Njoo uifahamu Taxi Mtandao BOLT/UBER

Njoo uifahamu Taxi Mtandao BOLT/UBER

Hapana kata Leseni Yako ..siku hizi Wana verification ambayo itakuhitaji ujipige picha ili application ifunguke picha wanalinganisha na ya kwenye Leseni...hivyo kama muda huo mwenye Leseni yake hayupo maana yake itakulazimu umtafute ili akufungulie Kwa kujipiga yeye picha...itakua ni usumbufu haswa binadamu wenyewe awatabiliki unaweza ukagombana nae akakataa kukufungulia...ni Bora ukakata Leseni Yako kuepuka usumbufu...Leseni ya pikipiki kuipata ni Rahisi sana...​
Mkuu huwa inagharimu kiasi gani kupata leseni ya pikipiki?
 
Kujiunga ni bure bure kabisa unatakiwa uwe na
✓LESENI ya udereva yenye Madaraja ya pikipiki kama unataka kuendesha piki piki au c1 kama unataka kuendesha tax
✓chombo chako kiwe na Leseni ya usafirishaji abiria inayotolewa na Latra
✓uwe na bima yoyote hata Third party
✓chombo chako kiwe na usajiri wa biashara
LESENI

DARAJA C1 = LESENI KWA MAGARI YA ABIRIA 15-29 KUSHUKA CHINI

C3 = MAGARI MADOGO YA ABIRIA WASIOZIDI WA4
 
Je kama hutak gar yako iwe na namba nyeupe haiwezekan?
Inawezekana, unaweza ukawa na plate ya njano ukafanya biashara ya Uber ( Japo kihunihuni, na kiujanja.. mamlaka zikikutia nguvuni uandae maelezo ya kutosha) Maana hiyo nyeupe ni yaliyosajiliwa kibiashara so watasema unawakimbia kwenye matozo na kodi

NB: Nimejaribu kujibu kadiri ninavyojua

Naomba akikujibu nitag mkuu!!
 
Tembelea kituo chochote Cha t.r.a ukiwa na Tin Yako au nida...miongozo mingine utaikuta huko huko....japo nasikia siku hizi kupata leseni Hadi uwe umeenda driving school
wanataka cheti cha kueleweka cha driving course mzee baba siku hizi na kiwe kimetoka mojawapo ya vyuo hivi
  1. VETA
  2. NIT
  3. UJENZI MOROGORO
  4. POLISI UFUNDI - DAR
Na kama ni vyeti vya nje ya hivyo vi4 hapo juu (yaanii vyuo binafsi), basi ni lazima viwe na sifa kuu mbili ambazo ni;
1. Muhuri na Sahihi ya Regional Traffic Officer (RTO) wa mkoa husika
2. Kuonesha madaraja ya leseni ambayo dereva anapaswa kupewa
 
wanataka cheti cha kueleweka cha driving course mzee baba siku hizi na kiwe kimetoka mojawapo ya vyuo hivi
  1. VETA
  2. NIT
  3. UJENZI MOROGORO
  4. POLISI UFUNDI - DAR
Na kama ni vyeti vya nje ya hivyo vi4 hapo juu (yaanii vyuo binafsi), basi ni lazima viwe na sifa kuu mbili ambazo ni;
1. Muhuri na Sahihi ya Regional Traffic Officer (RTO) wa mkoa husika
2. Kuonesha madaraja ya leseni ambayo dereva anapaswa kupewa
Ila vya veta havina Madaraja...ya Leseni...maana Mimi nilisoma course ya refreshing pale Tanga lakini cheti changu hakikuwekwa Madaraja... Nilisoma VETA
 
Back
Top Bottom