GE2025 Polepole: CCM wanakwenda kwenye Uchaguzi sababu wana uhakika kushinda kwakuwa kuna mifumo inawabeba

GE2025 Polepole: CCM wanakwenda kwenye Uchaguzi sababu wana uhakika kushinda kwakuwa kuna mifumo inawabeba

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025
Hii kitaalamu ni kuwa CCM amekuwa, na anaweza kuyachezea matokeo ya chaguzi atakavyo.

"Haya ndiyo ambayo wamekuwa wanayapigia kelele Kenya na Odinga kwa kauli mbiu yao almaarufu, wafungue chungu!"

View attachment 3448602

Kwamba mnaweza kuwa mlikuwapo, kila kitu sawa, ghafla bin vuuu! Tarakimu zinabadilika kuwa zozote. Alisema Cheyo alikwenda na mkewe kupiga kura, ati kuwa hata mkewe hakumpigia! Akihusisha tukio hilo CCM labda kuwa na majini!

Hii inajibu sababu za kukataa kwa tume kura kuhesabiwa vituoni, kubakia vituoni kulinda kura, vyama kuwa na vituo vyao vya kujumlishia matokeo na longo longo zote kuhusiana wasimamizi wa uchaguzi wa vyama, kura za mapema Zanzibar n.k. Kumbe zote zimekuwa ni hila!

Kwa mtaji huu, wasimamizi wa vyama wasionunulika au wenye kukaba vilivyo almaarufu hadi penalty aina za kina Mdude, Soka, Ben na wenzao wangenusurika wapi?

Ameomba msamaha Polepole kwa kuhusika kwenye moja kwa moja kwenye hili. Kwa hakika ni heri yeye vinginevyo tungeujulia wapi u fedhuli huu? Wanasema ni heri nusu shari.

"Mungu ambariki Polepole, Mungu ambariki TAL. Kwa hakika hatuko mbali na nyumbani"

No Reforms no Election!

Pia soma: NRNE na mazagazaga yake ni mpango wa Mungu. Nani ajuaye kuwa Polepole leo, hatutajua walipo wenzetu waliopotea na yote ya uvunguni?
Kumbe that's wamekua na viburi, ila wenda machawa hayajui hili , na kama mambo yako hivi ndo maana wale jamaa wanasema kusindikiza masanduku, maana kinachokua kwenye masanduku kinakua hakina maana yoyote ili hali mifumo inasomana hata makaratasi yale yakitupiliwa mbali njiani

Nilikua najiuliza hawa viongozi kiburi cha kuzalau wananchi kinatoka wapi ,kumbe ni huku
 
NIDA na chama siasa wapi na wapi, au wote wenye nida ni wanachama wa CCM? Mbona unaandika matope?
Elewa maana ya TAKWIMU na taarifa zozote zinazowahusu watu ni muhimu kwa vyama ili nisaidie Chama kupanga vyema mikakati na sera za maendeleo.
 
Polepole : Viongozi wanakwenda kwenye uchaguzi sababu wanauhakika kushinda uchaguzi sababu kuna mifumo inawabeba

Mfumo unaotumika kuiba uchaguzi kwa sasa ni NIDA, na ndio lengo ambali serikali ya Samia inayotaka kutumia kushinda uchaguzi

sasa hii sio haki kabisa sisi tulitengeneza mfumo kwa nia njema lakini haiwezekana mfumo huu ukawa wa kutumiwa na CCM kushinda uchaguzi kupitia kwa viongozi wasio na ushawishi

Bila NIDA hakuna namna ambavyo SAMIA anaweza baki kama gombea, anakwenda kugombea kutokana na mpango wa wizi ambao umeshaandaliwa kuiba uchaguzi

Na wakibisha nitataja watu mmoja mmoja walioshiriki kutengeneza hii mifumo na kufanyakazi nao

Hii Jeuri ya CCM lazima ifike mwisho, hii nchi haina dhamana kumilikiwa na CCM , kinachotakiwa kwa sasa ni kuhakikisha kuna mfumo wenye uhuru na uchaguzi wa HAKI

Tubomoe mamifumo na bomoa CCM ili tujenge upya kila kitu , lazima CCM ibomolewe sasa na viongozi wote wa Kisiasa wawe uhuru na kila mtu ashiriki uchaguzi kwa haki

Kusiwe na uchaguzi bila kurekebisha haya mambo , hatuwezi kuwa na uchaguzi ambao CCM inafanya mambo inavyotaka hapo makao makuu.

