Picha ya Rais: RC Makonda amtaka Msanii Idris Sultan kujisalimisha kituo cha Polisi

Picha ya Rais: RC Makonda amtaka Msanii Idris Sultan kujisalimisha kituo cha Polisi

Kama Mimi nj idris nisingeenda kuripoti. Kwakuwa simfahamu baba keagan ni nani?
Huyu Mr ziro anataka kutolea matamko cheo chake cha kiserikali kupitia jina la kihuni mitandaoni?
Wahed gademit kabisa ndio aliscore FFFFFFFFFFFFFF Form4 nisawa na magu atoe amri kwa jina la babajesca, could it sound? Yani tunaongozwa na watu malimbukeni na washamba kuipitiliza.
 
Ndiyo maana nikasema ni kosa letu sisi wananchi. Tukimkataa ni lazima atamwondoa. Na siyo kumkataa kwenye mitandao kama tunavyofanya sasa! Kumkataa kwa vitendo!
Ni vizuri unavyosema hivo ukatoa na maelekezo pamoja na mafundisho nini kifanyike, ikiwa na maana kuwa hamasa ukizingatia kuwa huyo jamaa ni mkurupukaji ndo mana hata viongozi wenzie na wananchi kwa ujumla hawampendi
 
Tayari kisha ambiwa ku report kituo chochote cha polisi
Nani kamwambia yy MTU anajiita baba keagan unaenda polisi? Ni sawa hapa remote nikwambie kuripoti polisi waambie makonda kasema nonsense jamaa anadhirisha ziro yake form 4
 
Ni vizuri unavyosema hivo ukatoa na maelekezo pamoja na mafundisho nini kifanyike, ikiwa na maana kuwa hamasa ukizingatia kuwa huyo jamaa ni mkurupukaji ndo mana hata viongozi wenzie na wananchi kwa ujumla hawampendi
Maelezo gani taena mazee wakati nimesema ni wananchio wote kwa umoja wetu kumkataa? Nini kifanyike? Tumkatae.
 
@"Chachu Ombara,
Nasikia Idrisa analeta furaha pale jumba kubwa. Makonda amechemka sana. Kigwangalla hongera naon unafanya kazi vyema. Idrisa hana kosa lolote
Naona umehamia chadema kabisa, hadi unamponda boss wako
 
Mkuu wa Mkoa Dar es Salaam, Paul Makonda kupitia ukurasa wake wa Telegram, kwa jina la Baba_Keagan amepakia ujumbe unaosema ''Naona mipaka ya kazi yako huijuwi. Nenda sasa hivi kituo chochote Cha polic uwambie Makonda kaniambie nije utakuta ujumbe wako''
​
Kupitia ukurasa wake wa Twitter, mchekeshaji Idris Sultan alipakia picha mbili za Rais Magufuli ambazo zimehaririwa na kuandika maneno haya "Kwa siku moja tukabadilishana kazi ili a-enjoy birthday yake kwa amani''

Ikumbukwe jana ilikuwa ni siku ya kusherekea mfanano wa siku ya kuzaliwa kwa Rais Magufuli na watu, taasisi na mashirika mbalimbali ya walituma salamu za siku ya kuzaliwa.

Kuna wengine walienda mbali mpaka kutengeneza video za utani, mfano Mchungaji muhuni, Masanja Mkandamizaji alipakia video ikimuonesha akiimwagia maji picha rasmi ya Rais Magufuli inayotumiwa kwenye ofisi,taasisi na mashirika mbalimbali kwa mujibu wa sheria.



======

UPDATES

Baada ya mchekeshaji Idris Sultan kutakiwa ajisalimishe Polisi, Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk Hamisi Kigwangalla amesema yupo Tayari kumuwekea Mwanasheria wa kumtetea na kumdhamini Msanii huyo.

