Pointers kwa wote wanaohofia usalama wa maisha yao kwa sababu ya harakati zao

Yaani wewe unajua halafu Polisi hawajui!? Ahahahahaha!!!
 
Hii nimeshatoa angalizo wakati fulani. Nashindwa kuelewa ni kwanini mapaka sasa chadema hawajaweza kuliangalia hili suala. Teknolojia zipo nyingi na nyingine zipo affordable kabisa. Mambo ya kutegemea clips za jambotv sio poa kabisa
 
Nadhani tumefikia tipping point, kuanzia sasa watanzania tubadili mtizamo. Kinachowapa kiburi Polisi ni silaha wanazobeba, hizo zinawatia uoga watu uliochanganyika na ukondoo fulani hivi wa kuheshimu sheria au mamlaka zilizokasimiwa kwao ili kuzisimamia.
Watanzania tunahitaji sasa kujilinda wenyewe kwa silaha kama wafanyavyo Polisi. Haiingii akilini kwa silaha za kivita kutumika dhidi ya raia tena wasiokuwa hata na manati.
Wananchi washirikiane kutoa taarifa mtaani ya uwepo wa magari yanayohusishwa na kutekwa kwa watu, ikiwezekana kuwahoji wanaojitambulisha kuwa ni Polisi, kila mtu ahakikishe hachukuliwi kirahisi rahisi kama ilivyozoeleka. 😡
 
Wakati alipofariki Mzee Kibao, nilisema humu, watauwawa wengi zaidi. Mpaka kufikia uchaguzi. Haya yanaendelea, nilitoa ushauri kila mtu sasa ajilinde mwenyewe.

Maana policcm ndiyo watakufanyia tukio, wanarudi kwa mlango wa nyuma kusema si wao. Je kuna kikundi kisichogusika kinafanya kinavyotaka?

Basi kama haya yote hayafanywi na policcm, kila mtu awe na silaha wakitokea chuma imeisha hii.
 
Hii nimeshatoa angalizo wakati fulani. Nashindwa kuelewa ni kwanini mapaka sasa chadema hawajaweza kuliangalia hili suala. Teknolojia zipo nyingi na nyingine zipo affordable kabisa. Mambo ya kutegemea clips za jambotv sio poa kabisa
Wamezidi uzembe.
 
NI UKWELI USIOPINGIKA KUWA HT HAO MAJAMBAZI YA MACCM YATAKUFA 2. TN MUNGU ATAYAUA VIFO VIBAYA SN
 
Mtu kama Mdude, kwa level ya ukosoaji wake anaishi vipi Iwambi huko. Mimi naona kuna haja ya Chadema kuwa na mkakati, wanajisahau sana kiukweli.

Ulitaka aishi ILEMI au Mabatini,wapi ambako wasingemfikia?!
 
Pole kwa wafikwa wa janga hilo Mungu asaidie awe salama, na pia nchi yetu tuna mwingiliano kwa kiwango cha juu sana kwa hiyo si vyema sana kuenenda kwa visasi ila asasi za kiraia, kisheria, haki za binadamu na sisi raia tulaani yanayofanyika. Ninapozungumzia mwingiliano ni kwamba tukienda kivisasi itakuwa hatari huyo Mdude mimi ni kabila moja na yeye kiukweli sasa pia sisi ni wakristo tuna ndugu ambao ni wapo kwenye vyombo vya usalama pia ,tunandugu karibia vyama vyote vya siasa, tunamwingiliano wa kindoa na waIslamu na pia tuna mwingiliano wa kindoa na makabila mengine . . . Hapa ndo juhudi ya kumjua mtendaji kabisa unaikuta inahitajika kuliko kulichukia kundi fulani. Nipo tayari kurekebishwa . . . Ahsante.
 
Tatizo ni mchakato wa kumiliki silaha ambao wameuhodhi wenyewe na kufanya umiliki wa silaha kwa mwananchi wa kawaida kuwa mgumu. Dawa sasa, ni kutumia hizo hizo silaha wanazokuja nazo kutishia watu. Mwananchi yeyote anayejua kutumia silaha akifuatwa alenge kuteka silaha.
 
Kuna bodycam pia.

Ukiwa umeivaa hata ukikamatwa barabarani tayari sura na sauti zao zitajulikana tu.

Hizi si zama za ujima.
Tulipofikia,tunahitaji zaidi ya camera,

Juzi tu hapa askari wamerekodiwa tena siyo sura tu mchana kweupe wakikamata watu Kisutu mahakamani na baadae watu hao walokamatwa wameokotwa wamevunjwa viungo na kutelekezwa.

Polisi imekanusha kuwakamata watu hao na waziri kapiga siasa tu na maisha yanaendelea kama hakuna kilichotokea.

Hizo sauti na sura ukirekodi unazipeleka wapi?
 
Hakika Mkuu, hamna ugumu wowote ku outsmart Serikali na Dola yake, wengi ni vilaza ,ndio maana hawawez kuficha uovu wao

Jambo la msingi ni kua mbele zaidi.

Kamera zifungwe hata kwenye magari.
 
Kama pale katini palikua na Camera kweli walipofanyia Uhuni Kitima?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…