Kauli ya mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam ndugu Paul Makonda ya kumtaka Idris Sultan kuripoti kituo chochote cha polisi ilikuwa ni kauli tata pia iliyojaa utani ndani yake.
Hapana shaka kuwa ndugu, Paul Makonda anafahamu fika kuwa Idris Sultani ni mchekeshaji, hivyo kutumia namna yake ya Comedy kufikisha ujumbe wa kumtakia heri mheshimiwa raisi Magufuli.
Makonda naye kwa namna fulani akijuwa kabisa kuwa, Instagram sio mahali sahihi kwa kutoa oda ya mtu fulani kukamatwa, kwa lengo lilelile la kuchangamsha genge aliposti kuwa Idris aripoti kituo chochote cha polisi.
Sikuona ubaya wa kauli zote mbili kwani wote hawakuwa serious. Kitu kilicho nishangaza ni kuona watanzania wanavyo lishadadia jambo hili kana kwamba ni kweli Idris ameisha kamatwa ama ameripoti kama alivyo takiwa.
Watanzania tuache mambo ya kushadadia vitu kwenye mtandao na pia kuwapa nafasi kubwa na kuwaogopa wateule wa raisi kana kwamba wako juu ya sheria.
Kama Idris amefanya kosa basi atahukumiwa kwa mujibu wa sheria na si kwa amri ya mtu fulani. Hakuna mwenye mamlaka ya kisheria kuamuru kumkamata mtu bila sababu na hata kama mamlaka hiyo anayo basi mahakama ndio muamuzi wa mwisho.