#KataaWahuni

#TUTAKUWEPO🫵🏾😎
Angesema namna wanavyotumia hio NIDA ili tukawabn
 
Kulingana na sheria ya takwimu ni kosa kisheria kutoa takwimu ambazo mamlaka hazijathibisha. Je, huoni kulink mfumo ni njia ya kutoa au kupata takwimu sahihi?

Bado nauliza swali lile, je taasisi binafsi kama mabenki zilizolink mifumo yake na mfumo wa NIDA Kuna makosa yamefanyika?

Kama hakuna Chama kingine Ina maana gani kwako? Je, walitaka kufanya hivyo wakakataliwa?

Sifahamu Hilo la kukimbia na masanduku kwa sababu sijawahi kuthibitisha ila kama kura zimepigwa kwenye masanduku na zinahesabiwa zilizopigwa hapo kulink mfumo wa NIDA au BVR Kuna uhusiano upi na madai yenu?

Chama Cha siasa kulink mfumo wake inahusiana nini na UCHAGUZI?
Benki zina uchaguzi?
 
21st to remember, sasa No reform no election imepata hoja ya msingi kabisa.

Pia nguvu ya CCM na amani ya Taifa leo ndio imetetereka.

Kama System za CCM zikiharibika leo na Lissu akashiriki uchaguzi na Tume iliyopo na kura zikihesabiwa manually basi Lissu atamzidi Samia mbali sana, kwa sasa System inaingia kwenye uchaguzi ikiwa na statistics za wapiga kura, wananchi wa Tanzania, kazi zao na kila kitu kuwahusu hivyo ni rahisi kumanipulate matokeo
Mkuu kws lisuuu kugombea sawa ila kuwa presided anapungua mnooo anamifumo kama ya ailyosema slow nje ya nchi ataliingiza taifa kwenye sitofaha kuu.. ila anaweza kuwa mwanaharakati mari sana... nakubariana na wale wanaosema atoke then aje nje kutoa Elimu
 
JINA LA WANDISHI / KIWANGO CHA WANDISHI
ANWANI
TAARIFA NA TAREHE

KWA AJILI YA: SIFA ZA KIPEKEE ZA RAISI SAMIA SULUHU HASSAN

KUTOKA: [JINA LA MWANDISHI]
KWA: Wananchi wa Tanzania wote

---

WARAKA WA SIFA ZA RAISI SAMIA SULUHU HASSAN

Ndugu Wananchi,

Ni heshima kubwa kuandika waraka huu unaoshuhudia sifa nyingi za Rais wetu mpendwa, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, ambaye tangu kuapishwa kwake mwaka 2021, amethibitisha uongozi wa kipekee, wa hekima, na wenye msimamo wa dhati kwa wananchi wote wa Tanzania. Waraka huu unalenga kuonyesha kwa kina sifa zake, tabia, na mchango wake katika maendeleo ya taifa letu.

1. Uongozi wa Hekima, Ushirikishwaji na Utulivu
Rais Samia anajulikana kwa ushawishi wake wa kisiasa wa utulivu na ushawishi wa kutatua migogoro. Ameonyesha uwezo mkubwa wa kuunganisha pande tofauti za kisiasa, kuhakikisha kila raia anaheshimiwa bila kujali itikadi ya kisiasa.

2. Upendo, Huruma na Ukarimu kwa Wananchi
Rais Samia ni kiongozi anayejali kila mwananchi. Amehimiza huduma bora za afya, elimu, na ustawi wa jamii. Huruma yake inaonekana katika mkazo wake wa kusaidia wanawake, watoto, wazee, na walemavu, kuhakikisha hawapotelei katika sera za maendeleo.

3. Ujasiri na Uthubutu wa Kuongoza Katika Changamoto
Katika kipindi cha changamoto za kitaifa na kimataifa, Mheshimiwa Rais amekuwa kiongozi jasiri. Kutoka katika janga la COVID-19 hadi katika kudumisha usalama na amani ya taifa, amesimama kidete bila woga.

