Prof. Mukandala: Matokeo ya Rais yahojiwe Mahakamani
lakini mimi pia navutwa shati
1623627160694.png

Pamoja.
 
Mimi binafsi sijaona lolote la maana katika tume hiyo. Mambo yote yapo kwenye Katiba. Mikutano,ruzuku uwiano wa wanawake vipo kwenye Katiba. Wamekula hela ya bure tuu hawa. Mikutano mbona tulikuwa tunafanya enzi za JK kwani ikawaje?
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan akipokea Ripoti ya Kikosi Kazi cha Kuratibu Maoni ya Wadau wa Demokrasia ya Vyama Vingi vya Siasa Ikulu jijini Dar es Salaam leo tarehe 21 Oktoba, 2022

Mapendekezo 18 ya Ripoti yanasomwa na Prof. Rwekaza Mukandala
  1. Kikosi kazi kinapendekeza mikutano ya hadhara ya vyama vya siasa iruhusiwe kufanyika kwa mujibu wa katiba na sheria, mikutano ya ndani ya vyama vya siasa iendelee kufanyika bila vikwazo vyovyote, yafanyike marekebisho ya sheria ili kuhakikisha mikutano ya hadhara inafanyika kwa ufanisi.
  2. Sheria ya vyama vya siasa ifanyiwe marekebisho ili kulipatia baraza la vyama vya siasa linaloundwa na vyama vyenyewe mamkala ya kushughulikia swala la uvunjifu wa maadili ya vyama vya siasa kupitia kamati yake ya maadili, msajili wa vyama vya siasa aandae muongozo wa chaguzi za ndani za vyama vya siasa.
  3. Mfumo wa sasa wa kugawa ruzuku kwa vyama vya siasa uendelee, isipokuwa 10% ya fedha zinazotolewa sasa zitolewe kwa mgawanyo sawa kwa vyama vyote vyenye usajili kamili.
  4. Tume ya taifa ya Uchaguzi isilazimike kufuata amri au maagizo ya mtu yeyote, idara yoyote ya serikali, chama chochote cha siasa, taasisi au asasi yoyote na utendaji wake uruhusiwe kuhojiwa kwenye mahakama ya juu ili kuongeza uwajibikaji wa tume.
  5. Wajumbe wa tume ya taifa ya uchaguzi wateuliwe na kamati inayoongozwa na jaji mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (mwenyekiti) jaji mkuu wa Zanzibar (M/mwenyekiti), kamishna wa serkretarieti ya maadili ya viongozi wa umma Tanzania bara, mwenyekiti wa tume ya maadili ya viongozi wa umma ya Zbar, mwenyekiti wa tume ya haki za binadamu na wajumbe 2 watakaoteuliwa na jaji mkuu wa JMT baada ya kupendekezwa na chama cha wanasheria Tanganyika na chama cha wanasheria Zbar. Pia, angalau wajumbe wawili wa uteuzi wawe wanawake, sifa za kuwa mwenyekiti, makamu au mjumbe ziainishwe, nafasi za ujumbe zitangazwe, watu wafanyiwe usaili kisha majina yapelekwe kwa Rais kwa uteuzi
  6. Matokeo ya Rais jahojiwe kwenye Mahakama ya juu
  7. Wasimamizi wa uchaguzi wazingatie sheria, maadili, weledi, uwazi na ushirikishwaji wa wadau wakati wa kufanya kazi zao. Wasimamizi watakaokiuka taratibu wawajibishwe kwa mujibu wa sheria.
  8. Tume ya taifa ya uchaguzi ipewe fedha kwa wakati ili iweze kutelekeza majukumu yake ipasavyo.
  9. Itungwe sheria kusimania shughuli za tume ya uchaguzi, pia iwepo sheria moja ya kusimamia chaguzi zote badaa ya uwepo wa sheria mbili kama sasa, maafisa wa uchaguzi watakao engua wagombea kushiriki uchaguzi bila kuzingatia sheria na weledi wawajibishwe kwa mujibu wa sheria.
  10. Matumizi ya tehama kwenye uchaguzi yaboreshwe na kuongezwa.
  11. Sharti ya uwepo wa sera ya jinsia liwepo kwenye kila chama cha siasa, na ujumuishi wa makundi maalumu, pia ushiriki wa jinsia moja kwenye vyombo vya maamuzi isipungue 40%. Pia, utaratibu wa uwakilishi wa viti maalumu kwa wanawake uendelee, isipokuwa sheria ziboreshwe kuweka ukomo wa miaka 10 pekee.
  12. Sheria zinazokwamisha ushiriki wa wa watu wenye ulemavu kwenye siasa ziangaliwe upya
  13. Juhudi za ushirikishwaji wa vijana kwenye siasa ziongezwe
  14. Serikali iongeze utoaji wa elimu ya uraia, pia ifundishwe kwenye ngazi zote za elimu, pia mtaala wa elimu uzingatoe elimu ya uraia na mpiga kura.
  15. Swala la rushwa litamkwe katika katiba ya nchi ili wananchi watambue kuwa vitendo vya rushwa havitavumiliwa wala kuonewa muhali. Katiba ya Chama cha Siasa iwe na adhabu ya kumuondoa katika Mchakato wa Uchaguzi Mgombea aliyedhaminiwa na chama akithibitika kuhusika na vitendo vya rushwa
  16. Kuanzishwe utaratibu wa mijadaa kila mwaka itakayohusisha viongozi wakubwa wa kitaifa na kisiasa ili kudumisha mshikamano, mahakama iwe ni mamlaka ya mwisho ya kuamua pindi maridhiano yanapokwama
  17. Wanahabari waunde chombo cha kusimamia wanahabari na vyombo vyao, vyombo vya umma vitoe muda sawa wa kutangaza habari za wagombea wa vyama vyote kwa usawa, uwepo mchakato wa wazi wa kuwajibisha vyombo vya habari badala ya kufungiwa pekee na mkurugenzi wa habari na mawasiliano
  18. Mchakato wa katiba mpya uendelee, hata hivyo mjadala wa kitaifa kuhusu katiba mpya uanze kabla ya kuanza kwa mchakato wa kuandika katiba mpya ili kujadili maswala ya msingi kama muungano, mamkala ya Rais, madaraka ya serikali za mtaa, Rushwa, mfumo wa uchaguzi n.k. Pia, sheria ya mabadiliko ya katiba na sheria ya kura ya maoni zihuishwe pamoja na kuundwa kwa jopo la wataalamu ili kufanya mapitio ya katiba inayopendekezwa kwa kuzingatia hali ya sasa ya kiasiasa, kiuchumi na kijamii.
View attachment 2393650
Rais Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha na Mwenyekiti wa Kikosi Kazi kuhusu Uratibu maoni ya wadau wa Demokrasia ya Vyama vingi vya Siasa Profesa Rwekaza Mukandala, Makamu Mwenyekiti Hamad Rashid Mohamed pamoja na Wajumbe wa Kikosi Kazi hicho mara baada ya kupokea Ripoti yao Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 21 Oktoba, 2022.

