Kijana wa Kizimkazi 2030
JF-Expert Member
- Apr 25, 2026
- 4,842
- 10,164
Chonde chonde msiwachome sindano za ganzi mapolisi wetu maana hao ndo wanaotulinda
Haiwezekani utumie service road kwa makosa,halafu ugeuke mtemi mangungo,na bondia!Kasome na wewe uwe daktari....eti wapo polites...what is this?..
Wewe jamaa lofa sana...alafu mbona chawa wengi ni vilaza ?
Somesheni watoto aisee...
Yupi aliyeanza kujichukulia sheria dhidi ya mwingine?Unasema kumtandika ni sahihi,halafu unasema huwezi kujichukulia sheria kijinga jinga, kipi ni kipi hapo?
Litafautiliwa!Kuna dada anaongoza genge la uhalifu na ukwepaji Kodi, ana kesi 7 za jinai, 4 za civil na zingine za Regulatory Authorities, yeye anasema hapa hakuna jinai ni madai tu nenda Mahakamani. Yule inaonekana ana hongwa na kula rushwa.
Hii mambo ya kupeana adhabu kinyume cha sheria huwezi elewa kwanini ni muhimu kuadhibiwa kwa mujibu wa sheria mpaka likukute jambo.Vitu vingine ni vya kujiepusha navyo tu, hivi kweli umkwide police akiwa kwenye sare za kazi utegemee kusalimika?
Aisee...Alafu wamekuja kutangaza kapigwa na wananchi🥹🥹ila mapolisi
Police headquarters Dodoma ofisi ya IGP walinipigia simu. Nilikuta missed call, baada ya mimi kuandika barua pepe kwenda PCCB na Ubalozi wa Uholanzi hapa nchini Tanzania.Litafautiliwa!
Hao wananchi waliompiga wamekamatwa? Maana ni kosa kisheria kujichukulia sheria mkononi.Alafu wamekuja kutangaza kapigwa na wananchi🥹🥹ila mapolisi
Yaani hii inafanya taarifa zinazotolewa na Polis zisiaminike kabisa. Hapa kuna mashuhuda vipi zile habari ambzo hakuna mashuhuda! Kweli hatuna jeshi la Polis. Ni kama genge flani hivi linalomiliki silaha za moto.Alafu wamekuja kutangaza kapigwa na wananchi🥹🥹ila mapolisi
Kila mtu ana kiwango chake cha ustahimilivu , Nimefanya kazi na huyo jamaa kwanza ni very humble na mpole sana pamoja na kukupita Kila kitu hadi dhambi anatenga muda na kukusikiliza pia anarekebishika ,Kuna nyuma ya pazia wanalofahamu wahusika wao tu wawili likaleta haya yote.Vitu vingine ni vya kujiepusha navyo tu, hivi kweli umkwide police akiwa kwenye sare za kazi utegemee kusalimika?
Ndani ya kila taasisi (Police au Ualimu) kuna watu wema na wale wa hovyo.Hakuna mwananchi wa kumsaidia polisi hasa nyakati hizi.
Ila wanajeshi si wana hospitali zao ? Hakuna kilichoharibika 😁Hao wanajeshi ndio wapumbavu...
Vitq ni vita mura. Wananchi Vs CCM na sasa ni Madaktari Vs Polis. Ushindi wa Madaktari utapelekea ushindi wa wananchi dhidi ya CCM mana CCM mbeleko yao itakuwa imekatika.Sasa ni zamu ya watumishi wa Wizara ya Mambo ya ndani kuandikiwa dawa za uongo pamoja na familia zao
Hivi ni kweli kuwa kila kosa la barabarani adhabu yake ni kuandikiwa faini tu? Shida Dr. alileta ujuaji na kiburi kwenye fani za watu wengine. Si angesikiliza elimu maisha yakaendelea?kwa yule jamaa mpaka kufika ile hatua ,si kawaida maana si mtu washari,polisi alichomoa ufunguo wa gari,baada ya jamaa kumwambia kama lipo kosa niandikie faini nikalipe,polisi akagoma,
Hii ni chicken syndrome.Hivi ni kweli kuwa kila kosa la barabarani adhabu yake ni kuandikiwa faini tu? Shida Dr. alileta ujuaji na kiburi kwenye fani za watu wengine. Si angesikiliza elimu maisha yakaendelea?
Kumtetea ni ngumu sana. Iko siku tutasikia daktari kapigwa na ndugu wa mgonjwa akiwa kwenye chumba cha matibabu na tulivyo na Nchi ya hovyo tutawasifu ndugu wa mgonjwa.
Kumpiga mtu anayetekeleza jukumu lake kisheria ni suicide hakuna cha kusingizia eti ni mpole nk nk. Imagine je kama alihatarisha usalama wa watoto may be kwenye zebra? je kama alibamiza boda? Je kama gari haina bima? Watu hawataki kujua kisa kapigwa polisi, kesho utapigwa wewe na watu wenye kiburi na dharau ukiwa unatimiza majukumu yako. Dr aache ujuaji na kiburi; period
Hoja ya kupigwa na wananchi au kutokupigwa ni hoja nyingine kabisa.Hii ni chicken syndrome.
Hoja si kosa la daktari, hoja ni adhabu. Je ni kweli amepigwa na wananchi? Kama si wananchi, kupigwa ni adhabu za kisheria? Achana na chicken syndrome.
Ndio mumpige mtungo?kisasi ni haki
Mada inasema polisi wamempiga daktari mpaka kulazwa, inamaana hoja ni daktari kupigwa. Angepelekwa mahakamani tusingejadili suala la kupigwa.Hoja ya kupigwa na wananchi au kutokupigwa ni hoja nyingine kabisa.
Kujadili chimbuko sehemu inayotakiwa kujadili adhabu ndo chicken syndrome yenyewe mkuu. Yaani Ile jinai inayotendeka inatumika kama kichaka cha kuficha jinai ya mtoa adhabu.Mie nimeongelea chimbuko la tatizo. Kila tatizo liongelewe kivyake. Nililoliona mimi ni hilo la daktari akiwa kamkalia polisi aliye kwenye mazingira ya kazi yake. Si ustaarabu na hakuna usomi utakaojustfy hiyo... the aftermath ni issue nyingine that's why hapa imekuja kama tetesi..
Another Chicken syndrome. Kwamba mvunja sheria hata angeuwawa kwa silaha ya askari suala lingekuwa kuvunja kwake sheria si kuuwawa.Imagine polisi angekuwa na silaha? Polisi wenzie si wangemuua jamaa kwa kudhani anataka kuchuku silaha aitumie?? Daktri kazingua na kaonesha kiburi na dharau
Lakini kwa hali ilivyo sasa raia wengi bado wanaamini polisi ni adui zao namba moja.Ndani ya kila taasisi (Police au Ualimu) kuna watu wema na wale wa hovyo.