Nipo tayari kutoa milioni 5 kwa mtu atakayenionyesha hili andiko

Kwa jina la Baba na la Mwana na la Roho Mtakatifu
Mkuu umejibu vyema, me nakupa mfano mdogo tuu.
Tuna Rais ambaye ndie kiongozi wa nchi, Huyo huyo ni amiri Jeshi mkuu. Huyo huyo ni mwenyekiti wa chama tawala.
Sasa Rais ni jina? Ni cheo
Amiri jeshi ni jina? Ni cheo
Mwenyekiti wa chama ni jina? Ni cheo
Jina lake ni Samia Suluhu

Unaposema kwa jina la Baba, Baba sio jina ni cheo. Mwana sio jina ni cheo, Roho Mtakatifu sio jina ni cheo, Jina ni moja tu nalo ni Jina la YESU KRISTO.

Usiwe na wasiwasi kwamba itakuwaje Sasa,unaweza rudia tena kubatizwa na hakikisha unabatizwa kwa jina la Yesu Kristo. Soma Matendo ya Mitume 19:1-7 utapata kitu.
 
Kabla ya Yesu watu walibatizwa kwa jina gani?
 
Nashukuru mkuu, hatulumbani bali tunaelekezana. Tunaweza kupata andiko linalosema mtu akibatizwa kwa jina la Baba na Mwana na Roho Mtakatifu na aliyebatizwa kwa jina la Yesu Kristo ni sawa. Mimi kwa uelewa wangu mdogo ni kwamba kipindi Yesu yupo hapa duniani Kuna mambo alikua akiwafunulia wanafunzi wake lakini walikua haelewi na ndio maana baada ya makutano kutawanyika, walikua wakimuendea jioni au usiku kumuuliza juu ya Yale aliyokuwa akiyaongea katika makutano. Alipoondoka duniani aliwaahidi kuto waacha Yatima akiwatumia Roho Mtakatifu ili awafunulie Yale aliyokuwa amewaagiza kufanya. Na ndio maana utaona Yesu aliwaagiza wakahubiri ulimwengu kwote wakiwabatiza watu kwa jina la Baba na Mwana na Roho Mtakatifu lakini waliposhukiwa na Roho Mtakatifu aliwafunulia kwamba ubatizo ni kwa jina la Yesu Kristo.
 
Umemjibu vyema sana kwa kuongezea kutoka kwenye neno la msingi la agizo la yesu pale mathayo 28:19
Wanafunzi walipokuwa wanasema watu wabatizwe kwa jina la yesu , kwa lugha na tafsili za kale ilikuwa na maana ya agizo la yesu kwa namna mbalimbali baadhi ya maneno linapotumia neno jina
Matendi 4:7
Matendo 9:29
 
Kubatizwa kwa Jina la Yesu maana yake ni kubatizwa kama Yesu alivyoagiza SIO kubatizwa kwa Jina moja la Yesu.
Watu wanaofundisha kubatizwa kwa Jina la Yesu tu hawaamini pia kuwa Mungu ana nafsi tatu: Mungu Baba, Mungu Mwana na Mungu Roho Mtakatifu. Watu hawa wanadai Utatu ni fundisho la kibinadamu lisilo la kibiblia! Wenye imani hiyo bila shaka ni wavivu wa kusoma Biblia maana mafundisho ya Utatu yako wazi kabisa.
 
Hakuna mahali katika Biblia ambapo majina ya wanafunzi au watu fulani yameorodheshwa moja kwa moja kwamba walibatizwa kwa fomula kamili ya “kwa Jina la Baba, Mwana na Roho Mtakatifu” kama ilivyoandikwa kwenye Mathayo 28:19. Hata hivyo, agizo hili la Yesu ndilo msingi wa ubatizo wa Kikristo, na kanisa la kwanza lilitekeleza agizo hili.
Katika Matendo ya Mitume, watu wengi walibatizwa baada ya kuamini, kama vile wale 3,000 siku ya Pentekoste (Matendo 2:41), lakini maandiko yanasema walibatizwa “kwa jina la Yesu Kristo”. Hii haimaanishi walipuuzia agizo la Mathayo 28:19, bali walikuwa Wayahudi waliomtambua tayari Mungu Baba na Roho Mtakatifu; walihitaji tu kumkiri Yesu kama Masihi.
Kwa hiyo:
• Watu waliobatizwa siku ya Pentekoste (takriban 3,000), na wengine waliotajwa katika Matendo (kama Kornelio, Towashi wa Ethiopia, na wengine), walibatizwa kwa utambuzi wa Baba, Mwana na Roho Mtakatifu, ingawa mara nyingi maandiko yanataja “kwa jina la Yesu” kama msisitizo wa imani yao mpya kwa Kristo.
• Hakuna orodha ya majina binafsi ya watu walioandikwa walibatizwa kwa fomula kamili ya Mathayo 28:19, lakini Wakristo wote wapya walifuata agizo hilo la Yesu.
Kwa muhtasari, Biblia haitaji majina ya watu mmoja mmoja waliobatizwa kwa maneno hayo kamili, lakini inathibitisha kwamba kanisa la kwanza lilifuata agizo la Yesu la kubatiza kwa jina la Baba, Mwana na Roho Mtakatifu
 
