Pamoja na utajiri wake; matatizo ya Elon Musk na familia yake ni makubwa kuliko maskini

Hizi ni aina ya nyuzi ambazo masikini tunazitumia kujifariji huku maisha yakiendelea kutupiga knockout....umasikini ni laana na pesa ndio funguo ya kutatua matatizo ya maisha
 
Pesa nzuri huoni inafanya watu wanatakata?Alaaah Kwanza hivi unadhani huyo Elon musk asingekua na Hela angekua kapuku kama ww ungekuta unamtaja ? Suala la huyo punga sese wake ampige Shaba tu mamaee
Kama Marvin Gaye Sr siyo
 
Hizi ni aina ya nyuzi ambazo masikini tunazitumia kujifariji huku maisha yakiendelea kutupiga knockout....umasikini ni laana na pesa ndio funguo ya kutatua matatizo ya maisha
Nani kalaaniwa kati ya maskini ambaye wanaye wako straight au Elon Musk bilionea namba moja duniani lakini mwanaye wa kiume BWABWA na mjegeje kaukata kabisa??
 
Mask katika ukuaji wake alikabiliwa na changamoto kadhaa likiwemo suala la kutengana na kuachana kwa wazazi wake. Mwaka 1980 wazazi wake waliachana (Elon akiwa na umri wa miaka 9) hivyo hili lilikuwa ni tatizo.

Kwa kuwa aiishi na baba yake pamoja na ndugu wengine ni dhahiri Elon alianza kukabiliana na changamoto za nidhamu na kuna wakati imesemwa alipigana shule na mtoto mwenzie.

Elon ameonekana alizaliwa na uwezo wa kiakili (akiwa na miaka 10 aliweza kufanya programing kwa michezo ya kompyuta na video games).

Hivyo Elon ni mmoja wa watu ambao huzaliwa katika mazingira mazuri lakini pia yeye changamoto ambazo husababisha kuwepo hitilafu katika nidhamu ya mtoto katika hatua za ukuaji.

Mambo mengi ambayo Elon huyatamka au kuyafanya mengi yatokana na yale alopitia katika ukuaji wake kukosa mwongozo likiwemo lile la kutamka maneno au kufanya vitendo bila kuchuja au kuangalia madhara yake.
 
Hili ni kweli angalia amekurupuka kusitisha shughuli za USAID bila kujali madhara kwa nchi zote ambazo zilikuwa zinapokea misaada hiyo
 
Hili ni kweli angalia amekurupuka kusitisha shughuli za USAID bila kujali madhara kwa nchi zote ambazo zilikuwa zinapokea misaada hiyo
Hichi anokifanya na Raisi Trump kitaleta madhara fulani kwa wamarekani wale ambao watakuwa ni homeless wakirudi kwao.

Hawa ndo huenda wakachukua nafasi ya homeless wageni walorudishwa kwenye nchi zao.

Hawa wapo wataonunua bunduki na kuanza zogo.
 
Nani kalaaniwa kati ya maskini ambaye wanaye wako straight au Elon Musk bilionea namba moja duniani lakini mwanaye wa kiume BWABWA na mjegeje kaukata kabisa??
Wote wana laana za aina tofauti katika hii dunia umasikini sio baraka
 
Weee na umasikini wako una uhusiano mzuri na jamaa zako
 
Kuna kina pangupakavu nao wana matatizo hayo ya kifamilia + uchawi, elimu duni na umasikini uliokithiri.

Si ajabu Musk haoni kama hayo ni matatizo.
 
Ukiwa na pesa hata figo zikiharibika huna mawazo ya bei ya kubadili, Maskini safari yake imeishia hapo
Mwamba wa Clouds aliyetibiwa South Afrika tukaambiwa shida ni figo na tukazika Bukoba, hakuwa na hela ya kubadilisha hizo figo ?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…