Papa Francis: Hisani ya Kichungaji itumike wapenzi wa jinsia moja wanapowaomba mapadri baraka

Papa Francis: Hisani ya Kichungaji itumike wapenzi wa jinsia moja wanapowaomba mapadri baraka

Status
Not open for further replies.
Kuna sisi ambao tuliondoka RC miaka kadhaa nyuma tukaonekana kana tumefanya kitu gani sijui.... Haya .... Ninyi mliobakigi huko RC mje hapa mtuambie hiki Ni kitu gani??? Mtudadavulie kuwa kiongozi wenu kasema Nini hapa??? Maana hata hatujaelewa....
Uliokoka au ulikuja kwenye uislamu
 
. Kweli we ni msen**, kwa hiyo papa akiluhusu, lazima wafumuliwe,

. DADA VIPI WEWE, TOKA ULIVYO TOLEWA MALINDA.. AKILI ZAKO ZIMEKUHAMA KABISA. Holeshit
Mkubwa kisha sema,subiri tu uliwe trako,utakua unauza bei gani? au free of charge?
 
Fake news.Na mnaoshabikia mtakuwa na hizo elements..Kichwa cha habari na maelezo ni vitu viwili tofauti...
 
Nafikiri huu ndio wakati wa wakatoliki kusilimu au kurejea kwenye dini za mababu.

Sisemi kuwa miongoni mwa waislamu hakuwa watu wanao fanya mambo hayo? La haha! Mambo hayo yanafanywa na watu wa dini zote wakristu kwa waislamu. Tatizo ni pale taasisi kama taasisi ya kidini inapo yatambua mapenzi ya namna hiyo.

Poleni sana wakatoliki.

====

"Hatuwezi kuwahukumu ambao wanakanusha tu, kukataa na kuwatenga,"

Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani Papa Francis amependekeza kuwa atakuwa tayari kuona Kanisa Katoliki likibariki wapenzi wa jinsia moja.

Akijibu kundi la makadinali waliomuomba ufafanuzi juu ya suala hilo, alisema ombi lolote la baraka linapaswa kushughulikiwa na "hisani ya kichungaji".

Aliongeza, hata hivyo, Kanisa Katoliki bado linachukulia uhusiano wa jinsia moja "kuwa dhambi" na halitatambua ndoa za jinsia moja.

Ombi hilo lilikuwa mojawapo ya maombi yaliyotumwa kwa Papa kabla ya mkutano wa kimataifa wa wiki nzima kujadili mustakabali wa Kanisa unaotarajiwa kuanza mjini Vatican siku ya Jumatano.

Katika Kanisa Katoliki, baraka ni maombi au ombi, ambalo kwa kawaida hutolewa na kiongozi wa kiroho, akimwomba Mungu amtazame mtu au watu wanaobarikiwa.

BBC Swahili
wanataka wapewe ruhusa ya kuchezea kinyesi na bado waende kanisani.. Dr. Slaa anaita hii, kupakua kinyesi sebuleni na ili hali msosi unakaribia...
 
Ni sawa lakini dini kama dini ya ki islamu haitambui hayo mahusiano
msijione mko smart sana kwa mapenzi ya jinsia moja, mnakutwa na tayari wako ndani ya dini yenu mnayoiita dini ya mnyaazi mungu. Tayari ndoana mmeimeza hamtikisiki tena chambo mmeibugia, ni suala la muda tu nanyi mtaipata fresh dini yenu haitasalimika na tufani hii ya hayo mapenzi
 
Aliongeza, hata hivyo, Kanisa Katoliki bado linachukulia uhusiano wa jinsia moja "kuwa dhambi" na halitatambua ndoa za jinsia moja.

Mbona kama conclusion ipo hapa...
 
Mbona kama conclusion ipo hapa...
Usihangaike nao watu wa hivyo. Hao ndiyo wanaopigania ushoga uruhusiwe hivyo wanahakikisha wanau trendisha kivyovyote na kupotosha taarifa
 
Wapendwa wenzangu napenda kujua kama hizi habari ni za kweli?

Tumebiwa tangu wadogo kwamba POPE mtakatifu, hata uchaguzi wake ni kitakatifu.

Anaongea kitakatifu, akibariki na kuguswa mikono na kubusiwa mikono kitakatifu.

Imenichanganya akili sana.

Screenshot_2023-10-03-13-36-54-43_0b2fce7a16bf2b728d6ffa28c8d60efb.jpg

---
Papa Francis amependekeza kuwa atakuwa tayari kuona Kanisa Katoliki likibariki wapenzi wa jinsia moja.

Akijibu kundi la makadinali waliomwomba ufafanuzi juu ya suala hilo, alisema ombi lolote la baraka linapaswa kushughulikiwa na "hisani ya kichungaji".

"Hatuwezi kuwa majaji ambao wanakanusha tu, kukataa na kuwatenga," alisema.

Aliongeza, hata hivyo, kwamba Kanisa bado linachukulia uhusiano wa jinsia moja "kuwa dhambi" na halitatambua ndoa za jinsia moja.

Ombi hilo lilikuwa mojawapo ya idadi iliyotumwa kwa Papa kabla ya mkutano wa kimataifa wa wiki nzima kujadili mustakabali wa Kanisa unaotarajiwa kuanza mjini Vatican siku ya Jumatano.