MKuu kama Yesu aliwaagiza wanafunzi wabatize ina maana wanafunzi walitii agizo hilo kama kawaida. Mathayo 28:18

Jaribu kutoka kwenye box. Hizo m5 baki nazo
 
MKuu kama Yesu aliwaagiza wanafunzi wabatize ina maana wanafunzi walitii agizo hilo kama kawaida. Mathayo 28:18

Jaribu kutoka kwenye box. Hizo m5 baki nazo
Nashukuru mkuu, sio kwamba wanafunzi hawakutii agizo la kubatiza, ila walibatiza kwa Jina na wala sio majina..nauliza tuu jina la Baba ni lipi? Jina la Mwana ni lipi? Na Jina la Roho Mtakatifu ni lipi?
NB: Hela nitabaki nayo kwasababu hakuna mtu kwenye biblia aliyebatizwa kwa jina la Baba na Mwana na Roho Mtakatifu wala hakuna kitu ktu kinachoitwa utatu. Mtakatifu
 
Sasa mkuu kwa maelezo haya huoni kwamba biblia inatambua ubatizo kwa jina la Yesu Kristo na sio kwa jina la Baba na Mwana na Roho Mtakatifu?
 
Hakunaababa si jina wala.mwaana wala roho mtakatifu.
Wote walibatizwa kwa jina la yesu kristo.
Peepo tu hatoki kwa jina la baba na mwana na roho.

Lolote mfanyalo kwa neno ama kwatendo fanyeni kwa jina la Bwana yesu kristo
 
Baba jina lako ulilonipa nami nawapa.
Jna la baba ni yesu kristo
 
Hakunaababa si jina wala.mwaana wala roho mtakatifu.
Wote walibatizwa kwa jina la yesu kristo.
Peepo tu hatoki kwa jina la baba na mwana na roho.

Lolote mfanyalo kwa neno ama kwatendo fanyeni kwa jina la Bwana yesu kristo
Nimekuelewa sana mkuu. Kama wanaamini katika utatu Mtakatifu, wakemee pepo kwa utatu Mtakatifu.
 
Hakunaababa si jina wala.mwaana wala roho mtakatifu.
Wote walibatizwa kwa jina la yesu kristo.
Peepo tu hatoki kwa jina la baba na mwana na roho.

Lolote mfanyalo kwa neno ama kwatendo fanyeni kwa jina la Bwana yesu kristo
Mimi naweza kutoa pepo kwa jina la baba na mwana na roho kinacho angaliwa ni imani sio jina, ndio maana kuna watu wanaweza kutumia jina la yesu na pepo lisiondoke pia usikalili msingi ni imani, mungu ni mwelewa sana anasikia na atatenda kutokana na imani yako hata ukitumia mungu wa Ibrahim wa usaka na yakabo pepo litakimbia.
 
Wewe ndie unaekalili na kuaminishwa isivyo mkuu. Nionyeshe andiko katika biblia linalounga mkono hoja yako.

Mimi naanza na hili
Marko 16:16-18
16 Aaminiye na kubatizwa ataokoka; asiyeamini, atahukumiwa.

17 Na ishara hizi zitafuatana na hao waaminio; kwa jina langu watatoa pepo; watasema kwa lugha mpya;

18 watashika nyoka; hata wakinywa kitu cha kufisha, hakitawadhuru kabisa; wataweka mikono yao juu ya wagonjwa, nao watapata afya.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…