Maneno ya Rais Samia Suhuhu Hassan
Kazi hii imechukua miezi 10, haikuwa rahisi. Pengine ningewaacha ingechukua zaidi ya muda huu, lakini mimi pia navutwa shati.

Wananchi waelewe kuwa maoni ya kikosi kazi sio amri kwa Serikali. Tutaitana tena tuangalie na hali halisi ndani ya serikali na hali halisi ya sheria zetu pia ili tuweze kuyafanyia kazi vizuri

Tumepokea, na kama mlivyoona ripoti yenu ina mambo kadhaa, sisi kwenye serikali inabidi tujipange vikosi kadhaa, na wengine kati yenu tutawaomba mje kwenye vikosi kazi hivyo tujadili.

Siyo kwamba leo tumepewa ripoti ya kikosi kazi, kesho tutaanza kutekeleza hapana. Tumepokea, na wananchi wasikie tumepokea na tutafanyia kazi.

Na nyie watu wa siasa mjichambue, ni kazi ya jaji mtungi na watu wake. Nakubailiana na hoja ya 40% ya wanawake kwenye vyama vya siasa.

Tumepokea marekebisho ndani ya vyama vya siasa na wenyewe wasiwe mahodari wa kuirekebisha serikali lakini na wenyewe ndani tutizame je wanavyokwenda mambo ya usawa wa kijinsia yapo, mambo ya matumizi mazuri ya fedha yapo na mwengine akipata chama cha siasa anasema ni chake

Mgao wa ruzuku tutauangalia, hatuwezi kusema tutaongeza fedha zaidi sababu ni swala la kibajeti.

Matumizi ya teknolojia kwenye tume ya uchaguzi ni muhimu, ili teknolojia inayotumika iweze kutoa matarajio ambayo watu wanataka.

Tume ya uchaguzi tutalikalia kitako, ya serikali yatakwenda na ya ripoti nayo tutayaangalia.

Mijadala ya kisiasa kila mwaka iwepo, kaeni mjijadili, msijadili tu serikali, mjijadili na ninyi wenyewe. Mijadala heathy, hata serikali inaweza kuwezesha mijadala hii.

Wanawake mara nyingi nafasi muhimu wakigombea wanaambiwa kaa upande, au wanaambiwa njoo chukua hiyo gombea. Ukikuta wanawake kawekwa ni mwepesi mno, kapangwa kumsindikiza mtu. Kwa hili nakubaliana nao, ni pamoja na kuwasomesha wanawake, kuwatia moyo kwamba wanaweza.

Rushwa ni kidonda ndugu, hakuna hata chama kimoja kimenusurika hapa. Hakuna chama ambacho hakifanyi, nadhani ni tabia ambayo tunatakiwa kuibadilisha. Watu wajue, kuchaguliwa si mimi, ni chama. Hili la Rushwa, tujitazameni sote.

