Picha ya Rais: RC Makonda amtaka Msanii Idris Sultan kujisalimisha kituo cha Polisi

Picha ya Rais: RC Makonda amtaka Msanii Idris Sultan kujisalimisha kituo cha Polisi

this issue ukiondoa ushabiki usio na Tija na ukaiangalia kutoka katika angles toffauti (point of views) unakuta hakuna aliesahihi, wote Idris, baba Keagan na kigwangalla wana makossa..

Idris kuedit picha kama hiyo sio Sawa maana inaweza leta msuguano wa kimtazamo kwa watu tofaut( tayar umeshatokea). na kama akiachwa bila hatua yoyote kuchukuliwa atafungua ukurasa wa watu kumuedit mh. Rais wanavotaka maana itakua kitu cha kawaida, ikumbukwe magufuli sio trump na hatuko marekani, kule anaeditiwa mpka kwenye photo za mashoga, HATUTAKI KUFIKIA HUKO...

baba Keagan alichofanya si sahihi pia kutoa tamko kwenye ukurasa badala ya kufata protocol ( msiniuize hayo mambo ya protocol) sio Sawa Tena RC mzima , wengine tunajaji hii kitu kama misifa na Kiki kwa raia , na ningekua Idris nisingefika kituo chochote.

kigwangala na yy hatupo Sawa kwa sababu anachochea japo na yy tunajua kapata free kick.

Idris apewe onto ili hizi inshu za kuedit zisije kwenda viral kma kwa trump.

tusikilizie ANKO NA YY ATASEMAJE NA KUMTETEA NAN, maaan amnesty wanamspy pia
😃
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] huo nimkwara wa makonda baada ya idriss kuedit picha za Mheshimiwa kuhusu birthday yake. View attachment 1248858
Kwamba Magufuli hawezi kupiga pozi kama hili au kuna jingine lipo chini ya zuria?
Mbona yule mzee mwenyewe hanaga shida sana kama wasaidizi wake wanavyotaka kutuaminisha kwamba hata kutaniwa asitaniwe kweli? Tena utani umekuja siku mahususi ya kusherekea kuzaliwa kwake, hivi angetokea mtu na ndoo ya maji akapiga kupwaaa kwa mzee hao jamaa si wangempa kesi ya uhaini.
 
Naona hujui historia yao! Hapangiwi!! aliishasema yeye na bandari salama hata kama hajui kusoma!!
Ndiyo maana nikasema ni kosa letu sisi wananchi. Tukimkataa ni lazima atamwondoa. Na siyo kumkataa kwenye mitandao kama tunavyofanya sasa! Kumkataa kwa vitendo!
 
Mkuu wa mkoa wa Dar amemtaka mchekeshaji Idris Sultan ajisalimishe kituo chochote cha polisi kwa kosa la kuihariri (edit) picha ya Rais wa jamuhuri ya Tanzania ndgu JPM. Maoni yako kama mpenda haki, mzalendo wa nchi hii. Je wito wa Makonda ni final say au mahakama ndio yenye jukumu la kumuita mtu yeyote anaevunja sheria? Je kisheria Makonda yuko sahihi? Je nikosa kisheria kuhariri picha ya Rais bila kuiathiri? Msaada wanasheria mtusaidie.
Screenshot_2019-10-30-16-11-48-64.jpeg


======

UPDATES

Baada ya mchekeshaji Idris Sultan kutakiwa ajisalimishe Polisi, Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk Hamisi Kigwangalla amesema yupo Tayari kumuwekea Mwanasheria wa kumtetea na kumdhamini Msanii huyo.

Ameyasema hayo kwenye Ukurasa wake wa Twitter. "Nimeambiwa kuna msanii wa vichekesho anatafutwa na polisi, akikamatwa mniambie, nitajitolea mwanasheria wa kwenda kumuwekea dhamana na kumtetea. Rais wetu ni mtu wa watu na imejidhihirisha kwa jinsi wananchi walivyojitolea kumuombea dua siku ya kuzaliwa kwake! Wameonesha upendo". Amesema Kigwangalla.


 
Wenzake "kiki" wanazitafutia kwenye video za "faragha" huyu umaarufu kautafuta kwa kukatiza mbuga za Serengeti kwa baiskeli.
 
Huyu Baba Keagan ndiyo nani? Uandishi wake unatia mashaka sana. Halafu, mletamada tusaidie tujue kilichotokea. Umeandika kana kwamba tunajua kama wewe. Where is your evidence? Inasikitisha sana!
Wewe peke yako ndio hujamuelewa mleta mada usituchanganye na sisi, mleta mada amesema hivi "rc wa dar Basheite ameagiza msanii sultani ajipeleke mwenyewe kwenye kituo chochote cha polisi kitakachokuwa karibu naye kwa kosa la kuandika habari ambayo rc anaona kama ya kumdhalilisha bosi wake (rais)"
 
Hawa nao si wangekua wanaua kabisa? Huko marekani walitengeneza sanamu la Trump akiwa uchi sembuse picha tu tena mtu anakua amechoka anaamua kucheza na photpshop kama sehemu ya kupumzikia?
502776.jpg
 
Alipotea katika mazingira ya kutatanisha then taarifa ikasambaa kwny media then baadae Kipanya akaibuka akasema nashukuru wa-Tz dua zenu Mungu amezisikia niko salama na hakuongea chochote tena.

Mwaka gani huo??
 
Mkuu wa Mkoa Dar es Salaam, Paul Makonda kupitia ukurasa wake wa Telegram, kwa jina la Baba_Keagan amepakia ujumbe unaosema ''Naona mipaka ya kazi yako huijuwi. Nenda sasa hivi kituo chochote Cha polic uwambie Makonda kaniambie nije utakuta ujumbe wako''
​
Kupitia ukurasa wake wa Twitter, mchekeshaji Idris Sultan alipakia picha mbili za Rais Magufuli ambazo zimehaririwa na kuandika maneno haya "Kwa siku moja tukabadilishana kazi ili a-enjoy birthday yake kwa amani''

Ikumbukwe jana ilikuwa ni siku ya kusherekea mfanano wa siku ya kuzaliwa kwa Rais Magufuli na watu, taasisi na mashirika mbalimbali ya walituma salamu za siku ya kuzaliwa.

Kuna wengine walienda mbali mpaka kutengeneza video za utani, mfano Mchungaji muhuni, Masanja Mkandamizaji alipakia video ikimuonesha akiimwagia maji picha rasmi ya Rais Magufuli inayotumiwa kwenye ofisi,taasisi na mashirika mbalimbali kwa mujibu wa sheria.



======

UPDATES

Baada ya mchekeshaji Idris Sultan kutakiwa ajisalimishe Polisi, Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk Hamisi Kigwangalla amesema yupo Tayari kumuwekea Mwanasheria wa kumtetea na kumdhamini Msanii huyo.

Ameyasema hayo kwenye Ukurasa wake wa Twitter. "Nimeambiwa kuna msanii wa vichekesho anatafutwa na polisi, akikamatwa mniambie, nitajitolea mwanasheria wa kwenda kumuwekea dhamana na kumtetea. Rais wetu ni mtu wa watu na imejidhihirisha kwa jinsi wananchi walivyojitolea kumuombea dua siku ya kuzaliwa kwake! Wameonesha upendo". Amesema Kigwangalla.


Sasa hapa naona Kigwangalla anapinga maamuzi ya makonda.
Ngoja tuone ni nani mwenye sauti kati ya MAKONDA NA KIGWANGALLA
 
Back
Top Bottom