicho
 
Hakuna haja ya kulumbana.
Kwa jina la baba, mwana na Roho Mtakatifu= Jesus.
Msifanye mambo kuwa magumu.
Yesu aliwaagiza wakabatize kwa jina la baba mwana na Roho Mtakatifu ila mitume wakampa heshima yote wakijua yeye ndiye Mungu mwenyewe mkuu.
Anayebatiza kwa jina la baba mwana na Roho Mtakatifu hafanyi dhambi ila anayebatiza kwa jina la Yesu huyo amepata ufahamu zaidi na kumtambua Mungu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…