Paul Makonda awa kiongozi wa kwanza kuzuiwa kuingia Marekani kwa kuwanyima watanzania HAKI YA KUISHI

Paul Makonda awa kiongozi wa kwanza kuzuiwa kuingia Marekani kwa kuwanyima watanzania HAKI YA KUISHI

Hatuna cha kupoteza eti kwa kumzuia RC Makonda kwenda Marekani. Kwanza wajiulize tangu Rais wetu John Pombe Magufuli aingie madarakani alishawahi kwenda ubarozi wa Marekani nchini kuomba Viza ya kuingia Marekani? Ukweli ni kwamba hajawahi kwahiyo RC Makonda aende Marekani kutafuta nini ambacho bosi wake haoni haja?
Yeah kweli kabisa
IMG-20200201-WA0047.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hatuna cha kupoteza eti kwa kumzuia RC Makonda kwenda Marekani. Kwanza wajiulize tangu Rais wetu John Pombe Magufuli aingie madarakani alishawahi kwenda ubarozi wa Marekani nchini kuomba Viza ya kuingia Marekani? Ukweli ni kwamba hajawahi kwahiyo RC Makonda aende Marekani kutafuta nini ambacho bosi wake haoni haja?
You are very wrong, na kama akili za watanzania walio wengi ni kama hizi tumekwisha!!! Kiongozi fulani wa nchi fulani anapowekewe vikwazo kuingia Marekani huwa siyo adhabu kwake bali ni adhabu kwa Taifa hilo kwa sababu usisahau jina la nchi hiyo linakuwa limechafuka, watalii hupungua, wawekezaji hupungua, misaada hupungua, e.t.c.
 
Hatuna cha kupoteza eti kwa kumzuia RC Makonda kwenda Marekani. Kwanza wajiulize tangu Rais wetu John Pombe Magufuli aingie madarakani alishawahi kwenda ubarozi wa Marekani nchini kuomba Viza ya kuingia Marekani? Ukweli ni kwamba hajawahi kwahiyo RC Makonda aende Marekani kutafuta nini ambacho bosi wake haoni haja?
Maneno ya mkosaji. Mbona mnabwata sana baada ya huo mkopo kucheleweshwa?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hivi hako ka.katazo kao ka.green card nako kanatuhusu? Kuna watanzania wangapi wanakacheza?
 
Hii movie ilianza pale ubalozi wa USA na UK nchini Tanzania walipotoa tahadhari ya uwezekeno wa kutokea shambulio la kigaidi maeneo yenye wageni wengi (wazungu) . Ninavyo kumbuka makonda alijitokeza kwenye media na akapingana nao kwa kusema hakuna hatari yoyote. Maafisa wetu wanafanya kazi nzuri. Lakini sababu nyingine inaweza ikawa msimamo wa makonda kuhusu ushoga. Ushauri wangu kwa watanzania hakuna mzungu atakayepambana kwa faida ya mtanzania, watu weusi tuache ujinga
 
Hiyo kodi yetu mpaka ikodishe meli nadhani raia watakuwa wapo tayari barabarani wakipinga hali ngumu ya maisha
Inabidi nicheke tu badala ya kukasirika kwa lugha zako zisizo na chembe ya werevu na busara.
Unadhani kuita daktari nchini toka Marekani au Ulaya ni dola ngapi?

Ngoja nikusaidie kuona mbali wewe mjuaji,
Makonda kwa nafasi yake na kama anapata baraka ya afanyayo toka juu ana uwezo wa kutumia fedha zako (kodi za wananchi) kualika madaktari bingwa toka nje kwa kisingizio cha kuja kusaidia wananchi maskini wenye matatizo sugu ya kiafya kama mfano wa ile meli ya kichina aliyo alika, humo ndani ya msafara wanakuja madaktari bingwa na vifaa kamili ndani ya meli yenye hadhi ya hospital ya rufaa ya nchi zilizo endelea wanakuja kumtibu yeye.
Wanazuga kutibu wanyonge na vipanado toka kwa mabeberu kwisha kazi.

