Polisi waonya mikusanyiko ya kumpokea Lissu, na maandamano ya wanafunzi

Polisi waonya mikusanyiko ya kumpokea Lissu, na maandamano ya wanafunzi

Taarifa ya polisi imerudiarudia mara kadhaa maneno "kwa mjibu wa sheria," na kuongeza "hakuna aliye juu ya sheria."

Natumaini wanaelewa maana kamili ya maneno haya ambayo hata wao yanawahusu kuyaheshimu.
 
Ina maana hawakuomba kibali cha maandamano mpaka Leo? Mbona kama hawana weledi?
Hao wanafunzi hata mi siwaelewi kwanini wanataka kuandamana? Kuhusu kumpokea mtu sidhani kama inahitaji kibali
 
Club ya Simba walivyopokelewa juzi wakitokea Mtwara baada ya kubeba kombe la ligi waliomba kibali..acha kuwa na akili kama za geshi la polithi kama kweli wewe sio lumumba

Hii ni vita(mapambano) na inabidi kutumia mbinu mbalimbali sio lazima kujilinganisha na simba au CCM juzi wamefanya maandamano kumtambulisha H. Mwinyi we unadhani waliomba kibali??

Ila CDM wangeomba wao halafu tuwasikie Polisi wanatoa visababu gani vya uongo na kweli hapo tungekua na la kusema
 
Nilitaka nishangae hawa viumbe walikalie hili kmya,nadhan ingekuwa mara ya kwanza
 
ngoja nyumbu atayekaidi akutane na kifinyo ...
 
kweli tuko kwenye msiba mzito hatuwezi kuandamanakupokea mtu tukaacha msiba huo utakuwa ni ulofa
 
Hakuna uwezekano wowote wa wao kupewa kibali chochote, maana rais aliyepo hampendi Lissu. Sasa hivyo vyombo vya dola vingetumika tu kutokuwa hicho kibali. Sio mara moja au 2 vibali vinakataliwa kutolewa kwa sababu za kisiasa.
Sio rais tu ,hata raia,kwani lissu ni nani hadi apendwe na kila mtu? Pesa yenyewe tu kuna baadhi wanaichukia màana imewaletea madhara makubwa,ije kubwa huyu rais wenu wa mitandaoni?


Tena naamba ajichanganye tummalize mapema sana
 
Ombeni kibari jmn tukampokee mtanzania mwenyewe, wengine hatutaki kuvunjwa miguu na mikono
 
Sio rais tu ,hata raia,kwani lissu ni nani hadi apendwe na kila mtu? Pesa yenyewe tu kuna baadhi wanaichukia màana imewaletea madhara makubwa,ije kubwa huyu rais wenu wa mitandaoni?


Tena naamba ajichanganye tummalize mapema sana

Hilo la kummaliza mapema mbona linaeleweka, safari hii ubebe bunduki ww usimuachie yule fala mwenzako. Naongelea rais maana ndio mwenye amri kwenye taasisi za kimamlaka. Raia kama ww ni mviziaji tu, huna lolote unaloweza kufanya kwenye maeneo ya kimamlaka.
 
Maandamano ya nini wao wamesema wanaenda kumpokea lissu kama vile ilivyopokelewa club ya Simba ikitokea Mtwara baada ya kupokea kombe lao la ligi...wasio kuwa na weledi ni hawa waliotoa andiko lisilokuwa na kichwa wala miguu..walivyo vilaza hata anayepokelewa wanajitoa akili eti hawamtaji jina...kisa maelekezo kutoka juu

Wewe bawacha hata Simba huwa wanakibali... kama ni mkusanyiko wa kukuaanya watu wengi ni lazima waombe kibali sio gheto pale
 
Jeshi la polisi limesema limeona baadhi ya viongozi wa CHADEMA wakihamasisha kukusanyika ili kumpokea mmoja wa kiongozi wanayetarajia kurejea nchini Julai 27, 2020.

Polisi wamesema hawana taarifa rasmi ya mikusanyiko hiyo inayohamasishwa mitandaoni. Wamesema ni haki yao kukusanyika lakini hakuna haki bila wajibu, hivyo wamewataka viongozi hao kufuata sheria.

Aidha jeshi la polisi limesema linafuatilia wanaosambaza ujumbe wa kuhamasisha wanafunzikugoma kwa kutoingia madarasani ili kushinikiza Bodi ya Mikopo kurejea masharti ya mkataba ya fedha ya kujikimu.

Polisi wamesema hawatasita kuwachukulia hatua wanaokiuka sheria, kwa kuitisha mikusanyiko na maandamano yasiyo na Baraka za kisheria, hivyo wamewataka wanafunzi wafuate njia stahiki za kufikisha malalamiko yao na sio kukiuka sheria.



View attachment 1516564
View attachment 1516567
Hakuna anaye omba mauti, lakini kwa busara za kawaida hii ni bahati mbaya kwa ujio WA Lisu and na so called mapokezi ya Lisu. Kifo na maombolezo ya kifo cha BWM is a national event. Lakini ujio wa Lisu siyo. Pasipo kutarajia wala kupanga police sasa wamepata legitimate reason ya kuzuia mkusanyiko wa mapokezi ya Lisu.

Labda kwenye same flight kuna viongozi wa kitaifa toka nchi za nje wanaokuja msibani. And therefore ni makosa kwa Chadema to ignore haya mazingira mapya.

Kwa hiyo ingekuwa busara viongozi wa Chadema wakaepuka confrontations na police isiyo ya lazima. Ingependeza wajitokeze viongozi wachache and family members tu kwenye mapokezi hayo na baadae wapange those mega events kwa ajili yake baada ya siku 7 za maombolezo. Simple common sense.
 
Jeshi la polisi limetoa tamko pole na la kistaarabu sana . Safi sana
 
Back
Top Bottom