Picha: Rais Samia Suluhu aongoza kikao cha Baraza la Mawaziri

Picha: Rais Samia Suluhu aongoza kikao cha Baraza la Mawaziri

Ile kubwa Chamwino ndiyo iko kwenye ujenzi,ila mule ndani kuna jengo la ofisi ya Rais na liko na ukumbi mkubwa tu wa kufanyia kikao kama hiki..
Nadhani pia wameangalia mawaziri wengi kwa muda huu wapo DSM although haina justification ya gharama maana kiukweli tunaingia gharama kubwa sana kuhudumia Ikulu kuu mbili.

But kuna gharama hatuwezi kuziepuka just like kuoa wake wawili inabidi ukubali tu. Nyerere alishatuingiza kingi kuhusu kuhamia Dodoma na bwana yule akakazia kuhamia huko hakuna ujanja ain't no turning back kwa sasa.

Tumelivagaa wenyewe Ila ndio inatupa akili ya kuhoji kodi tunazolipa
 
Ingekuwa kashindwa saa hizi makongamano ya katiba yangekuwa yameshafanyika, si mwanza tu bali nchi nzima. Pia mbowe angekuwa ameshaachiwa ndani ya siku moja km walivyoamuru chadema. Km hilo halitoshi, chanjo isingekuwepo km mwenye chuki pole pole anavyotaka na hata tozo ingekuwa imeshaondoka. Atapiga maendeleo na hamtaamini na nia zenu mbaya.......mtayasema wenyewe, mtake msitake. Naamini ni suala la muda tu
Umeongea utoto Sana. Acha niishie hapo
 
Kwahiyo hayo ndo unahitimisha kuwa ameshindwa?!! Hivi ulisifia chochote alipogundua hilo suala la wizi? Maana hata hatujui ulianza lini. Kesi ni mchakato, inatoka inapokamilika si pale wanapotaka watu fulani waliokaa kimitego na majungu ba husda.

Hilo suala alilolitangaza waziri mkuu; je, leo unapolaumu umejiridhisha kuwa factors zote zilikuwa constant kutoka siku hiyo hadi hii leo?!!

Factors zipi boss, IGP alisema ndani ya siku 7 atatoa taarifa rasmi ya huo wizi, mpaka leo kimya na ni zaidi ya mwezi. Au unadhani ukiongea kiswahili na kuchomeka vijimaneno vya kiingereza ndio utaonekana msomi?

Hayo uliyotaja ndio hitimisho lako kuwa amefanikiwa? Au unajichanganya nini boss. Sina chochote cha kusifia kwa hayo majizi ya kura, na aliyegundua hilo suala la bomba la mafuta alikuwa Mkuu wa wilaya, ila hao wanajiita wakubwa wakalipotezea maana wanalijua kwa undani wake. Kwa maneno marahisi wana mahusiano na huyo mwizi wa mafuta.
 
Ulitaka ashauriwe na binladen?
Hii nchi ni ya kipuuzi Sana wahalifu wakubwa na wahujumu uchumi wakubwa wanapeta mitaaani, yaani mtu kajiunganishia Bomba la mafuta yupo kitaa anavuta shisha, mwingine kakutwa na mapesa lukuki kwenye ndoo nyumbani anakula Bata anakuja kukamatwa Mbowe kisa kudai katiba eti ni GAIDI[emoji144]
 
Clerk at job

kuna haja ya chokochoko mpya(katiba)

Ccm msiendelee kutupima
 
Ingekuwa kashindwa saa hizi makongamano ya katiba yangekuwa yameshafanyika, si mwanza tu bali nchi nzima. Pia mbowe angekuwa ameshaachiwa ndani ya siku moja km walivyoamuru chadema. Km hilo halitoshi, chanjo isingekuwepo km mwenye chuki pole pole anavyotaka na hata tozo ingekuwa imeshaondoka. Atapiga maendeleo na hamtaamini na nia zenu mbaya.......mtayasema wenyewe, mtake msitake. Naamini ni suala la muda tu
Hivi ndivyo vipimo vyako vya kuweza?

Hakika utakuwa hupo sawa!
 
Factors zipi boss, IGP alisema ndani ya siku 7 atatoa taarifa rasmi ya huo wizi, mpaka leo kimya na ni zaidi ya mwezi. Au unadhani ukiongea kiswahili na kuchomeka vijimaneno vya kiingereza ndio utaonekana msomi?

Hayo uliyotaja ndio hitimisho lako kuwa amefanikiwa? Au unajichanganya nini boss. Sina chochote cha kusifia kwa hayo majizi ya kura, na aliyegundua hilo suala la bomba la mafuta alikuwa Mkuu wa wilaya, ila hao wanajiita wakubwa wakalipotezea maana wanalijua kwa undani wake. Kwa maneno marahisi wana mahusiano na huyo mwizi wa mafuta.
Hili jambo lina kitu nyuma yake, siyo bure.

Toka mwanzo limekuwa kama halikuwa tukio la kustua kabisa.

Ni kama wanasubiri lipowe kabisa na watu wasahau kwamba halikutokea.

Huyu 'Maza Mizinguo' nimeshamwona ni mtu wa 'mission mission' za chini chini. Nchi ikitulia vizuri, huyu anazo dalili za upigaji mkubwa sana, hasa kwa ndugu zake na watu walio karibu naye.
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan aongoza Kikao cha Baraza la Mawaziri kilichokutana leo tarehe 07 Agosti, 2021 Ikulu Jijini Dar es Salaam. https://t.co/Nm1ct3TGZi
View attachment 1884186

7 August 2021

PROF: LIPUMBA AMZUNGUMZIA MBOWE KUHUSU SUALA LA UGAIDI.

Prof. Ibrahim Haruna Lipumba asema Haingii akilini gaidi na mhaini akapelekewa salamu za rambirambi tarehe 8 Julai 2021 na Rais ambaye ni amiri jeshi Mkuu wa vyombo vyote vya ulinzi na usalama, halafu tarehe 23 Julai 2021 Freeman Mbowe akakamatwe kwa ugaidi wa mwaka 2020. Maana rais kila siku hupewa taarifa za usalama za nchi nzima, iweje tarehe 8 Julai 2021 Freeman Mbowe apelekewe salamu za pole za rambirambi za msiba wa kaka yake. Ina maana rais alikuwa hana taarifa za ugaidi wa Freeman Mbowe mpaka tarehe 21 Julai 2021 siku ya kongamano la CHADEMA juu ya katiba ya nchi, anahoji Prof. Ibrahim Haruna Lipumba.

Source : StarTV Habari
 
Kuruhusu kushauriwa na lile genge la yule mtawala muovu.
Fisadi n mkwele ndiyo mshauri wake ila tumepatana chochote tunacho panga kikibuma lawama tutazipeleka kwa hayati Magufuli
 
Back
Top Bottom