Petroli na Diesel bei Juu. Dola yaelezwa kuwa sababu ya bei kupaa
aposto kuna muujiza………😂😂😂😂🤣
Muujiza gani?: bei ya petrol na disel zimelipuka badala ya kupanda

Aiseee huu ni mlipuko sio mfumuko….
Sema mlipukooooooo😂😂😂😂🤣

Samia uchumi umemshinda kabisa
 
Hali inazidi kuwa Tete,tunarudi Kwa mwaka Jana

======
MAMLAKA ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), imetangaza bei mpya za mafuta ambazo zinaonesha Petroli imepanda kwa sh. 443 huku Dizeli ikipanda kwa 391 kwa Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa bei mpya zilizotangazwa leo na EWURA, Petroli iliyokuwa inauzwa sh. 2,736 imepanda hadi 3,199 huku Dezeli iliyokuwa inauzwa sh. 2,544 imepanda hadi 2,935, kwa Dar es Salaam bei ambazo zitaanza kutumika kesho Jumatano, Agosti 02,2023 saa 6:01 usiku.

Aidha EWURA imesema sababu za mabadiliko ya bei hizo kwa mwezi Agosti 2023 ni changamoto za upatikanaji wa Dola za Marekani, mabadiliko ya sera za kikodi, kushuka kwa thamani ya Shilingi dhidi ya Dola ya Marekani, ongezeko la gharama za mafuta katika soko la dunia na gharama za uagizaji wa mafuta.

Imesema kwa mwezi Agosti 2023, bei za rejareja za mafuta katika Mikoa ya Tanga yatauzwa sh. 3,245 na Mtwara ni sh. 3,271.
Nchi ipo kwenye outopiloti
 
Bei mpya tayari au inaanza kesho? Nina safar ya likizo kwenda Dar. Nikajaze saivi kama imeshaanza nabeba abiria kila.mmoja 30k 😆😆😆
 
Ongezeko la 400 kwa lita ni kubwa sana
Hapo kuna watu wanapata mabilioni ndani ya siku 1 maana kama mtu alikuwa na lita milioni 2 tayari faida kapata na hii ilitegemewa maana mafuta yalifichwa mapema mno, maana bei ilishajulikana itapanda
Mwezi unaokuja itapanda tena maana dollar itakuwa imefika 2700 hivyo lita itafika 3500 hadi mwaka uishe mafuta yatakuwa 4000 huko

Sent from my M2006C3LG using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom