Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Nani kalaaniwa kati ya maskini ambaye wanaye wako straight au Elon Musk bilionea namba moja duniani lakini mwanaye wa kiume BWABWA na mjegeje kaukata kabisa??Hizi ni aina ya nyuzi ambazo masikini tunazitumia kujifariji huku maisha yakiendelea kutupiga knockout....umasikini ni laana na pesa ndio funguo ya kutatua matatizo ya maisha
Hili ni kweli angalia amekurupuka kusitisha shughuli za USAID bila kujali madhara kwa nchi zote ambazo zilikuwa zinapokea misaada hiyoMambo mengi ambayo Elon huyatamka au kuyafanya mengi yatokana na yale alopitia katika ukuaji wake kukosa mwongozo likiwemo lile la kutamka maneno au kufanya vitendo bila kuchuja au kuangalia madhara yake.
Hichi anokifanya na Raisi Trump kitaleta madhara fulani kwa wamarekani wale ambao watakuwa ni homeless wakirudi kwao.Hili ni kweli angalia amekurupuka kusitisha shughuli za USAID bila kujali madhara kwa nchi zote ambazo zilikuwa zinapokea misaada hiyo
Wote wana laana za aina tofauti katika hii dunia umasikini sio barakaNani kalaaniwa kati ya maskini ambaye wanaye wako straight au Elon Musk bilionea namba moja duniani lakini mwanaye wa kiume BWABWA na mjegeje kaukata kabisa??
Mara nyingi wanaume wanaotumia pesa kupata wanawake ni wanaume wasio na mvuto wowote..Lakini mkuu tuache masihara kidogo pesa inaweza kkupatia Asilimia kubwa ya wanawake ata kama hawakupendi
Tafuta pesa alafu ndo uje ulete hoja mezani ya kupingaMara nyingi wanaume wanaotumia pesa kupata wanawake ni wanaume wasio na mvuto wowote..
Kweli kuwa Bilionea siyo mwisho wa matatizo. Angalia mahusiano mabaya ya Elon Musk dhidi ya wanafamilia wake:-
1. Wake wa Zamani
Elon Musk amewahi kuoa mara mbili kwa wanawake wawili tofauti:
- Justine Musk (2000–2008): Justine alikuwa mke wa kwanza wa Musk, na walizaa watoto watano pamoja (mapacha na mapacha watatu). Mtoto wao wa kwanza, Nevada, alifariki kutokana na ugonjwa wa ghafla wa watoto wachanga (SIDS). Talaka yao haikuwa nzuri, na Justine baadaye alieleza ndoa yao kama iliyojaa changamoto za kihisia. Alisema alihisi kufunikwa na mafanikio na malengo makubwa ya Musk.
- Talulah Riley (2010–2012, 2013–2016): Musk alimuoa mwigizaji wa Uingereza Talulah Riley mara mbili. Walifunga ndoa mara ya kwanza mwaka 2010, wakatalikiana mwaka 2012, kisha wakaolewa tena mwaka 2013 kabla ya kutalikiana tena mwaka 2016. Uhusiano wao ulikuwa wa kirafiki zaidi kuliko ndoa yake ya kwanza, na Riley alisema wanaendelea kuwa marafiki.
2. Mwanaye mvulana aliyejigeuza kuwa mwanamke, na kisha kujitenga na Elon Musk
Binti wa Elon Musk, Vivian Jenna Wilson, alijitenga naye kabisa baada ya kubadili jinsia. Aliomba rasmi kubadilisha jina lake mwaka 2022 enzi hizo akiitwa Xavier Musk, akisema hataki tena kuhusiana na baba yake. Ingawa Musk amesema uhusiano wao uliharibika kwa sababu ya "itikadi kali za kisasa," inaonekana kuwa kuna sababu kubwa zaidi. Ripoti zinasema kuwa Vivian amekata mawasiliano kabisa na baba yake.
3. Baba yake, Errol Musk
Elon ana uhusiano mgumu na wa mvutano na baba yake, Errol Musk. Amewahi kumuelezea baba yake kama mtu mgumu na wakati mwingine mkatili, akisema kwamba alikulia katika mazingira magumu. Errol naye ametoa kauli tata kuhusu Elon na familia yao. Moja ya mambo yaliyozua mshangao mkubwa ni kwamba Errol alipata mtoto na binti wa kambo wake, jambo ambalo lilimchukiza sana Elon. Ingawa wamekuwa wakizungumza mara kwa mara kwa miaka, uhusiano wao bado haujawa mzuri.
Mara nyingi wanaume wanaotumia pesa kupata wanawake ni wanaume wasio na mvuto wowote..Lakini mkuu tuache masihara kidogo pesa inaweza kkupatia Asilimia kubwa ya wanawake ata kama hawakupendi
NishatafutaTafuta pesa alafu ndo uje ulete hoja mezani ya kupinga
Hakuna kila kituKumbe kila kitu nini ?
Sio kweli juzi baba ake alikuwa anahojiwa wapo connected vibaya mnoKawaida hata kukosa maaasiliano na baba??
Mwamba wa Clouds aliyetibiwa South Afrika tukaambiwa shida ni figo na tukazika Bukoba, hakuwa na hela ya kubadilisha hizo figo ?Ukiwa na pesa hata figo zikiharibika huna mawazo ya bei ya kubadili, Maskini safari yake imeishia hapo