Pointers kwa wote wanaohofia usalama wa maisha yao kwa sababu ya harakati zao

Pointers kwa wote wanaohofia usalama wa maisha yao kwa sababu ya harakati zao

Bodycam inakusanya data na kuzituma kwingine on a real-time basis? Kama sivyo, wakikupoteza unapotea na data zako!
I am for whatever it takes.

Nadhani zipo ambazo zinahifadhi data kwingineko kiasi kwamba hata bodycam ikiharibika, bado data zako zitakuwepo mahala.

Mimi nina dashcam inayorekodi ndani na nje. Hata kama siendeshi gari, camera ina uwezo wa ku detect impact na kuanza kurekodi.

Na inahifadhi kila kitu kwenye app/ account.

Na hata kama bodycams hamna zinazopeleka data kwingineko, ni bora kuwa nayo kuliko kutokuwa nayo.

I am for anything that can help.

Sitaki watu wawe helpless kabisa.

Mfano huyo Mdude hata hatujui hao watu waliompiga wanafananaje.
 
Naona watu wengi sana hapa mnachangia comments zenu lakini bila ya kujua kwa undani kuhusu uzito wa tatizo ambalo Wananchi wa Tanzania wanakabiliwa nalo kwa Sasa.
Hali iliyopo hapa nchini kwa Sasa ni sawa kabisa na hali jinsi ilivyokuwa kule nchini Afrika Kusini enzi za Utawala wa Ubaguzi wa Rangi mara tu baada ya Chama Cha Upinzani Cha ANC wakati huo kufutiwa Usajili wake kama Chama Cha Siasa na kisha Chama hicho kilipigwa marufuku na Utawala wa Makaburu na mwisho kabisa chama hicho kutangazwa kuwa ni Kundi la Kigaidi.

Watu hao waliokwenda nyumbani kwa Mdude Nyagali na kumteka kwa nguvu wanaonekana walikuwa ni Task Force.
 
Hujaeleweka.
 
Wewe huko kwenu usukumani umeweka cctv nyumbani? Au unajisemea tu kwa kuwa uko majuu maboxini kwa hiyo unaona kila kitu ni rahisi?
Camera zipo kila kona ya nchi hii wewe.

Unaishi wapi wewe? Zizini?
 
Polisi wetu hata waliyoyafanya hadharani wanayakataa, sasa ukiweka kamera ndiyo watakubali? Juzi hapa wamebeba watu mchana kweupe kwenye magari yao hapa mahakam ya kisutu, na wakaenda kuwapiga na kuwadhuru wanachadema.

Siku hiyi hiyo Jeshi la Polisi walikataa kwamba sio wao na video zipo zikiwaonyesha wao wakiwakamata watu kisutu na kuwaweka chini ya ulinzi na kuwapandisha kwenye magari yao ya polisi.

Sasa nini kitawafanya wakubali kwamba wao ndio wahusika wa kila uovu nchi hii.

Wote tunaelewa anakingwa Mamaaaa ashinde, lakini huwezi kuwa mwehu kusema kwamba kwasababu Nyumba ya Mdude Nyagali haina kamera basi polisi hawahusiki.

Tundu Lisu aliposhambuliwa Dodoma waliondoa video wao hao hao polisi, na walikana hawahusiki.

Hoja kama hizi hazina faya yoyote, wananchi wantekwa majumbani na barabarani na polisi wamekanusha zote.

Nchi hii itapona tukipata jeshi letu wananchi, viongozi wakabaki na majeshi yao naamini tutawashinda.
Watu mna mindset za kichovu na kiunyonge sana.

Kwa mtaji huo watu wataendelea kupigwa kizembe zembe sana kwa sababu watesi wanajua wanadili na watu waoga.

So what kama polisi wakikataa kuwa wao ndo wanaoonekana kwenye video? Unategemea mhalifu akubali tu kirahisi rahisi?

Cha msingi kama mhalifu ndo yeye anayeonekana kwenye video, akubali au akatae kuwa ndo yeye, hiyo hainihusi.

Kinachonihusu ni mimi kujiridhisha ni nani na nani waliohusika halafu nitajua mwenyewe cha kufanya.
 
Naona watu wengi sana hapa mnachangia comments zenu lakini bila ya kujua kwa undani kuhusu uzito wa tatizo ambalo Wananchi wa Tanzania wanakabiliwa nalo kwa Sasa.
Kiongozi ulinzi na usalama wako unaanzia kwako binafsi, hata Yesu mwenyewe hakukaa hivi hivi alikuwa anatembea na kakikundi wamejizatiti kiulinzi.. kwa maana walijua wanawindwa na tawala ya kipindi hiko...

