Pre GE2025 Pascal Mayalla: Vyama vya siasa visipewe ruzuku, viongozi wake wajitolee

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Naunga mkono hoja,huu ni wizi wa pesa za Umma.Zito apuuzwe na ruzuku ifutwe
 
CDM kwa mfano, walishaomba ruzuku hizi zifutwe kitambo sana, lakini cha kushangaza CCM wamegomea maana wao ndiyo wazoaji wakuu wa hizi ruzuku - wanakula ma-billion ya shillingi kila mwezi ndiyo hizo hizo wanazotanulia kununulia ma V-eiteee.
 
Viongozi wasipewe usafiri wala kujaziwa mafuta ya gari , wajinunulie magari na kujaza mafuta kwa pesa zao za mshahara.

Wabunge wasipewe posho za vikao , bungeni ndio ofisini kwao kama ambavyo daktari anaenda hospital kuattend wagonjwa hospital ndio ofisini na halipwi posho ya kwenda ofisini na wabunge wasilipwe posho ya kuwepo ofisini bali mshahara tu.
 
Kwa kweli Mayala Paschal hii ni point nzuri na kubwa sana brother. Hivi vyama , ni vyama vya matumbo tu. Hakuna vyama hapo.Wiz wiz tu.
 
Mayala yuko sahihi. Ni matumizi mabaya ya pesa za Umma. Vyama vijitegemee. Kama ni misaada ya nje hata sasa wanapata pamoja na kupata ruzuku.

..kwanza vyama vyote vifutwe.

..pili serikali itafishe mali za vyama vyote vilivyoko sasa hivi.

..tatu vyama visajiliwe upya na kusiwepo chama chochote kitakachopewa ruzuku.
 
Mimi ningekubaliana na wewe kama hivi vyama mbadala vingekuwa serious...
Hakuna kitu kilionesha upumbavu wao mkubwa kama issue ya kumpokea Lowassa na kitu kiitwacho kuunga juhudi...huu ndio ulikuwa upumbavu namba moja.
Kwa kifupi wote ccm na vyama vingine ni magenge ya wezi hivyo KATA RUZUKU..kila mtu afe kivyake...
 
Hata hiyo rudhuku hamstahili.
Naunga mkono hoja
P
 
Pascal Mayalla wewe ni muaminifu. Asante
Inawezekana na ni rahisi sana kuvinyima ruzuku vyama vile ambacho havipo madarakani yaani vyama vya upinzani, lakini ukweli ni kwamba chama tawala ni lazima kitapata mapesa mengi sana kutoka Serikalini kupitia njia watakazoziibua kwa wakati maalum necessarily !!
Epa and so on and so forth !!
Huwezi kumzuwia kula chakula mtu aliyepo jikoni anapika !!
Atakula tu hata kwa kificho !!
 
Inawezekana ukamzuwia kula chakula mtu mwenye funguo za jikoni ??!!
😂
 
Pascal ana akili nyingi sana. Kaka huna baya
 

View: https://youtu.be/kpOuytUa4O4?si=0CEA3qzDha1b5_HQUkiiweka kule kwenye thread starter utakuwa umewatendea haki zaidi wasomaji wako.
P
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…