Nyerere, Mwinyi, Mkapa, Kikwete, Magufuli na Samia, yupi Rais bora kwako?

JF inatakiwa iwe hivi kwa Watu wenye hekima kama wewe, sasa nashangaa kuna Mawatu yanaongozwa na hisia hadi kuandika takataka humu JF kuhusu Marais wetu wa nchi na bado moderators wanawachekea tu.
Hii extremism imekuwa inspired na viongozi wa kisiasa, kiongozi wa kisiasa anapotakamka waziwazi kuwa wanaompinga hawatakiwi kuishi, lazima awagawe sana watu
Nashukuru sasa hivi angalau nchi inarudi kwenye mstari
 
1. Nyerere.
Aliunganisha Taifa na kuweka misingi ya utawala.

2. Mkapa
Alifufua uchumi wa Taifa
 
Kwanza si vema kumlinganisha Nyerere na maraisi wengine, Nyerere ni Baba wa taifa, Mpigania Uhuru. Mwondoe kwenye huu mlinganisho tafadhali. Hakuna wa kulinganishwa nae. Mlinganishe na akina Nelson Mandela ndo Size yake.
 
Mkuu unamkumbuka Waziri Mkuu wa kwanza wa Rais A.H. Mwinyi?
 
Magu kiboko,aliagiza nchi nzima wafanyakazi wapeleke TIN number zao na wakafanya hivyo.sasa sijui akili yake alitaka azitumie vipi maana toka alale sijaona matumizi yake.
Ila kwangu mimi nilikuwa naona angewatoa wafanyakazi hewa kwenye kampuni binafsi.
 
Nakubaliana nawe. Lakini nampinga kwa kuuza NBC kwa wageni wakati wazawa walikuwa wanaweza kuinunua!
 
Nyerere
Alikuwa rais wa hovyo kuwahi kutokea nchi hii!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…