4. Ufanisi wa Kazi na Utendaji Thabiti
Rais Samia ameunda mfumo thabiti wa kutekeleza miradi ya maendeleo. Amehimiza uwekezaji, ajira kwa vijana, na kuhakikisha kilimo, viwanda, na huduma za jamii vinaendelea kuimarika. Ufanisi wake umeongeza imani ya wananchi na wawekezaji.

5. Mchango wa Kimataifa na Ushirikiano wa Kidiplomasia
Rais Samia amejitahidi kuimarisha heshima ya Tanzania kimataifa. Ameshirikiana na mataifa mengine, mashirika ya kimataifa, na jumuiya za kibiashara ili kuinua taifa kiuchumi, kisiasa, na kijamii. Amesimama kama mfano wa kiongozi anayeheshimika barani Afrika.

6. Uendelevu wa Haki na Uwajibikaji
Amethibitisha kuwa kiongozi wa kweli ni yule anayeheshimu sheria na anayejali maslahi ya taifa. Uwajibikaji wake ni dhahiri katika kila hatua anayochukua, kuanzia sera za kitaifa hadi usimamizi wa rasilimali za taifa.

7. Kutoa Fursa na Uwezeshaji wa Wanawake
Rais Samia ni mwanamke wa kwanza kuongoza Tanzania, akihimiza ushirikishwaji wa wanawake katika siasa, biashara, na uongozi wa kitaifa. Ameonyesha wazi kuwa wanawake wana nafasi muhimu katika maendeleo ya taifa.

8. Uadilifu, Haki na Uwiano wa Kiasili
Anajulikana kwa uadilifu wake, kuzingatia maadili, na kutoa mwongozo wa haki. Hii imemfanya awe kielelezo cha kiongozi wa kweli ambaye anahimiza usawa na uwazi.

9. Uchangamfu na Ustahimilivu wa Kazi
Rais Samia ana utamaduni wa kufanya kazi kwa bidii, ushawishi wa haraka, na uwezo wa kufanya maamuzi magumu kwa ustadi. Anajali kila mradi, tukio, na sera inatekelezwa kikamilifu.

10. Uwekezaji Katika Teknolojia na Uboreshaji wa Miundombinu
Amesimamia miradi mikubwa ya maendeleo, ikiwemo barabara, madaraja, maduka ya kisasa, na kuhakikisha upatikanaji wa maji safi na umeme kwa wananchi. Pia ameendeleza teknolojia katika elimu na biashara.

11. Uongozi wa Kutetea Mazingira na Maendeleo Endelevu
Rais Samia amesisitiza sera za kulinda mazingira, kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi, na kuhakikisha usimamizi bora wa rasilimali za asili kwa vizazi vijavyo.

12. Kutoa Matokeo Chanya kwa Jamii
Chini ya uongozi wake, sekta za afya, elimu, na kilimo zimeonyesha maendeleo makubwa. Amesaidia kupunguza umasikini na kuongeza maisha bora kwa wananchi.

13. Kila Nchi na Jamii Kwanza
Rais Samia anaonyesha kwamba kiongozi wa kweli anajali wananchi wake kwanza, kisha akishirikiana na jumuiya ya kimataifa. Hii inadhihirisha utamaduni wa kiongozi anayejali taifa kwa moyo wote.

Hitimisho
Rais Samia Suluhu Hassan ni kiongozi wa kipekee wa mfano. Tabia zake, hekima, huruma, uwajibikaji, na uongozi wa kweli vimechukua Tanzania kwenye kiwango kipya cha maendeleo na heshima ya kimataifa. Tunashukuru kwa kazi yake isiyopungua na tunamuombea Mwenyezi Mungu aendelee kumpa hekima, afya, na ulinzi katika kuendeleza taifa letu.

