Polisi Tanzania: Hatutegemei kuona sherehe za Pasaka wakati Nchi bado ipo kwenye maombolezo

Polisi Tanzania: Hatutegemei kuona sherehe za Pasaka wakati Nchi bado ipo kwenye maombolezo

Amani ya bwana iwe nanyi!
Leo jeshi la polisi nchini kupitia kwa msemaji wake limewataka wananchi kusheherekea sikukuu ya pasaka bila shamrashamra kwa kile walichodai kuwa taifa lipo kwenye maombolezo ya kifo cha aliyekuwa Rais wa awamu wa tano marehemu John Pombe Magufuli.

Hii si sawa maana pasaka ni sherehe ambayo wakristu wanafurahia kufufuka kwa mwokozi wao Yesu kristo na shamrashamra ni sehemu ya ibada. Kitendo cha kuzuia shamrashamra hakikubariki hata kidogo. Taifa hili kuna watu wataliangamiza kwa ujinga wao.
 
Wakristo ijumaa kuu tunaadhimisha kifo cha Bwana Yesu, na alfajiri ya jumapili tunasherekea kufufuka kwake, sasa inakuwaje tunalazimishwa kutii sheria za wanadamu halafu tuzidharau za MUNGU?. ..
Bwana Yesu aliyeyashinda mauti,ameanza sherehekewa toka miaka elfu mbili iliyopita,sijawahi acha msherehekea anapofufuka na hata pasaka hii nitamsherehekea,alishuka kuzimu akayshinda mauti na siku ya tatu akapaa mbinguni,kwanini nisishangilie siku hiyo? thubutuuu 😂
 
Huu ujumbe wa Polisi kuwa tusifanye Shamrashara ya Pasaka sijaulelewa!

Ni kwamba tutulie kimya tusikumbuke Ukombozi tuliopatiwa na Mwokozi wetu!

Mfano Mimi na wanangu siku hiyo huserebuka na nyimbo Kama ..Hakuna Mungu Kama Wewe,Hakuna mwanume Kama Yesu, Tumeokolewa kwa Neema,Siku ya Mapambazuko!

Na ukumbuke hapo huwa tunafunga mtaa ,tukila na kunywa na majirani sambamba na kukhubiri Kristo!

Swali langu ni hii imezuiwa!

Na kiukweli mwaka huu nilipanga kufanya makubwa zaidi!
 
Inabidi tuwe na utu,hili jambo si la kila pasaka.Tuomboleze,Tuache mihemko
 
Duuuuu sasa mmeanza kuingilia na imani za watu kweli?
 
Waombe labda mikia washinde lakn yakifungwa na AS VITA takunywa mpaka asubuh
 
Jeshi la polisi nchini limewataka waumini wa dini ya Kikristo na Watanzania wote kusherehekea sikukuu ya Pasaka huku wakikumbuka bado Taifa liko katika siku 21 za maombolezo kufuatia kifo cha aliyekuwa Rais wa Tanzania Dkt. John Magufuli....
Tanzaia Kuna Mila na destuli nyingi kulingana na makabila na maeneo. Pia kuna tamaduni tofauti za kuomboleza msiba. Wengine unywa pombe na kucheza ngoma kujifariji.

Wengine uzika na kumaliza msiba baada ya siku tatu, arobaini, na hata zaidi ya hapo. Ni busara tu itumike kuliendea hili, vile kukaa na majonzi muda mwingi yaweza pelekea maradhi ya Sonona. Ni fikra zangu tu.

Apumzike kwa amani mpendwa wetu.
 
Yaani hawa wafuasi wa Ibilisi wanawawapangia wakristo namna ya kusherekea ? Na waisoam mtawafanyia hivyohivyo kwenye sikukuu ya Idd ? Polisi mnatia aibu Sana mtakatifu Jiwe tayari kazikwa huko na shuka jekundu .
Screenshot_20210401-170458.png
 
Jeshi la Polisi nchini limesema halitegemei kuona sherehe na shamrashamra za Pasaka kama za kipindi cha nyuma katika kipindi hiki ambacho nchi bado ipo kwenye maombolezo ya kuondokewa na Hayati Dkt. John Pombe Magufuli.

====

Ndugu wanahabari, kama mnavyojua bado taifa letu lipo katika siku 21 za maombolezo kutokana na kifo cha alikuwa Rais wwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Hayati Dkt. John Pombe Joseph Magufuli.

Kutokana na tukio hilo kubwa la majonzi napenda kuwajulisha kwamba nchi yetu bado ipo shwari pamoja na kwamba kuna matukio machache ya kijinai yaliyotokea na ajali za barabarani zilizotokea ambazo kwa pamoja zinaendelea kushughulikiwa na baadhi ya watuhimiwa waliohusika katika matukio hayo wameshakamatwa.

Ndugu wanahabari, kufuatana na kalenda, kila ifikapo wakati huu waumini wa madhehebu ya Kikristo huungana kwa pamoja katika kusherehekea sikukuu za Pasaka...

Tuna imani, kama kila mwananchi atazingatia na kufuata Sheria na kujiepusha na vitendo vya kiuhalifu, ibada za Pasaka zitamalizika salama tukizingatia kuwa bado tupo katika kipindi cha maombolezo na hatutegemei zile sherehe na shamrashamra tulizozoea kipindi cha miaka ya nyuma kuwepo katika kipindi hiki.
dah hii ndo Tanzania usikute mkuu wa nchi mama samia hajui hili bango la kuzuia shamra shamra
 
Back
Top Bottom