Kuna ' Members ' kama Watatu hivi hapa hapa walianzisha ' threads ' zao wakijiaminisha kabisa na wakitaka Makonda ' atumbuliwe ' upesi na nikawaambia kuwa wanapoteza muda Wao na hilo kamwe halitowezekana. Kwa wenye Akili sawasawa Vichwani mwao watakubaliana na Mimi kuwa hadi Makonda anakuja na Kauli hizi za Nyodo na Dharau ni kwamba kuna Mtu anampa Kiburi, Jeuri, ana Faidika nae, anamlinda na ameshamuhakikishia kuwa hatomtoa hadi atakapomaliza Muhula wake huu wa Kwanza. Kama ni Makonda ' Kutumbuliwa ' hapo alipo hilo lingefanyika Siku nyingi sana ila jiulizeni ni kwanini ' hatumbuliwi ' ila wale wanaofanya ' just minor blunders ' za Kiutendaji hawacheleweshwi ' Kutumbuliwa ' katika nafasi zao? Namalizia kwa Kusisitiza kutokana na sababu zangu za ndani kabisa kuwa RC Makonda ' hatotumbuliwa 'ng'o hapo alipo na atamaliza pamoja na ' Mteuwaji ' wake hadi mwisho wa Muhula wake. Mkiambiwa kuwa kuna Watu wanajua ' Kuroga ' vizuri nchini Tanzania muwe mnaamini na mnatuelewa.