Uchaguzi 2020 Polepole: Kuna mgombea mmoja amekimbia yupo nje ya nchi, ameona maji yamemfika shingoni. CCM tunafanya kampeni za kisayansi

Yani huyu ng'ombe kubeba watu kwenye matrekta na malori na mabasi ndo kisayansi....?
Kusomba watoto wa primary na kukatisha masomo yao ndio sayamsi?
 
Hata wakiondoka wote mradi Mgombea wangu yupo mimi safiiii
 
Kampeni za CCM 2020 tunazifanya kisayansi, tumegawanya viongozi waandamizi wa chama kwenye maeneo tofauti. Msafara mkuu unaongozwa na Dkt. Magufuli, msafara mwingine wa Mhe. Samia Suluhu, na mwingine unaongozwa na Kassim Majaliwa, sisi hatutumii chopa." - Humphrey Polepole.

Mzee Jakaya Kikwete yupo Ukanda wa Kusini kule anavuruga, Mzee Pinda na Spika Job Ndugai nao wanaendelea. Muziki ni mzito mpaka sasa tunapozungumza kuna mgombea mmoja amekimbia yupo nje ya nchi, ameona maji yamemfika shingoni, tunafanya kampenzi za kisayansi." -Humphrey Polepole

Tangu Mhe. Magufuli aingie madarakani hakujawa na mfumuko wa bei, tumefanya kazi nzuri mno, bidhaa haiongezeki, Mhe. Magufuli amefuta kodi kwa wenye mishara midogo, hawa wanaosema ni wapotoshaji, tumelazimika kuwajibu, tunawaambia wasifanye siasa na hivyo." - Humphrey Polepole.

"Ukisema kushuka kwa Diplomasia ni uongo, Mhe Magufuli ameingia tu madarakani akapewa Uenyekiti wa EAC, ameendeleza mwendo wa kubana matumizi, miradi mikubwa imefanyika, ameacha alama, SADC amefanya mambo makubwa, MSD inapeleka dawa nchi zote za SADC." - Humphrey Polepole.

Tumefuatilia na kujiridhisha kwamba ni uongo mtupu, na TCAA imeshatoa ufafanuzi, lakini unajiuliza nini dhamira ya kusema uongo, kwamba mmezuiliwa kwenda kufanya kampeni maana yake unataka kupandikiza chuki, na hata hakukuwa na mpango wa safari"

An empty container is noisy!
 
Wapinzani wana nongwa kama nywele zinaota tuuu - Humphrey Polepole

Tundu anasema majudge hawajui kiingereza - Humphrey Polepole

Tundu ana kauli ya UHURU na HAKI lakini wamewanyima waandishi wa habari uhuru na haki - Humphrey Polepole

Wapinzani wanapinga matumizi ya ndege lakini wao wanatumia chopa - Humphrey Polepole

Wapinzani wanataka kufanya mambo kinyume cha maadili ya mtanzania na kinyume cha imani za dini - Humphrey Polepole

Wapinzani wetu hawapo serious.....kauli mbiu ya kugawa ubwabwa - Humphrey Polepole

Kura zikipigwa Leo Magufuli anashinda kwa 85% - Humphrey Polepole

CCM imejenga na kuboresha vituo, vya afya, hospitali za wilaya na mikoa, hospitali za rufaa, imeajiri madaktari zaidi ya 1000, imenununua vifaa tiba na sasa inaelekea kuboresha bima - Humphrey Polepole
 
Sukari ?

Unajua kama mtu anaweza kudanganya moja kwanini asidanganye mawili au matatu au yote?, tangu huyu jamaa aache kuongelea issue na kuamia kwenye mipasho na taarabu wala huwa simpi time ya kumsikiliza
Anayezungukwa na wasanii naye huwa msanii.
 
Hamphrey Pole Pole mwenezi wa CCM acha uongo mchana kweupe hivi unamdanganya nani ya kwamba tangu 2015 mfumuko wa bei haujapanda kweli?Hivi sukari bei ya 2015 na leo ni sawa hebu acha porojo aisee
Unasema wenye mishahara midogo wamefutiwa kodi mbona unakuwa muongo hivyo aisee please acha kudanganya watu.Mtu analipwa shilingi laki mbili 200,000 anakatwa kodi hivi wewe umetumia takwimu za mwaka gani niulize.Watanzania sio wapumbavu kiasi hichi,kwanza waambieni wanannchi zile milion hamsini kila kijiji zi wapi,Laptop kila mwalimu ziko wapi?Mlikuja na huduma za Afya kwa wazee na watoto bure mmezikata sasa hivi Mzee na Mtoto lazima walipie,Bima kwa ujumla mmeikorokochoa huna aibu wakaa mbel ya vyombo vya habari kusema uongo.

Nakumbuka enzi zile ukiwa na akili zako timamu alidai serikali tatu leo hii umevurugwa hata umejisahau aisee muogope Mungu
 
Wapinzani wana nongwa kama nywele zinaota tuuu - Humphrey Polepole

Tundu anasema majudge hawajui kiingereza - Humphrey Polepole

Tundu ana kauli ya UHURU na HAKI lakini wamewanyima waandishi wa habari uhuru na haki - Humphrey Polepole

Wapinzani wanapinga matumizi ya ndege lakini wao wanatumia chopa - Humphrey Polepole

Wapinzani wanataka kufanya mambo kinyume cha maadili ya mtanzania na kinyume cha imani za dini - Humphrey Polepole

Wapinzani wetu hawapo serious.....kauli mbiu ya kugawa ubwabwa - Humphrey Polepole

Kura zikipigwa Leo Magufuli anashinda kwa 85% - Humphrey Polepole

CCM imejenga na kuboresha vituo, vya afya, hospitali za wilaya na mikoa, hospitali za rufaa, imeajiri madaktari zaidi ya 1000, imenununua vifaa tiba na sasa inaelekea kuboresha bima - Humphrey Polepole
Old wine in an old bottle.
 
Sukari ?

Unajua kama mtu anaweza kudanganya moja kwanini asidanganye mawili au matatu au yote?, tangu huyu jamaa aache kuongelea issue na kuamia kwenye mipasho na taarabu wala huwa simpi time ya kumsikiliza
Unategemea Mc Polepole aongee nini cha maana?
 
Kuengua wagombea ndo sayansi? Yani ni sawa na kuulizwa tafuta thamani ya x kwenye mlinganyo afu ww unaifuta hyo x kwenye huo mlinganyo ili usiione au isionekane! Upuuzi kabisa huu! Eti ni chama kinachoongzwa na mtu mwenye Phd.. ivi kwann mnadhalilisha taaluma kiasi hiki?
 
Sasa hili litampatia vipi kura? Mpaka wewe ushupae kuwa analeta challenge kwa JPM? Hujui kuwa wananchi wengi wanataka aongezewe muda ili akamilishe haya mazuri anayokufanyia wewe na watanzania kwa ujumla? Yeye ameshasema hataongeza na atafuata katiba ya JMT. Sasa huyu analeta uongo gani majukwaani.

Wananchi gani, hao wanaoshurutushwa kumkubali? Kama ameshasema, huko bungeni chini ya spika wanaposema watamuongezea, ina maana wao hawamsikii anachosema?
 
Back
Top Bottom