Kwa kukusaidia tu huko Marekani na Uingereza wamejaa madaktari bingwa ambao very rogue, wao pesa tu, wengine wahindi, waarabu, warusi na waamerika ya kusini ambao ni maarufu Marekani wanakofanyia kazi zao.

Money can buy anything, anyone provided reasonable price is reached.
Kila mtu na kila kitu kuna bei yake ya kununuliwa kiasi kikifikia biashara inafanyika tu.
Hakuna namna.
Go figure my friend!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kama una AKILI Timamu ZUIO hili la
BASHITE na mke wake huko USA ni kuchokonolewa kwenye UTOSI wa RAIS JOHN P. MAGUFULI.

Pia ni kutangaziwa tunafahamu kila kitu kinachoendelea katika UTAWALA wake tangu Mwaka 2015 Hadi leo.
 
Bila shaka Kauli ya Marekani ina uhusiano mkubwa sana na uwepo wa Zitto na Lissu (sstt) katika Inchi hizi za Kibeberu.
Beberu pamoja na kutaka aendelee kutawala kiuchumi kama ilivyo kwa hulka hata ya wafanyabishara wa Ki Tanzania, lakini kamwe hapendi kuona mtu moja anajitokeza na kutishia uhai wa watu wengine.

Wako radhi kutumia gharama kubwa kumuondoa kama walivyofanya kwa akina Gadaffi, Osama na wengine.
Serikali yetu tukufu ilitumia nguvu kubwa na ujasiri wa hali ya juu kuliangamiza bila huruma kundi la watu wachache waliokuwa wanaua watu huko Kibiti.

Kwa hiyo, kama tuhisi mambo haya ni ya kweli, tuchukue hatua. Kama ni ya uongo, tuchue nafasi kuyapinga hadharani hata kwa maandamano kwenda kwa Mkuu wa Mkoa wa Dar na kumpa Moyo asiwe na wasi wasi kwa sabau sisi tuko upande wake.
 
Taarifa ya Marekani nikianza na aya ya kwanza na ya pili inatuonesha Watanzania Makonda ni mtu wa aina gani. Japo kingereza changu cha ugoko lakini tutachambua mstari kwa mstari kuona Wamarekani wanatuma ujumbe gani kwetu wanyonge kama ifuatavyo.

AYA YA KWANZA

Makonda has involved in gross violation of human right which includ Denial of the right to life, Liberty or the security of persons. ( Kwamba Makonda anahusika kwa kiwango cha juu mno ktk uvunjaji wa haki za Binadamu ambazo zinahusu kama
1.Kukiuka haki ya mtu ya kuishi yaani anafanya Mauaji ya Watu wasio na hatia.

2. Anakiuka haki ya watu kuwa huru yaani anateka, anatesa, anapoteza watu.

3.Anahatarisha usalama wa watu yaani anatishia ana ua watu, au kutesa raia.

"Specifically the Department has credible information that Makonda was involved in in such violations in his capacity as the regional commissioner of Dar es salaam".( Kwamba Marekani inazo taarifa za uhakika pasipo na shaka kuwa Makonda ametenda uharifu huo dhidi ya binadamu akitumia cheo chake kama mkuu wa mkoa wa Daresalam)

'In that role Makonda has also been implicated in oppression of the political oppression, crackdowns on freedom of expression and association and the targeting marginalized individuals" ( Kwamba akiwa ktk wadhifa huo Makonda ndio mwasisi wa kupanga na kuteleza uzalilishaji na ukatili dhidi ya Viongozi wa kisiasa wa upinzani, kuzuia uhuru wa kujieleza na kukutana na kuwalenga makundi mbali mbali yakijamii dhidi ya ukatili huo)