Ndio maana wale askari wa kuhani walipojitokeza kumkamata Yesu , Petro alimkata sikio yule askari akiitwa Maliko, ndipo Yesu akakataza yeye kama mkuu wa msafara wasianzishe vurugu, lakini isingalikuwa hivyo basi pale pangetosha..

Kumbuka wale waliokuja kumkamata ni askari kama leo walivyo polisi, hivyo inawezekana biblia isieleze kwa urefu yaliyotokea lakini ilitokea vurugu tena kubwa hadi kumkamata Yesu...

Wote tunasikitishwa na yanayoendelea, wanaharakati wanapaswa kujiweka katika hali ya tahadhari ya kiusalama, na vyama vyao vina jukumu la msingi la kuhakikisha ulinzi wao. Hii ni muhimu ili kuendeleza mapambano ya haki za binadamu, demokrasia, na uhuru wa kujieleza.
 
I am for whatever it takes.

Nadhani zipo ambazo zinahifadhi data kwingineko kiasi kwamba hata bodycam ikiharibika, bado data zako zitakuwepo mahala.

Mimi nina dashcam inayorekodi ndani na nje. Hata kama siendeshi gari, camera ina uwezo wa ku detect impact na kuanza kurekodi.

Na inahifadhi kila kitu kwenye app/ account.

Na hata kama bodycams hamna zinazopeleka data kwingineko, ni bora kuwa nayo kuliko kutokuwa nayo.

I am for anything that can help.

Sitaki watu wawe helpless kabisa.

Mfano huyo Mdude hata hatujui hao watu waliompiga wanafananaje.
Hakika! …Sijui watawala wanaipeleka wapi hii nchi. Bila mass (popular) uprising, I am afraid, hii nchi haitarudi kwenye mstari!
 
Interesting… Nilikuwa sijui kwamba wanaoteka na kutesa/kuua watu wanafuata sheria!
Hao polisi na wanajeshi ana uhakika gani kuwa ndio watekaji? Msukuma mmoja akiwa mwizi wa ng'ombe ina maana wasukuma wote ni wezi wa ng'ombe?
 
Hao polisi na wanajeshi ana uhakika gani kuwa ndio watekaji? Msukuma mmoja akiwa mwizi wa ng'ombe ina maana wasukuma wote ni wezi wa ng'ombe?
Unazidi kunitoa usingizini. Nilikuwa sijui kwamba April 24, 2025 pale Kisutu vilikuwepo vyombo vya dola sanjari na wale watekaji ambao wamekuwa wakitafutwa na polisi kwa muda mrefu bila mafanikio. Siku ile tena watekaji walifanya yao mbele ya polisi na kuwapeleka mateka wao kwenye pori la Mabwepande! Isn’t this interesting?
 
Hao polisi na wanajeshi ana uhakika gani kuwa ndio watekaji? Msukuma mmoja akiwa mwizi wa ng'ombe ina maana wasukuma wote ni wezi wa ng'ombe?
suala limetoka katika level ya utashi wa watu na kuonekana ni wa kitaasisi, hata kama sio wa kitaasisi, Polisi au Mtumishi yeyote akifanya mambo ambayo ni kinyume na kiapo chake anatia doa taasisi nzima hata kwa wale walio wasafi. Samaki mmoja akioza ni wote
 
Utani utani tu Kuna siku hii nchi itakuwa si sehemu salama kwetu wote.Mama kakausha,ni kama vile mzanzibar aliyetumwa kuiharibu Tanzania bara.
Acheni uhuni,unajua mama amekuwa mpole sana ila kuna watu wachache wanataka kumkwamisha.
Sasa ujue mtu mwema anaweza kuwa na watu wanampambania na yeye hawajui kabisa.
 
Acheni uhuni,unajua mama amekuwa mpole sana ila kuna watu wachache wanataka kumkwamisha.
Sasa ujue mtu mwema anaweza kuwa na watu wanampambania na yeye hawajui kabisa.
Angekemea hivi vitendo kujiepusha na hizo lawama, Polisi wanatumia nguvu kupita kiasi kwa watu ambao hawana silaha yeyote, anaepukaje hizo lawama?
 
Acheni uhuni,unajua mama amekuwa mpole sana ila kuna watu wachache wanataka kumkwamisha.
Sasa ujue mtu mwema anaweza kuwa na watu wanampambania na yeye hawajui kabisa.
Kuna Mwaka kipindi cha Nyerere yalitokea mambo kama haya Waziri mwenye dhamana aliwajibika kuonyesha kuwa lilikuwa jukumu lake kusimamia vyombo vitimize majukumu yao kwa mujibu wa sheria, Yaani mtu anayesimamia sheria anayetakiwa awafundishe wengine utekelezaji wa sheria yeye ndo anazivunja.
 
Back
Top Bottom