Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kaenda kujifunza ujasusi akirudi ameiva CIA hawajali kabila sla rangi kwenye jeshi lao.
Kuna watu kibao ambao hawajapigwa ban ila wamepinga ushoga na kuchukua hatua,ushoga hapa sio issue!
Bishana na vyombo vya habari vya kimataifa, mimi sikuwezi:
Tupate kwanza Wadhamini,Katika sababu zilizotajwa kwa Makonda kuzuiliwa kwenda Marekani ni "kuwanyima watu haki ya kuishi na usalama wao" Hi ni sentensi nzito kwa watu wanaofikiria mambo kwa umakini, kwa kuwa unapomnyima mtu haki ya kuishi ina maana huyo mtu haishi tena, hayuko hai tena kwa kuwa umeondoa haki yake ya kuishi, au umemnyima haki yake ya kuwa hai - umemuua. Hilo ndilo wanalosema USA juu ya Makonda.
Watu wengi wanafikiria kwamba Makonda amezuiliwa kwenda USA kutokana na msimamo wake juu ya suala la ushoga, lakini ni wazi kutokana na kauli ya USA kwamba kuna zaidi ya hilo. Je kuna mambo ambayo Watanzania tumefumbwa kwa muda mrefu sana na serikali yetu lakini USA wana taarifa zote?
Kumekuwa na taarifa nyingi kuhusiana na watu kuuwawa, kutekwa na majaribio ya kuuwawa ncini ambazo serikali haijawa wazi sana kuzieleza au kuonyesha kuwa inayafanyia kwa uzito upelelezi wa hayo matukio. Kuna dalili basi, kwamba hawa USA wana ufahamu wa haya mambo kuliko tunavyofikiria.
Ipo siku ukweli wote utawekwa wazi. Lakini kwa sasa, Makonda kutuhumiwa kwamba amekuwa akiwanyima watu haki ya kuishi ni jambo kubwa sana!
Reference:Makonda apigwa 'stop' kuingia Marekani
View attachment 1343097
CCM njooni huku mumtetee na kumpa pole mwanachama wenuYuko kwenye kitimoto anapitia wakati mgumu sana.... Sa hivi ni either ADB au watanzania lazima upande mmoja utoswe...
Yapo mengi mno Hawa mashetani wamefanya mkuu, mwisho wao hatimaye umefikaMkuu mbona haujamtaja kamanda chacha wangwe? Jaribio la kumuua Kagenzi aliyekuwa mlinzi wa Dr.slaa.
Vipi jaribio la kumpa sumu zitto kule bagamoyo?
Kwa sababu Makonda siyo CCM na CCM hawana tabia ya kutetea mtu anayefanya ujinga hata akiwa mwenzao! Kwa kifupi Makonda anachukiwa sana.Wakuu, habari
Naona IDs zote za CCM hazimtetei makonda au kumpa pole kwa kuzuiwa kuingia marekani kuna nini kimetokea?, wamemzilia?, mwenye taarifa atuambie
Mbona USA ilimnyima haki ya kuishi yule jenerali wa IRANI?Tusiwe kasuku
Wew unajua aliko Ben Saanane? Rais anapokea ripoti ya makinikia Dar halafu Makonda anafanya ninii Dodoma? Ni kwa Nini alisema Roma atapatikana Jpili? Hivi unaweza kuniambia mkuu yupi wa mkoa Tanzania anaweza akavamia studio na askari wenye bunduki wa ikulu? To conclude angalia akili ya Bashite pia angalia akili za Musiba hahafu tafakari kwa kina ujue Nani anawatuma,ukumbuke pia Nape alitumbuliwa na kutishiwa bastola mchana kweupe. Usisahau pia siku ya shambulio la Lissu lililokusudua kutoa uhai wake walinzi hawakuwepo area DHuo ndio ukweli Mkuu. Lakini kuna watu hapa kwa makusudi kabisa wanataka kuwapotosha Watanzania wajikite kwenye kudhani Makonda anazuiwa kwa sababu ya msimamo wake mambo ya ushoga. Ukweli ulio wazi ni kwamba USA wanamtuhumu Makonda kuhusika na kuua watu. Sasa watu gani Makonda kahusika kuwaua? Hilo ndilo swali Watanzania tunapasa kuwashikia bango USA watufafanulie.
Naomba uwa tag wote kwenye uzi huu,labda bado hawajapata habari🙂Wakuu, habari
Naona IDs zote za CCM hazimtetei makonda au kumpa pole kwa kuzuiwa kuingia marekani kuna nini kimetokea?, wamemzilia?, mwenye taarifa atuambie