Hii hoja ya Mayalla ina pande mbili, positive ambayo naona wengi wanaishangilia, na negative, ambayo naamini wengi hawajaifikiria.
Kuitaka serikali kuondoa ruzuku kwa vyama vya siasa, hasa kwa wakati huu wa vyama vingi, kwa upande mwingine kutamaanisha kuineemesha zaidi CCM.
CCM ina vitega uchumi kila kona ya nchi, wanakusanya kodi kwenye fremu mbalimbali karibia mikoa yote Tanzania Bara, hawa wamejiwekeza kiuchumi, hivyo hata leo ukiwaambia unaondoa ruzuku kwao hawataumia pakubwa.
Tatizo ni kwa hivi vyama vyetu vingine, kuviambia visubiri michango ya kujitolea toka kwa wanachama wao, hiyo kwangu ni sawa na ndoto isiyo na uhakika wa kutokea, hata kama vyama vitaweka kiasi kidogo vipi cha makusanyo, bado havitakuwa na uhakika wa kufikia malengo waliyojiwekea kwa wakati husika.
Sasa kwenye mazingira haya, unakuja kuviweka vyama hivi kwenye mizania moja na CCM, hapo hakuna namna, lazima CCM itaendelea kuwa na uwezo mkubwa kiuchumi utakaokifanya kijiendeshe bila shida, ila kwa hawa watakaosubiri michango ili wafanye mikutano ya siasa, walipane mishahara, mafuta ya magari, gharama za kuendesha ofisi, naona hivi vyama vitapotea kimoja baada ya kingine.
Sent from my SM-G900H using
JamiiForums mobile app