AYA YA PILI

"The United states remain deeply concerned over deteriorating of respect of human right and a rule of law in Tanzania". ( Kwamba Marekani bado inayo mashaka makubwa na inafuatilia kwa kina juu ya kuongezeka kwa Ukatili dhidi ya ubinadamu na kutoheshimwa kwa haki za Binadamu na utawala wa Sheria nchini Tanzani)

"This includes actions taken by the Government that curtail freedom of expression, freedom of association and the right to peaceful assembly".( Hii inahusiana hatua zilizo chukuliwa na Serikali ya Tanzania ambayo inazuia na kuwekea watu vikwazo kinyume cha sheria kuzuia uhuru wao wa.
1. Kujieleza
2.Kukutana
3.Kunyimwa uhuru wa kukutana bila kughasiwa )

"Target marginalized people and the political opposition and Jeopardize people".( Yaani serikali imekuwa ikiwalenga na kuwatendea uharifu Makundi mbali mbali ktk jamii kama wanaharakati, waandishi wa habari, viongozi wa dini, Viongozi wa vyama vya siasa wa Upinzani na Kuhatarisha Maisha ya Watu )

Wakati Marekani ikitueleza wana wa Nchi kuwa bila kuwa na shaka wala kupepesa Macho kuwa Makonda ni muaji na wanao ushahidi juu ya matendo yake hayo, Bwana yule aliye mteu ambaye ni Boscow Ntaganda wa Pili ajaye kwa jina la LUSIFA amekuwa akisikika mara kwa mara akimsifu Makonda kuwa ni mchapa kazi.

Kwamba Bwana Bosco Ntaganda wapili ajaye kwa jina la LUSIFA anasema Makonda huwa natekeleza kazi zake hizo anazo mtuma yeye mwenyewe kwa uaminifu mkubwa, ambazo Marekani wamesema Makonda anafanya haya

1. Anaua watu wasio na hatia( Denial right to life)
2.Anateka anatesa raia (Denial right to Liberty
3.Anapoteza watu, anahatarisha usalama wa watu.( Denial right to Security of persons )
Tutaelewana tuu taratibu.




Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hiyo kodi yetu mpaka ikodishe meli nadhani raia watakuwa wapo tayari barabarani wakipinga hali ngumu ya maisha

Sent using Jamii Forums mobile app
Watanzania wengi wanadhani vitu vingi vina gharama kubwa sana na haviwezekani.
Kabla ya Magufuli watu walidhani kununua ndege ni pesa nyingi sana na Tanzania haiwezi, naona Magufuli kawaonesha hawakuwa sahihi wenye dhana hiyo.
Kama Kinana alikuwa anamiliki au anaanasimamia meli kadhaa na wapo watanzania wengine wanamiliki au wanaendesha/kusimamia meli unafikiri kukodi meli ni bei kubwa hivyo?
Watu wasingeweza kusafirisha mizigo ya mazao kwenda nje, au kuleta mizigo ya mitumba nchini kwa meli.

Alafu siku nyingine uwaze zaidi ya unacho soma juujuu, nimesema pale vizuri kabisa kama anaungwa mkono na watu wa juu yake hilo halishindikani. Kwa maana inaweza kutumiwa ofisi ya juu yake ikafanya mualiko wa madaktari toka ughaibuni kama vile alivyoweza kuleta meli ya wale madaktari wachina kuja kutibu watu, au umeshau?

Si alikuwa Makonda huyu huyu? Kuna watu huko duniani ni mabingwa wa mambo mengi na wao hawana mipaka wala hawafungamani na serikali moja au mtu mmoja, hufanya kazi na mtu yeyote duniani ili mradi pesa tu.
Hujiulizi waasi wa viata mbalimbali za wenyewe kwa wenyewe wanapata silaha wapi?
Wanapata supplies za mafuta na ammunition wapi wakati ni illegal duniani kote kuuza silaha kiholela?

Think far!
 
Back
Top Bottom