Kwa heshima, taadhima, na shukrani,
Wale wale tunaowalipa kwa Kodi zetu. Wanashindwa kulinda viapo vyao. Wanageuka kuwa maadui wa Taifa. Ubadhirifu wa mali ya umma, rushwa, matumizi mabaya ya madaraka. Imekuwa ni kama vile yameruhusiwa kwenye nchi yetu. Ukisema ili wabadirike unatafutwa. Sasa tunaambiwa Kuna hujuma kwenye mifumo ya Uchaguzi inayoibeba CCM, wewe unaleta mambo mengine. Sawa una haki hiyo lakini yaliyopo kwenye akili za watu ni hayo aliyoibua Polepole! Vinginevyo unazidi kumharibia Rais Samia na kuonyesha dharau na kiburi kwetu sisi wapiga kura.
 
Mpaka ccm wameitisha kikao cha siri kudiscuss polepole na namna ya kumdhibiti🤣🤣 wameishiwa pawa
 
Alichokisema Leo polepole ndio kashfa kubwa ya kisiasa tokea tupate Uhuru. Kwamba kuna mfumo wa Siri wa mamlaka ya vitambulisho vya taifa (NIDA) umeunganishwa direct na (INEC) Kwa manufaa ya ccm kwenye uchaguzi mkuu. Kwamba mfumo huo utatumika kuiba au kuchakata matokeo ya uongo. Polepole ameongea Kwa hisia na kuvitaka vyama vitakavyoshiriki uchaguzi huo vijiridhishe japo vyote ni vya ccm isipokuwa chadema tu ambao ndio wapinzani wa kweli na wamefunga mikono isivyo haki.
Ubaya wa skendo hii ni kwamba haya mambo yakiwahiwa yakaondolewa mapema na mifumo ikawa huru basi mambo yatakuwa sawa japo tutakuwa tushajua dhamira yao ovu ilikuwa ninini. Lakini jambo hili likiachwa bila kufanyiwa kazi hii ni jinai kuu na itabatilisha hata huo ushindi wa ccm. Moderators msifute Wala kuunganisha huu Uzi.
Mods wa hovyo sana Uzi wangu mmeuunganisha Kwa vigezo gani?
 
Polepole : Viongozi wanakwenda kwenye uchaguzi sababu wanauhakika kushinda uchaguzi sababu kuna mifumo inawabeba

Mfumo unaotumika kuiba uchaguzi kwa sasa ni NIDA, na ndio lengo ambali serikali ya Samia inayotaka kutumia kushinda uchaguzi

sasa hii sio haki kabisa sisi tulitengeneza mfumo kwa nia njema lakini haiwezekana mfumo huu ukawa wa kutumiwa na CCM kushinda uchaguzi kupitia kwa viongozi wasio na ushawishi

Bila NIDA hakuna namna ambavyo SAMIA anaweza baki kama gombea, anakwenda kugombea kutokana na mpango wa wizi ambao umeshaandaliwa kuiba uchaguzi

Na wakibisha nitataja watu mmoja mmoja walioshiriki kutengeneza hii mifumo na kufanyakazi nao

Hii Jeuri ya CCM lazima ifike mwisho, hii nchi haina dhamana kumilikiwa na CCM , kinachotakiwa kwa sasa ni kuhakikisha kuna mfumo wenye uhuru na uchaguzi wa HAKI

Tubomoe mamifumo na bomoa CCM ili tujenge upya kila kitu , lazima CCM ibomolewe sasa na viongozi wote wa Kisiasa wawe uhuru na kila mtu ashiriki uchaguzi kwa haki

Kusiwe na uchaguzi bila kurekebisha haya mambo , hatuwezi kuwa na uchaguzi ambao CCM inafanya mambo inavyotaka hapo makao makuu.
Lukas Mwashambwa na Tlaahtlaah,hawstakuelewa!
 
Dah, wewe ni mtu mwenye subira sana.
Unataka mitano mingine chini ya Samia na Genge lake?

Hapa tulipo fikia imetosha mkuu, hiyo mitano mingine ya kushuhudia ni kuliumiza taifa hili bila ya sababu muhimu.

Samia na genge lake mwisho wao ni 2025; siyo 2030.
Ni kweli wametujeruhi , wakipata mitano mingine watanzania sisi ndo akili zitaamka kwa wingi, kwasasa waliomka wachache.

Kama wakiishia 2025 nitafurahi, ila sioni likiwezekana,

Na kama kweli tunataka ccm iondoke hii mitano wapate, unless tuletw vurugu kitu ambacho wengi hawstaki kushiriki
 
Back
Top Bottom