Ameyasema hayo kwenye Ukurasa wake wa Twitter. "Nimeambiwa kuna msanii wa vichekesho anatafutwa na polisi, akikamatwa mniambie, nitajitolea mwanasheria wa kwenda kumuwekea dhamana na kumtetea. Rais wetu ni mtu wa watu na imejidhihirisha kwa jinsi wananchi walivyojitolea kumuombea dua siku ya kuzaliwa kwake! Wameonesha upendo". Amesema Kigwangalla.

Nadhani Ni ucheshi tu yaani comedy, kwani angeshindwa kuwaambia police wamkamate. Huyu dogo nayeye kajitakia muwage munaangalia watu wakutania, siungeenda kwenye party ya Irene owoye ukawatania huko
 
Kibailojia iko hv .:wanawake tuna asili ya mood swings ..hata km sio mjamzito tuna asili hizo ...iwe karibu na kipindi cha mp au mwezi kuandama!MTUVUMILIE🤔
 
Halafu nchekie kwenye Google huyo mutu kwa avatar yako alishakufa au bado yupo hai?
Huyu ni Dustin Hoffman na yuko hai. Picha ya karibuni ni hii. Ana miaka 82 sasa.

1572450062901.png
 
Vinyago vya Trump anavyotengenezewaga angeshakamata watu wote duniani
Trump karibu kila Jumamosi watu wanamchamba yeye, familia yake, baraza lake la mawaziri, mkewe, mpaka vimchepuko vyake. Saturday Night Live.

Na hakuna mtu kukamatwa wala nini.

Huko kwa Mnyamani ukijisahau ukapiga chafya ikasikia umepiga chafya kwa kusema "raisiiii" unapigwa pingu na kupelekwa selo chapchap.

Umemdhalilisha rais.

Rais ndiye mtu dhalili kuliko wote katika nchi, kakubali kufanya kazi ya kuongoza watu, kazi ya lawama, kazi ya matusi.

Kinga yake dhidi ya matusi inatakiwa kuwa ndogo kuliko mtu mwingine yeyote Tanzania.

Waswahili waliposema "Ukubwa gunia la chawa" walikuwa na maana sana.

Tatizo kwetu wakubwa wanataka sifa tu, hawataki karaha za uongozi.

Hawaelewi maana ya "Noblesse Oblige".

Anayepewa talanta zaidi, atadaiwa zaidi.

Atadaiwa maendeleo zaidi, atadaiwa uvumilivu zaidi, atadaiwa kutokuwa na privacy zaidi, atadaiwa kuchunguzwa zaidi, n.k.

Na kama anajua hawezi hayo, asigombee uongozi. Mbona wengine tusiotaka kutukanwa na kukejeliwa na kila mtu tumekataa uongozi?
 
Naona mipaka ya kazi yako huijuwi. Nenda sasa hivi kituo chochote Cha polic uwambie Makonda kaniambie nije utakuta ujumbe wako''

🤔🤔🤔 Leadership skill iko wapi tena? OMG

 
Makonda chukua time tumekushtukia hacha usanii wa Kishamba. unataka kujifanya una uchungu na mh Raisi kuliko mama Janeth na watoto wake wakina Suzana Maghufuli

Ulikua hivi kwa kikwete alivyotoka tu madarakani sasa hivi unawadharau vibaya mno , na magufuli akitoka madarakani utamuona hafai kama ilivyo kwa familia ya JK

Mh Raisi Maghufuli hawa viongozi njaa type za Makonda ndio wanaokugombanisha na kukutengenezea chuki kwa wanachi wako
 
Kama Mimi nj idris nisingeenda kuripoti. Kwakuwa simfahamu baba keagan ni nani?
Huyu Mr ziro anataka kutolea matamko cheo chake cha kiserikali kupitia jina la kihuni mitandaoni?
Wahed gademit kabisa ndio aliscore FFFFFFFFFFFFFF Form4 nisawa na magu atoe amri kwa jina la babajesca, could it sound? Yani tunaongozwa na watu malimbukeni na washamba kuipitiliza.
Yaani mpaka hasira, huu ushamba umekuwa sasa kama sifa kwa taifa
 
Kamgusa ampae riziki ya kutamba mjini hana wivu kuliko mama j
 
Back
Top Bottom