Polisi waonya mikusanyiko ya kumpokea Lissu, na maandamano ya wanafunzi

Polisi waonya mikusanyiko ya kumpokea Lissu, na maandamano ya wanafunzi

Nimewaambia mnataka kuwapa akina ACP&SACP umaarufu tu kama ilivyokuwa kwa Gilles Mroto.

Hao aliowaomba wamhakikishie ulinzi akirudi watamwambia usalama wake uko hatarini kwenye hayo mapokezi na story inaishia hapo.

Hizo T shirts zenu jiandaeni kuzifanya pajamas ama mzilegeze shingoni ziwe za kunyonyeshea.
😁😁!

Bado sana!!
Binadamu akionewa sana siku zote hutafuta njia yake. Kuna kitu CCM mnakitengeneza endeleeni kukitengeneza na soon mtakipata. Unafikiri Omar Al Bashir alifikaje mwisho???
 
Jeshi la polisi limesema limeona baadhi ya viongozi wa CHADEMA wakihamasisha kukusanyika ili kumpokea mmoja wa kiongozi wanayetarajia kurejea nchini Julai 27, 2020.

Polisi wamesema hawana taarifa rasmi ya mikusanyiko hiyo inayohamasishwa mitandaoni. Wamesema ni haki yao kukusanyika lakini hakuna haki bila wajibu, hivyo wamewataka viongozi hao kufuata sheria.

Aidha jeshi la polisi limesema linafuatilia wanaosambaza ujumbe wa kuhamasisha wanafunzikugoma kwa kutoingia madarasani ili kushinikiza Bodi ya Mikopo kurejea masharti ya mkataba ya fedha ya kujikimu.

Polisi wamesema hawatasita kuwachukulia hatua wanaokiuka sheria, kwa kuitisha mikusanyiko na maandamano yasiyo na Baraka za kisheria, hivyo wamewataka wanafunzi wafuate njia stahiki za kufikisha malalamiko yao na sio kukiuka sheria.



View attachment 1516564
View attachment 1516567

Wangeongezea maneno "kuepusha mikusanyiko kama tahadhari ya Corona wangeleweka vyema"

Maafande fanyieni editting hiyo memo tafadhali.
 
Binadamu akionewa sana siku zote hutafuta njia yake. Kuna kitu CCM mnakitengeneza endeleeni kukitengeneza na soon mtakipata. Unafikiri Omar Al Bashir alifikaje mwisho???
Labda kizazi kijacho siyo hiki cha sasa!
 
Binadamu akionewa sana siku zote hutafuta njia yake. Kuna kitu CCM mnakitengeneza endeleeni kukitengeneza na soon mtakipata. Unafikiri Omar Al Bashir alifikaje mwisho???
Mpuuzi wewe watu tuko kwenye msiba unaleta siasa
 
Ina maana hawakuomba kibali cha maandamano mpaka Leo? Mbona kama hawana weledi?
Sio kwamba hawana weledi,wapo watu wanavuruga kwa makusudi,chunga sana watu wanaojifanya wanapromote maandamano put them on screen you might find their true color.
 
Hiyo tarehe mimi nitakua na kula tunda kimasihara kutoka tanga,mtoto wa kidigo nitakua nae siku 4 hapa mjini sina wasiwasi kabisa.
 
CHADEMA msiwape polisi sababu za kuwatwanga. Fuateni maelekezo yao kuepusha shari. Huu sio muda wa "kutunishiana misuli" na jeuri na kutoa mifano ya mapokezi ya Hussein Mwinyi huko Pemba. Ukishakuwa mtoto wa kambo, the rules of the game change somehow..
 
Ndio maana tunasema huko CDM hakuna weledi tena, yaani fujo za threads kwenye mitandao zimejaa, kumbe hata ruhusa hawajaomba!!
Kuna watu wanataka kuwatanguliza wenzao kichwa kichwa kwa ajili ya kupata Kiki
Wewe usiyekuwa na akili, Hakunaga kibali cha kwenda kumpokea mtu
 
Nimewaambia mnataka kuwapa akina ACP&SACP umaarufu tu kama ilivyokuwa kwa Gilles Mroto.

Hao aliowaomba wamhakikishie ulinzi akirudi watamwambia usalama wake uko hatarini kwenye hayo mapokezi na story inaishia hapo.

Hizo T shirts zenu jiandaeni kuzifanya pajamas ama mzilegeze shingoni ziwe za kunyonyeshea.
😁😁!

Bado sana!!
Poleni sana, yaonekana wiki hii usingizi hauji
 
Ina maana hawakuomba kibali cha maandamano mpaka Leo? Mbona kama hawana weledi?
Maandamano ya nini wao wamesema wanaenda kumpokea lissu kama vile ilivyopokelewa club ya Simba ikitokea Mtwara baada ya kupokea kombe lao la ligi...wasio kuwa na weledi ni hawa waliotoa andiko lisilokuwa na kichwa wala miguu..walivyo vilaza hata anayepokelewa wanajitoa akili eti hawamtaji jina...kisa maelekezo kutoka juu
 
Wasiwasi wake tu kwani masaa 24 yameisha pita? Kisheria notice ya kuomba kubali hutolewa ndani ya masaa 24 na bado hayajaisha sasa wasiwasi wake nn?
 
Halafu wanataka wakusanyike

Pamoja na kwamba hata wangeomba wangenyimwa ila at least wangekua wamefuata sheria
Club ya Simba walivyopokelewa juzi wakitokea Mtwara baada ya kubeba kombe la ligi waliomba kibali..acha kuwa na akili kama za geshi la polithi kama kweli wewe sio lumumba
 
Ndio maana tunasema huko CDM hakuna weledi tena, yaani fujo za threads kwenye mitandao zimejaa, kumbe hata ruhusa hawajaomba!!
Kuna watu wanataka kuwatanguliza wenzao kichwa kichwa kwa ajili ya kupata Kiki
RUHUSA YA NINI..TUMIA AKILI WEWE...TANGU LINI MTU AKAOMBA RUHUSA YA KUMPOKEA MTU...
 
Msitake kupotosha, tunajua fika kuwa hizo ni figisu za siasa chafu kwakuwa ni Lisu, ila ingekuwa kiongozi wa ccm bila hata kibali angepokelewa kwa mbwembwe. Tena ingekuwa ni kiongozi wa ccm kisha akute watu wameenda kumpokea kwa ridhaa yao, angefurahi ile mbaya.

Hilo la kuzuia yeye kupokelewa na wafuasi wake tulilitarajia, kutokana na mshindani wake hataki kuona jambo litakalomuumiza roho. Hiyo tunaita ni kutumia madaraka kupambana na wivu wa kisiasa.
Unakumbuka Jafo alimhamisha mtaalamu kisa hakukuwa na watu wakati anazindua barabara
 
Back
Top Bottom