Mzembe flani
JF-Expert Member
- Jul 1, 2019
- 203
- 230
Kwamba Magufuli hawezi kupiga pozi kama hili au kuna jingine lipo chini ya zuria?[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] huo nimkwara wa makonda baada ya idriss kuedit picha za Mheshimiwa kuhusu birthday yake. View attachment 1248858
Na Baba Mwanaasha lakini ni sisi tulimwita mweneywe alitumia majina yake siku zoteHata Jk pia tulimwita Baba Ridh
Ndiyo maana nikasema ni kosa letu sisi wananchi. Tukimkataa ni lazima atamwondoa. Na siyo kumkataa kwenye mitandao kama tunavyofanya sasa! Kumkataa kwa vitendo!Naona hujui historia yao! Hapangiwi!! aliishasema yeye na bandari salama hata kama hajui kusoma!!
Wewe peke yako ndio hujamuelewa mleta mada usituchanganye na sisi, mleta mada amesema hivi "rc wa dar Basheite ameagiza msanii sultani ajipeleke mwenyewe kwenye kituo chochote cha polisi kitakachokuwa karibu naye kwa kosa la kuandika habari ambayo rc anaona kama ya kumdhalilisha bosi wake (rais)"Huyu Baba Keagan ndiyo nani? Uandishi wake unatia mashaka sana. Halafu, mletamada tusaidie tujue kilichotokea. Umeandika kana kwamba tunajua kama wewe. Where is your evidence? Inasikitisha sana!
chonde chonde mkuu naomba kujua ni ka mchezo gani hako π π π π π
Alipotea katika mazingira ya kutatanisha then taarifa ikasambaa kwny media then baadae Kipanya akaibuka akasema nashukuru wa-Tz dua zenu Mungu amezisikia niko salama na hakuongea chochote tena.
Mkuu wa Mkoa Dar es Salaam, Paul Makonda kupitia ukurasa wake wa Telegram, kwa jina la Baba_Keagan amepakia ujumbe unaosema ''Naona mipaka ya kazi yako huijuwi. Nenda sasa hivi kituo chochote Cha polic uwambie Makonda kaniambie nije utakuta ujumbe wako''
Kupitia ukurasa wake wa Twitter, mchekeshaji Idris Sultan alipakia picha mbili za Rais Magufuli ambazo zimehaririwa na kuandika maneno haya "Kwa siku moja tukabadilishana kazi ili a-enjoy birthday yake kwa amani''
Ikumbukwe jana ilikuwa ni siku ya kusherekea mfanano wa siku ya kuzaliwa kwa Rais Magufuli na watu, taasisi na mashirika mbalimbali ya walituma salamu za siku ya kuzaliwa.
Kuna wengine walienda mbali mpaka kutengeneza video za utani, mfano Mchungaji muhuni, Masanja Mkandamizaji alipakia video ikimuonesha akiimwagia maji picha rasmi ya Rais Magufuli inayotumiwa kwenye ofisi,taasisi na mashirika mbalimbali kwa mujibu wa sheria.
======
UPDATES
Baada ya mchekeshaji Idris Sultan kutakiwa ajisalimishe Polisi, Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk Hamisi Kigwangalla amesema yupo Tayari kumuwekea Mwanasheria wa kumtetea na kumdhamini Msanii huyo.
Ameyasema hayo kwenye Ukurasa wake wa Twitter. "Nimeambiwa kuna msanii wa vichekesho anatafutwa na polisi, akikamatwa mniambie, nitajitolea mwanasheria wa kwenda kumuwekea dhamana na kumtetea. Rais wetu ni mtu wa watu na imejidhihirisha kwa jinsi wananchi walivyojitolea kumuombea dua siku ya kuzaliwa kwake! Wameonesha upendo". Amesema Kigwangalla.
Wewe na baba Keagan wako mna uandishi mbovu sana. Nadhani mmesoma shule moja na matokeo yalifananaThihaka sio nzuri,
ningekua baba Keagan ningemuweka ndani mpk
apate msamaha wa Rais
Sasa hapa naona Kigwangalla anapinga maamuzi ya makonda.
Ngoja tuone ni nani mwenye sauti kati ya MAKONDA NA KIGWANGALLA
Upo sahihiWewe na baba Keagan wako mna uandishi mbovu sana. Nadhani mmesoma shule moja na matokeo yalifanana