Katika Kanisa Katoliki, baraka ni maombi au ombi, ambalo kwa kawaida hutolewa na mhudumu, akimwomba Mungu amtazame mtu au watu wanaobarikiwa.
Maaskofu katika nchi kadhaa, ikiwa ni pamoja na Ubelgiji na Ujerumani, wameanza kuwaruhusu mapadre kuwabariki wapenzi wa jinsia moja, lakini msimamo wa mamlaka ya Kanisa ulibakia kutoeleweka.

Mnamo 2021, kufuatia ombi kama hilo la ufafanuzi, ofisi ya mafundisho ya Vatikani iliamua kutoruhusu zoea hilo.

Akijibu ombi la hivi punde zaidi, Papa alisema kwamba Kanisa linaelewa ndoa kuwa "muungano wa kipekee, thabiti, na usioweza kutenganishwa kati ya mwanamume na mwanamke" na inapaswa kuepuka "aina yoyote ya ibada au sakramenti ambayo inaweza kupingana na imani hii".
Lakini aliongeza kuwa "baraka inapoombwa, ni kuonyesha ombi kwa Mungu kwa msaada, dua ya kuishi bora".

"Busara ya kichungaji lazima itambue vya kutosha kama kuna aina za baraka, zinazoombwa na mtu mmoja au zaidi, ambazo hazileti dhana potofu ya ndoa," alisema.

Akionekana kupendekeza kwamba maombi ya baraka yazingatiwe kwa msingi wa kesi baada ya kesi, alisema kwamba "maamuzi ambayo yanaweza kuwa sehemu ya busara ya kichungaji katika hali fulani haipaswi kuwa kawaida".
"Sheria ya Canon haifai na haiwezi kufunika kila kitu," alisema.

Aliongeza kuwa Kanisa linapaswa kukaribia uhusiano wake na watu kila wakati kwa "fadhili, uvumilivu, ufahamu, huruma, na kutia moyo".

Mnamo Februari, kura ya viongozi wakuu katika Kanisa la Uingereza iliunga mkono mapendekezo ya kuruhusu maombi ya baraka kwa wapenzi wa jinsia moja.

Hatua hiyo ilimaanisha kwamba wanandoa wa jinsia moja wanaweza kwenda katika kanisa la Anglikana baada ya sherehe ya ndoa halali kwa ajili ya huduma zikiwemo maombi ya wakfu, shukrani, na baraka za Mungu.

BBC Swahili
 
Kuna sehemu nimesoma, Papa hajaruhusu hilo jambo.

Ila ikitokea siku wakaamua kubariki huo ushweitwani, haki ya nani nitaachana kabisa na mambo ya kusali. Kubariki huo upuuzi, kutaleta mgawanyiko mkubwa kwenye Kanisa.
Hizo kauli zake tayari ni mtego.

Toka kwenye dini hiyo ambayo Yesu hakuianzisha.

Baki na Imani katika Yesu Kristo wa Nazareth.

Yesu aliwahubiri INJILI wezi, mashoga, waongo, kamwe hakuwabariki, aliwakemea.
 
Nafikiri huu ndio wakati wa wakatoliki kusilimu au kurejea kwenye dini za mababu.

Sisemi kuwa miongoni mwa waislamu hakuwa watu wanao fanya mambo hayo? La haha! Mambo hayo yanafanywa na watu wa dini zote wakristu kwa waislamu. Tatizo ni pale taasisi kama taasisi ya kidini inapo yatambua mapenzi ya namna hiyo.

Poleni sana wakatoliki.

====

"Hatuwezi kuwahukumu ambao wanakanusha tu, kukataa na kuwatenga,"

Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani Papa Francis amependekeza kuwa atakuwa tayari kuona Kanisa Katoliki likibariki wapenzi wa jinsia moja.

Akijibu kundi la makadinali waliomuomba ufafanuzi juu ya suala hilo, alisema ombi lolote la baraka linapaswa kushughulikiwa na "hisani ya kichungaji".

Aliongeza, hata hivyo, Kanisa Katoliki bado linachukulia uhusiano wa jinsia moja "kuwa dhambi" na halitatambua ndoa za jinsia moja.

Ombi hilo lilikuwa mojawapo ya maombi yaliyotumwa kwa Papa kabla ya mkutano wa kimataifa wa wiki nzima kujadili mustakabali wa Kanisa unaotarajiwa kuanza mjini Vatican siku ya Jumatano.

Katika Kanisa Katoliki, baraka ni maombi au ombi, ambalo kwa kawaida hutolewa na kiongozi wa kiroho, akimwomba Mungu amtazame mtu au watu wanaobarikiwa.

BBC Swahili
Kuwabariki alimaanisha nini? Kuwapa cheti cha kufunga ndoa? Tufafanulie, usichukue mambo kama dodoki linavyofyonza maji.....kwa ushabiki
 
Hizo kauli zake tayari ni mtego.

Toka kwenye dini hiyo ambayo Yesu hakuianzisha.

Baki na Imani katika Yesu Kristo wa Nazareth.

Yesu aliwahubiri INJILI wezi, mashoga, waongo, kamwe hakuwabariki, aliwakemea.
Sasa hiyo kauli ina mtego gani hapo! Halafu unafikiri mimi ni mtu mwepesi tu wa kunibadilisha mtazamo wangu wa kiimani!! Aisee pole sana.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom