Paul Makonda: Rais Samia anarogwa sana na watumishi wake

Amewajuaje wasirikina kama yeye siyo miongoni mwao?? Kutwa Kiongozi Mkubwa wa Mkoa kuhubiri ushirikina. Upumbavu wa hali ya juu. Kuwaambia watu kwamba kuna wanafanya ushirikina kwa watoto wenu ndiyo maana wanakuwa walevi, unategemea nn kama siyo kuwagombanisha raia anaowaongoza?? Hafai kuwa Kiongozi.

Hivi Tanz ina Mkuu wa Mkoa mmoja tu?? Napata sababu kwamba kwanini Wanaccm wenzie walimkataa kuwa Muenezi wa Chama chao. Sasa ni wakati nao Arusha wamtose. Vinginevyo watafarakanishwa kwa mahubiri ya kishirikina kila kukicha.
 
Mlozi yeyote namba moja atasema hivyo.
 
Hao walozi hawako serious. Mbona hakuna matokeo?
 
Nchi inavituko sana yeye amejuaje kama kweli yeye Hamlogi ? Uyu hajui Dunia katika hali ya kawaida huwezi tamaka maneno kama aya kwa Mkuu wa nchi ,kama anajua kwanini wasiambizane wakamalizana huko ,so ukisema mbele za watu inakusaidia nini
 
Kibongobongo ukishakuwa bosi lazima urogwe sana, na Kila mtu ana namka yake yakuroga.

Ukiwa kiongozi, ukilala ukiamka muombe Mungu akupe hekima na busara sana, akupe wepesi uishi Kwa haki na kutenda haki
 
Kwa mara kwanza ushirikina umeingia state house
 
Si aseme tu kuwa mama anamkubali sana hata alitaka kupewa uwaziri sema timu msoga haimtaki kabisa! Ila muhula ujao ana uhakika wa uwaziri hata asipogombea ubunge tena akiendelea kucheza vizuri uwaziri mkuu unamuhusu!
 
Huyu ndiye aliyekuwa anamtafutia Jiwe Wale Waganga wake 500
 
Nikifikiria yale mafuriko yanayokuwa kwa Mwamposa, Kuhani Musa, Kiboko ya wachawi (enzi zile), n.k., n.k., naanza kuamini Makonda si mjinga: anaongea na nafsi za Watanzania wengi kuliko tunavyofikiri.

Akiwa kama msanii hivi anaweza kuwa kioo cha jamii huyu jamaa. Inasikitisha. Imani za kishirikina ndio ada ya taifa hili!
 
Ina uhusiano gani na maendeleo ya Arusha ? Aache utoto wake na uchawa......afuate JD ya RC....period
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…