Prof. Assad: Mfumo wa Siasa una shida. Huwezi kuzungumzia Kilimo wakati huna Mabwawa

Prof. Assad: Mfumo wa Siasa una shida. Huwezi kuzungumzia Kilimo wakati huna Mabwawa

Hayo mabwawa kujengwa kwa Kila kijiji n muhimu sana unaweza ukajenga lakwako private wakaja viongoz wakakuweka ndan wanakwambia unakausha mto ukisema uingize mipira mton uvute maji pia n kosa nchi hii kilimo kiko nyuma viongoz ndohao

Hilo ndio tatizo maana kila jema wao kwao ni Shari
Kuendeleza kitu hawawezi na hata wakiambiwa wafanye wanataka rushwa kukamilisha kitu
Mbona Late Mengi aliruhusiwa kujenga kwenye hifadhi na alilinda eneo vizuri
 
Nchi hii takribani asilimia 70 ya watu wake wanafanya kazi kwenye kilimo na wanaishi vijijini lakini huoni jitihada za kueleweka za watawala kwenye hiyo sekta. Utapunguzaje umaskini, umachinga uliokithiri na bodaboda kama huwekezi serious kwenye Kilimo!

Suala la Rais na mawaziri kuzunguka mikoani linashabikiwa na raia wengi tu na wanaona huo ndio uchapakazi.Kuna watu hawataki kabisa kusikia kazi za Rais na mawaziri ni za ofisini zaidi na sio kuzunguka vijijini au mitaani, hawaelewi kwa nini kuna watendaji wa kata, Halmashauri, DED , mkuu wa wilaya na mkoa au majukumu yao ni yapi ndio maana unaweza kukuta waziri anakagua tiketi za mabasi stendi au anatatua mgogoro wa shamba kijijini! Huwezi kuendesha nchi ya watu milioni 60 kwa namna hii na ikasonga mbele.
Ni kweli kabisa mkuu dhana ya serikali za mitaa/Halmashauri imeanza kutoeleweka kabisa kipindi hiki. Pia bahati mbaya Sana awamu ya tano ilikuja na panga kali na kuzichinjilia mbali Halmashauri zote za wilaya kwa kuzipora vyanzo vyake vya mapato, hivyo zikawa tegemezi na omba omba kwa serikali kuu. Imagine Halmashauri inasubiri Rais aitembelee na kutamka natoa milioni 500 mjenge soko au stend au mnunue ambulance kweli???
 
Hahaaa!!mfano waziri wa maji kila siku yuko ziarani tu, kupiga mikwara kwa miaka zaidi ya sita sasa, lakini matatizo ni yale yale tu, kila anaporudi tena eneo lile anakutana na tatizo lile lile tena!!!
Hahahaaaa Sasa imagine huyu anapata wapi muda wa kukaa wizarani na kupanga Sera vipaumbele vya wizara? Kupanga mapendekezo ya sheria/kanuni mpya zinazoendana na mazingira etc
 
Siyo kila msomi anaweza kuyafanyia kazi mawazo yake wengi mpaka wapate nguvu kutoka upande mwingine.

Tuna mambo mengi yapo humu ambayo hao hao jamaa zako wanayatwaa hapa JF na kwenda kuyafanyia kazi huko unapopajua.
Nimesema kuwa wazo la kilimo cha umwagiliaji ni la siku nyingi. Tuuache kujipa ujiko eti wametowa hapa!! Tatizo liko kwenye kutekeleza.
 
Ni kweli kabisa mkuu dhana ya serikali za mitaa/Halmashauri imeanza kutoeleweka kabisa kipindi hiki. Pia bahati mbaya Sana awamu ya tano ilikuja na panga kali na kuzichinjilia mbali Halmashauri zote za wilaya kwa kuzipora vyanzo vyake vya mapato, hivyo zikawa tegemezi na omba omba kwa serikali kuu. Imagine Halmashauri inasubiri Rais aitembelee na kutamka natoa milioni 500 mjenge soko au stend au mnunue ambulance kweli???
Hawa watu wanaofanya kazi serikali za mitaa/Halmashauri wanalipwa. Kuwalipa watu ambao hawafanyi kazi wanazopaswa kufanya ni tatizo lingine kubwa zaidi, ina maana juu ya kukosekana tija na ufanisi katika utendaji pesa za walipakodi zinapotea bure tu. Vicious cycle .
 
Hahaaa!!mfano waziri wa maji kila siku yuko ziarani tu, kupiga mikwara kwa miaka zaidi ya sita sasa, lakini matatizo ni yale yale tu, kila anaporudi tena eneo lile anakutana na tatizo lile lile tena!!!
Bila kuondoa ccm tuzidi kukwama jamaa wamefika mwisho kufikiri hawawezi kututoa hapa
 
Mkoloni aliijenga nchi yetu kupitia kilimo tu sisi tumeshindwa nn
 
Hawa watu wakiwa wanakula hawasemi. Wakiwa na njaa, hasa njaa ya uzeeni watasema kila kitu.
 
Umaskini unaanzia kichwani!
Kwa hali ilivyo, HAKUNA HAJA YA KUWA NA WIZARA YA KILIMO
Wakulima wanaishi kama waokota matunda.
 
Mkoloni aliijenga nchi yetu kupitia kilimo tu sisi tumeshindwa nn
Uko sahihi mkoloni alikuwa mzuri Sana kwenye Rural economics

Tanzania hadi Leo pesa Za kigeni zinategemea kilimo cha pamba, kahawa, chai Na karafuu yaliyoletwa na wachumi WA kikoloni

Wakati WA mkoloni MA tulipopata uhuru matajiri walikuwa Wakulima WA vijijini inawezekana.Sema wengi serikalini wapi

Makabila Matajiri nI yatokayo Porini kunakolimwa hayo mazao
 
Pesa ipo kwenye kilimo soko la uhakika lipo
 
Nilikodi heka 5, nikanunua mbili..jumla zilikuwa saba...yaani mvua hakuna...uzuri mbegu nilikuwa sijanunua, haya mambo yakutegemea mvua sio kabisa
What a loss!
Pole mkuu ila mvua zipo njiani..mwaka huu ni maumivu kwa wakulima wengi.
 
Wanachama na wafuasi wengi wa CCM ni wakulima wa jembe la mkono linalotegemea Mvua… CCM na Mkulima ni marafiki wa kufa na kuzikana
Ikitokea chama cha siasa kikakomaa na hoja ya kilimo na wakulima, kitaing'oa CCM mapema asubuhi.
 
Back
Top Bottom