Isiwe lazima mgombea nafasi ya kazi za uraisi,ubunge,udiwani na mwenyekiti wa mtaa kupitia vyama vya siasa.Ukijumlisha wananchi wote wanaojiandikisha kupiga kura ni asili mia ndogo ndio wanachama wa vyama vya siasa.Kihesabu kumyima mgombea binafsi siyo sahihii.
Michakato ya mabolesho ya katiba iwe na time frame.
Bila time frame ni sawa sawa na hakuna.
Kwani JK alikuja na hizi swaga za amsha popo,kuunda Tume ya Jaji Warioba, ikafanya kazi nzuri,lakini matokeo yake mchakato ukaingiliwa dudumizi,na hadi leo hatuna katiba mpya japo ilitumia pesa nyingi za walipa kodi.
Tatu yapo baadhi ya mambo mazuri kwenye katiba ya Kenya haswa Supreme Court, Tume za Uchaguzi,Mawaziri kutokuwa wabunge na wabunge kuwafanyia vetting mawaziri wateuliwa.Mama Samia yafanyie kazi.
Hakuna kitu kinaniudhi kama kupita bila kupingwa.
Mwisho kila raia mwenye sifa za kupiga kura iwe lazima kupiga kura,Switzerland wana sheria hiyo.Tumechoka kuona watu wanalalamikia kiongozi ambae wengi wao hawakwenda kupiga kura.