Yeye ndio aliunda watu wasio Julikana huyu mama anaendeleza .
Ilikuwa nadra ila awamu ya tano na hii kama za kigaidiNot true wasiojulikana waliibuka zamani sana. Sema mitandao umeifahamu Juzi tu. Unamfahamu dokta aliyetekwa akang'olewa kucha kisa kuongoza migomo kwa madokta nchini enzi za JK
Ilikuwa nadra ila awamu ya tano na hii kama za kigaidi
Watu wazima wanatukanana kwenye dunia yako.Ndo nataka ujue hilo. Vizuri kama umejua sasa acha kuleta utoto kwa watu wazima.
Hoja zipi hizo Bwana Juma wakati CCM hawataki kujibu na kuishia kupiga na kuteka watu kama sote tunavyoshuhudia now haya matukio?Kuna mipaka ya uzushi jamani!! Kuwahusisha watu au taasisi Fulani bila ushahidi ni hatari Kwa jamii. Hizi ni tetesi tu, hivyo kuibebesha serikali lawama Kwa tukio ambalo halijathibitishwa ni ushahidi wa namna baadhi ya watu mlivyo tayari kutumia Kila jambo kama silaha ya kisiasa. Tusiwe Taifa la hisia, Bali la hoja.
Huyu ni mbaya zaidi sababu anakuchekea chekea na 4R zake always watu WA pwani wanafiki Sana then anauaAwamu ya tano ndo hawa hawa waliopo awamu ya tano muhula wa pili
Official closure of the awamu ya 6. Ni ujinga sana wamefanya.
Hofu kubwa imetanda kufuatia tukio la kuvamiwa na kujeruhiwa kwa Katibu wa Baraza la Maaskofu wa Kanisa Katoliki nchini Tanzania (TEC) Padri Dkt.Charles Kitima.
Kupitia mitandao ya kijamii, imeripotiwa kuwa watu Wasiojulikana walimvamia Dkt Kitima majira ya saa 3 usiku wa April 30, 2025 na kuanza kumshambulia wakati akiwa kwenye makazi yake yaliyopo Ofisi za Baraza la Maaskofu (TEC) Kurasini, Dar Es salaam.
Mashuhuda wa tukio hilo waliokuwa eneo la tukio lililozungukwa na mgahawa walisema kuwa Padri Dkt Kitima ikiwa ni utamaduni wake wa kupita na kusalimu watu katika mgahawa mmoja eneo hilo, ghafla walitokea watu Wasiojulikana na kuanza kumshambulia kwa sekunde chache na kisha kuondoka.
Padri Kitima alijeruhiwa maeneo mbali mbali ya Mwili maana alikuwa akivuja damu katika sehemu mbalimbali za mwili wake na haijulikani alijeruhiwa na kitu Gani.
Mara baada ya shambulizi hilo, Dkt Kitima amepatiwa matibabu ya awali kwenye Kituo kidogo cha afya cha TEC kilichopo eneo hilo.
=====
UPDATES:
Polisi wadai kumshikilia mmoja: Polisi: Tunamshikilia Mtu mmoja kutokana na tukio la Padri Kitima kushambuliwa
=====
TAARIFA ZA AWALI:
"Tumepokea taarifa muda huu kuwa Father Dr Charles Kitima ameshambuliwa usiku huu nyumbani kwake na kujeruhiwa vibaya - hali yake si nzuri
Tunaendelea kufuatilia hii taarifa ila ieleweke kuwa shambulio kama hii hatuwezi kuchukulia kama bahati mbaya "
Ameandika hivyo Maria Sarungi kupitia mtandao wa X.
Ikumbukwe Padre Charles Kitima ni Katibu wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC).
Kama hizi ni taarifa za kweli, ni nini hatima ya hali hii inayoendelea nchini?
CCM mnataka kutupeleka wapi kama taifa?
View attachment 3321209
View attachment 3321207
Sijasema hayoKwahiyo ukiingiza siasa ni haki kushambuliwa na hata kuuwawa?
huyo ni mtuhumiwa tu, nani kasema amehusika?Ukiacha utabiri .. mtu mmoja alohusika kwenye shambulio ashakamatwa ... Endelea na utabiri kiongozi 😂😂😂
Ubaya wa JPM umeendelezwa na Samia, sio kwamba ubaya wa Samia ndio unafuta maovu ya JPM. Hata kama alikua hafanyi yeye, kukaa kimya huku maovu yantendeka means alikua anasupport.Sasa mbona kelele zilienda kwa JPM tuu?
Ni vibaka wa Samia hawa na polisi hata wakisema nini hawataaminika.Najua uzi huu hautadumu na leo mods mtapambana kuzima kila uzi utakaohusu kupigwa kwa Padri Dr. KITIMA ila sisi Wakatoliki tupo tayari na tunasubiri tamko rasmi.
Tunasubiri tamko la viongozi wetu na tupo tayari kuitii Mamlaka yetu ya Kanisa kanisa moja la mitume. Kanisa katoliki.
Tunajua mtaleta blah blah na kuleta movies kama yule Mkenya wa kipindi kile ila kama Kanisa litafanya uchunguzi na kutupa majibu washirika wake.
napenda kutoa wito kwetu wakatiliki twemde kwenye Jumuia kwa wingi kuanzia Jumamosi hii na zingine kwani huko tutapata maelekezo rasmi ya Kanisa.
Mwenye namba na mawasiliano ya Steve Mengele atuwekee humu. Mfikishieni ujumbe ajipange kwani tunakuja.