Afadhali umeedit No18.

Ungeharibu thread.
 
Hapo ndipo tunapoona mapungufu ya waTanzania, suala hili silo la rais wala chama cha upinzani au tabaka fulani la wananchi.

Suala hili ni la waTanzania wote haitakiwi majority wakae wamewaachia ulingoni wapo rais na wapinzani.
Huu ni mchakato wa wanasiasa na sio watanzania. Sijasikia jambo litakalomsaidia mtanzania bali mawazo ya wanasiasa kutafuta namna bora ya kuendelea kula keki ya Taifa.
 
Idadi ya wabunge kupitia chama husika hupelekea mganwanyo huo wa 10% uendeje.
 
Kuna kipi kipya kilikuwa hakijasemwa wakati wa kukusanya maoni ya Katiba mpya chini ya Jaji Warioba?

Kama kuna kipya ambacho mtu amekiona kwenye hiyo tume atuambie wenzake. Wasomi wetu wanatia aibu sana. Kama ni wasomi wa kweli si wangemwambia tu Rais maoni anayoyatafuta yako kwenye makabrasha ya Tume ya Warioba!!?

Cha ajabu hata Warioba naye alikubali kuhojiwa na hiyo Tume ya Mukandala. CCM watu wa ajabu sana.
 
  • Sheria zinazokwamisha ushiriki wa wa watu wenye ulemavu kwenye siasa ziangaliwe upya
Hawa watu wana nafasi zao special ambazo wamepewa kama kundi la watu maalumu.

Mimi ninachoweza kupendekeza kwenye kundi hili ni kwamba wanapokuwa wamepewa hizo nafasi zao (uwaziri kwa mfano), wawe wanabadilishana wao kwa wao tu na kwa kipindi cha miaka mitano. Tuseme kwa mfano, akimaliza mmoja miaka mitano, miaka mitano mingine anafuata mwingine na inapotokea kwa mfano dharula kwamba Baraza la Mawaziri limevunjwa (kwa sababu nyingine maalum tofauti na uchaguzi mkuu) au limefanyiwa marekebisho madogo, hawa watu wasiondolewe kwenye nafasi zao, na hivyo wasihusike na mabadiliko hayo; unless kama mtu mwenyewe alliyekuwa kwenye nafasi ya aina hiyo, awe amehusika kwa kiwango kikubwa sana katika kuchangia marekebisho hayo kufanyika

Zaidi ni kuwa napendekeza neno ULEMAVU lisitumike kwenye majina ya Wizara au Tasisi wanazotumika, isipokuwa litumike neno "MAHITAJI MAALUM" . Tusitume majina kama . "WIZARA YA....... NA WENYE ULEMAVU" bali tutumie "WIZARA YA....... NA WENYE MAHITAJI MAALUM"
 
Tume ya taifa ya Uchaguzi isilazimike kufuata amri ya yeyote, na utendaji wake uruhusiwe kuhojiwa mahakamani
 
Mbona kama Time Huru ya uchaguzi haikuzingatiwa sana???? Shida nini?
 
nafasi itangazwe, watu wafanyiwe usaili kisha majina yapelekwe kwa Rais kwa uteuzi[emoji3064] Hii hapana
 
Idadi ya wabunge kupitia chama husika hupelekea mganwanyo huo wa 10% uendeje.
Hapo ndipo sasa inabidi Profesa anirudishe tena kwenye Lecture Theatre za UDSM ili akanipige Lecture upya. Wewe nimekuelewa, ila yeye amenipoteza kabisa; anaanza kuni-prompt nianze kufanya investment kwenye siasa wakati sikuwa na mpango huo
 
SSH anapita mle mle katika njia za JK, Kwamba ruhusu demokrasia na wataongea sana tu na kadri wanavyoongea wanapimwa na hao wanao wasikiliza mwisho wa siku madhara ya siasa zao yanapunguzwa nguvu na ule uhuru wa wao kuongea.

Inataka moyo sana haswa kwa mwanasiasa kuwa na uwezo wa kuvumilia kile kinachosemwa na kukichukulia kama ni maneno ya kawaida na kuendelea na maisha kama vile hakuna kilichosemwa.
 
Watanzania tuna mambo,eti tunaridhia na kumuomba MTU aliyopo madarakani ndio arekebishe Katiba na aturuhusu kufanya mikutano ya kisiasa.
Kwa kweli sisi ni matahira wa mwisho Duniani.
 
Serikali iongeze utoaji wa elimu ya uraia, pia ifundishwe kwenye ngazi zote za elimu, pia mtaala wa elimu uzingatoe elimu ya uraia.
Kwa mara ya kwanza kabisa, hii hoja nyingine ya muhimu sana imeibuliwa hapa. Mimi nitafurahi zaidi kama taasisi za elimu pamoja na wizara husika watalipatia priority zaidi swala hili kuliko lile jingine la kubadilisha lugha ya mtaala wa nchi nzima kwenda kwenye Kiswahili
 
Naipongeza Kamati. Wamejaribu sana sana kuukaribia mstari unaoliliwa miaka yote na Watanzania. Mstari wa usawa na uwazi kwenye siasa za Tanzania.

Lajini Kamati hii imekwepa kabisa tena kwa tahadhari kubwa eneo la Mgombea Binafsi. Haki hii inaitaka serikali kuwajibika kwa kuiongezea kwenye sheria ya Uchaguzi

Pia, wangesema kabisa, sheria ya Uchaguzi iwaengue wakurugezi wa Halmashauri na Manispaa kuwa Wasimamizi wa Uchaguzi. Kila wilaya kuwepo na vetting ya kupata wasimamizi wa Uchaguzi hadi ngazi ya Kata
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…