Nimekupata kamanda, kutopoteza sifa unamaanisha kwenda sawa na matakwa ya chadema ya katiba mpya, au sio? Ukweli ni kuwa sasa ndo ataweza kuongoza na kufanikisha vizuri.......angeendelea km alivyoanza kuwasikiliza hawa jamaa kiroho safi na kiupole, saa hz angelikuwa ameshaanza kuona joto la jiwe; ye akiwatangazia wananchi kuwa wafanye usafi, chadema wangepita baadae kuwaambia marufuku kufanya usanyi. Tumeyaona sana haya kipindi cha kikwete. Ajaribu aone! Kawaonyesha ubinadamu tu kidogo wa kuwatoa jela na kuwafutia kesi, tayari wanampangia habari za katiba mpya na maandamano km shukrani