Habari za wakati huu;
Wakati jamiiforums inaanzishwa kulikuwa na majukwa mengine ambayo yalikuwa yanabamba. Kuja kwa internet na website kuna maanisha kwamba sasa ni rahisi mtu kuanzisha biashara na kufikia wateja wa mbali zaidi.
Kila biashara inaweza kuwekwa mtandaoni hata hivyo ili kufanikiwa katika baishara yoyote ni lazima uamuze kwamba biashara yako itakuwa "digital first" kwa lugha nyingine unatakiwa ulenge kufanya biashara yako iuze kwa njia ya mtandao.
Wajasiriamali wengine sana wamewekeza kwenye mitandao ya kijamii kama insta na fb etc. Ambako wanajifanikiwa kutengeneza business ingawa bado scaling up ya biashara yao inakuwa chini. Ndio maana leo nimeamua kuleta fursa/ wazo la aina tano ya tovuti za kibiashara ambazo unaweza kuzianzisha.
Kabla ya kuendela inabidi nikueleze kidogo kuhusu tovuti na umuhimu wake,tovuti au website ni mkusanya wa kurasa za kidigitali zinazohusiana na zenye taarifa zinazohusu mtu, kampuni, biashara, bidhaa au huduma.Kwa mfano ukitembelea tzhosts.com utakutana na taarifa za huduma mbalimbali zinazouzwa nasi.
Vivyo hivyo ukitembelea tovuti kama alibaba, aliexpress, amazon, jiji na nyinginezo utakuta zinauza bidhaa na huduma tofauti. Hata youtube, jamii forum, facebook, twitter etc zote ni tovuti ambazo zinatumika kwa ajili ya shughuli na huduma mbalimbali.
Je unaweza na wewe kuanzisha tovuti ya kibiashara?Jibu ni Ndio.Unaweza kuanzisha tovuti ya kibiashara kwa gharama nafuu na huduma ya uhakika bila kuhitaji kuwa na utaalamu wa teknoloji.
Leo ninawaletea mawazo 5 au aina tano ya tovuti ambazo unaweza kuzianzisha na zikakuingizia mapato:
- Tovuti za taarifa za fursa zilizoko katika Eneo unaloishi-Aina hii ya tovuti unaitengeneza maalum kwa ajili ya wakazi wa mji wako au kata yako na unakuwa unaweka maudhui ambayo ni relevant/yanawahusu wakazi wa kata yako.
- Tovuti ya aina ya pili inaweza kuwa tovuti maalum kwa ajili ya simulizi na hadithi.Unaweza kuwa na tovuti maalum kwa ajili ya simulizi na hadith ambapo unaandika simulizi na hata ukitaka unawezesha kuziuza kama vitabu vya electronic e books kwa malipo ya njia ya mtandao.
- Tovuti nyingine unaweza kuanzisha kwa ajili ya kuuza mazao na bidhaa za ufugaji.Unaweza kuamua kuanzisha tovuti ya kuuza kuku wa kienyeji, mbuzi ngombe, kondoo,mayai n.k. n.k.Unakuwa na option ya kuuza akiwa mzima au amechinjwa.
- Unaweza kuamua kuanzisha tovuti ya kuuza mazao ya kilimo kama vile nafaka,matunda na mazao mengine.Unaweza kuamua kuuza zao moja au kuuaza mazao ya aina tofauti
- Unaweza kuanzisha tovuti maalum kwa ajili ya matangazo ya vifo/ndoa kwa eneo ulipo kwa ajili ya wakazi wa eneo hilo
- Unaweza kuanzisha tovuti maalum kwa ajili ya watu kuomba nafasi za kazi kwa kutuma CV zao kisha unazituma kwa waajiri tofuati kwa ajili ya Nafasi z kazi za muda au za kudumu.
- Unaweza pia kuanzisha tovuti zinazoelezea historia na wasifu a watu maarufu wa eneo unalokaa kama vile viongozi wa kidini,siasa na kijamii walio hai au waliokufa
- Unaweza kuanzisha tovuti maalum kwa ajili ya kuorodhesha sehemu za kula,kulala,kuburudika,kumbi za sherehe na starehe na kutoa taarifa na hata kuzifanya rating ya ubora.
- Unaweza kuazisha tovuti maalum inayotoa taarifa kuhusu fursa za uwekezaji na biashara zilizopo katika eneo ulipo
- Unaweza pia kuanzisha tovuti maalum kwa ajili ya historia ya kabila/jamii yako ikiwa pia na mafunzo kuhusu mila na desturi zenu na taari nyingine za msingi.
Aina zote hizi za tovuti zinaweza kuanzishwa na kusimamiwa kwa gharama nafuu na uhakika kutoka tzhosts.com.Wasiliana nasi leo kwa email
sales@tzhosts.com tujadili namna ambavyo unaweza kuzitumia tovuti hizi kwa jili ya kujiingizia kipato.