Njia rahisi inayoweza kumsaidia mwanamke aliyepo kwenye uchumba sugu, kupata ndoa

Wadada wenye uchumba sugu.

Kuna wadada wapo kwenye mahusiano zaidi ya miaka kadhaa, na wanatamani waolewe; lakini wanaume walionao bado wanawapiga dana dana.

Njia rahisi inayoweza kukusaidia, mwanaume wako afanye maamuzi ya haraka katika kukuoa, fanya hivi:-
  • Andaa bajeti ndogo ya laki mbili n.k
  • Mtoe 'out' mpenzi wako
  • Tafuta eneo tulivu, inaweza kuwa hotel yenye eneo kubwa, au sehemu yoyote wanazotoa huduma zote za chakula, vinywaji, malazi n.k
  • Tafuta meza ya nje iliyojitenga, yaani muwe wenyewe tu au kuwe na umbali kufikia meza nyingine.
  • Itakuwa vizuri zaidi kama itakuwa ni usiku
  • Agiza vinywaji vingi ili muhudumu asiwe anakuja mara kwa mara kwenye meza yenu.
  • Pia hakikisha umevaa nguo nzuri, inayomtamanisha mpenzi wako.
  • Pigeni stori za kawaida, ila mkifika chupa ya nne anza kuongea kwa hisia kwa kumuonyesha umuhimu wa mpenzi wako katika maisha yako.
  • Mpigie magoti huku ukitoa maneno ya mahaba ukiigiza kama unataka kulia, na kumuomba aweze kukusitiri katika ndoa.
  • Mlilie mpaka yeye mwenyewe aanze kulengwa na machozi, na hatimaye yeye mwenyewe atakuinua na kukumbatia, na atakupa jibu lako.
  • Baada ya kufanya hivyo, deka kama mtoto mdogo ikiwezekana uwe unamkalia kalia, huku mkiendelea kupata vinywaji.
  • Mkimaliza hapo, nendeni chumbani mkapumzike.
  • Kesho yake anza kutekeleza mlichoafikiana.
  • Baada ya hapo nawatakia ndoa njema.
[emoji16][emoji16][emoji16][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787] kummmmk ndoa imekuwa Almas

Makiwendo
Dinazarde
 
Unamkopesha tu kwenye ndoa nyie ni mwili mmoja, halafu siku hizi mmerahisha wenyewe na mambo yenu ya haki sawa yaani 50/50.

Kama ikiwezeka wewe unalipa nusu na yeye nusu na kama hana nusu unamkopesha mwenzio,ili mfunge ndoa ndoa ni jambo la heriiiiiii binti halihitaji kusubiri kama nafasi ipo malizeni mengine yata fahamika mbele kwa mbele...................😎😎😎😉😉

Tehetehetehe....tehe.
Nikopeshe 100k
 
Wadada wenye uchumba sugu.

Kuna wadada wapo kwenye mahusiano zaidi ya miaka kadhaa, na wanatamani waolewe; lakini wanaume walionao bado wanawapiga dana dana.

Njia rahisi inayoweza kukusaidia, mwanaume wako afanye maamuzi ya haraka katika kukuoa, fanya hivi:-
  • Andaa bajeti ndogo ya laki mbili n.k
  • Mtoe 'out' mpenzi wako
  • Tafuta eneo tulivu, inaweza kuwa hotel yenye eneo kubwa, au sehemu yoyote wanazotoa huduma zote za chakula, vinywaji, malazi n.k
  • Tafuta meza ya nje iliyojitenga, yaani muwe wenyewe tu au kuwe na umbali kufikia meza nyingine.
  • Itakuwa vizuri zaidi kama itakuwa ni usiku
  • Agiza vinywaji vingi ili muhudumu asiwe anakuja mara kwa mara kwenye meza yenu.
  • Pia hakikisha umevaa nguo nzuri, inayomtamanisha mpenzi wako.
  • Pigeni stori za kawaida, ila mkifika chupa ya nne anza kuongea kwa hisia kwa kumuonyesha umuhimu wa mpenzi wako katika maisha yako.
  • Mpigie magoti huku ukitoa maneno ya mahaba ukiigiza kama unataka kulia, na kumuomba aweze kukusitiri katika ndoa.
  • Mlilie mpaka yeye mwenyewe aanze kulengwa na machozi, na hatimaye yeye mwenyewe atakuinua na kukumbatia, na atakupa jibu lako.
  • Baada ya kufanya hivyo, deka kama mtoto mdogo ikiwezekana uwe unamkalia kalia, huku mkiendelea kupata vinywaji.
  • Mkimaliza hapo, nendeni chumbani mkapumzike.
  • Kesho yake anza kutekeleza mlichoafikiana.
  • Baada ya hapo nawatakia ndoa njema.

Na sisi ambao sio walevi itakuwaje?,maana mtu huwezi kutoa ahadi kizembezembe kisa juice ya ukwaju
 
Utakuwa hupati ndoa ..........ohooooooo shauri yako 😎😎😎.
Kwa hiyo mkuu unaona Ni haki Mimi nimpeleke chobingo shemeji yako nianze kumpigia magoti nalia anioe!like serious????si unaweza nitwanga Kofi la ujinga ukinibamba huko?🙆😆
 
Back
Top Bottom