Maswala ya mikutano hakuna anayekataa, lakini lazima kuwe na jicho. Hatutaki kurudi tulikotoka, polisi wataanza tena kupiga watu. Tunaposema kwamba kanuni lazima tuzitazame siyo kwa nia mbaya, ni nia njema. Lazima tutazame kanuni na sheria ndipo turuhusu.
Nilitegemea Tume ije na hoja ya mgombea binafsi kuruhusiwa na pili Tume ya uchaguzi iwe na wafanyakazi wake wa kudumu kuanzia wilayani hadi Taifa . Haya ndio yalipaswa kuwa mambo muhimu kuliko yote.
 
Hapa nimenogewa hadi nimefika kileleni!👇🤗🤗🤗
 
Tukiitoa ccm tunaingiza chama gani ikulu!?
Kwani hiyo ccm ina tofauti gani na vyama vingine? Jibu jepesi; chama chochote kile kilicho sajiliwa kama cha siasa, kina haki na uwezo wa kuongoza nchi.

Kwanza hicho chama chenyewe cha ccm kimejaa vilaza tu na wasomi wengi feki! Lakini bado kipo madarakani kwa miaka zaidi ya 40! Hao wengine watashindwa vipi kuiongoza nchi? Au unataka useme nini?
 
Chama chochote wananchi wanachoona kinafaaa. Mbona Kenya wameweaa kuweka vyama vinne tofauti madarakani. Sisi bado tunajitoa fahama kwa kuuliza chama kipi kitaingia madarakani.
Hawa ndiyo wale wanao danganya Watanzania wajinga eti wakichagua upinzani, kutatokea vita!!

Yaani ccm wanajiona wana uwezo na haki ya kila kitu kwenye hii nchi! Kumbe wengi wao ni viazi tu.
 
Kwani hiyo ccm ina tofauti gani na vyama vingine? Jibu jepesi; chama chochote kile kilicho sajiliwa kama cha siasa, kina haki na uwezo wa kuongoza nchi.

Kwanza hicho chama chenyewe cha ccm kimejaa vilaza tu na wasomi wengi feki! Lakini bado kipo madarakani kwa miaka zaidi ya 40! Hao wengine watashindwa vipi kuiongoza nchi? Au unataka useme nini?
Chadema chama mtu binafsi na anakiendesha Kama biashara maana kamuweka mkwewe pale juu na zaidi hakina watu wenye charisma ya uongozi,hatuwezi kumpa lema wizara,cuf hata sijui Kuna akina nani huko...ccm imesheheni,upinzani hakuna chama kinachounganisha nchi kidini,kikabila na Kanda,hiki kinaungwa mkono na watu wa dini hii kile wa dini ile...wenye akili hawawezi acha mambo ccm itolewe ili mambo yajiendee tu,nchi siyo mbuga za wanyama
 
Chama chochote wananchi wanachoona kinafaaa. Mbona Kenya wameweaa kuweka vyama vinne tofauti madarakani. Sisi bado tunajitoa fahama kwa kuuliza chama kipi kitaingia madarakani.
Kwa hiyo kwa akili zako KANU ya Kenyatta siyo hiyo aliyoitumia uhuru kukaa madarakani!!?..zaidi wanasiasa wa Kenya wanaakisi weledi wa kiungozi,huwezi kumpa nchi mbowe au lissu
 
Mapendekezo 18 ya Wadau wa Demokrasia ya Vyama vingi vya Siasa; Ripoti yanasomwa na Prof. Rwekaza Mukandala

1. Kikosi kazi kinapendekeza mikutano ya hadhara ya vyama vya siasa iruhusiwe kufanyika kwa mujibu wa katiba na sheria, mikutano ya ndani ya vyama vya siasa iendelee kufanyika bila vikwazo vyovyote, yafanyike marekebisho ya sheria ili kuhakikisha mikutano ya hadhara inafanyika kwa ufanisi.

2. Sheria ya vyama vya siasa ifanyiwe marekebisho ili kulipatia baraza la vyama vya siasa linaloundwa na vyama vyenyewe mamkala ya kushughulikia swala la uvunjifu wa maadili ya vyama vya siasa kupitia kamati yake ya maadili, msajili wa vyama vya siasa aandae muongozo wa chaguzi za ndani za vyama vya siasa.

3. Mfumo wa sasa wa kugawa ruzuku kwa vyama vya siasa uendelee, isipokuwa 10% ya fedha zinazotolewa sasa zitolewe kwa mgawanyo sawa kwa vyama vyote vyenye usajili kamili.

4. Tume ya taifa ya Uchaguzi isilazimike kufuata amri au maagizo ya mtu yeyote, idara yoyote ya serikali, chama chochote cha siasa, taasisi au asasi yoyote na utendaji wake uruhusiwe kuhojiwa kwenye mahakama ya juu ili kuongeza uwajibikaji wa tume.

5. Wajumbe wa tume ya taifa ya uchaguzi wateuliwe na kamati inayoongozwa na jaji mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (mwenyekiti) jaji mkuu wa Zanzibar (M/mwenyekiti), kamishna wa serkretarieti ya maadili ya viongozi wa umma Tanzania bara, mwenyekiti wa tume ya maadili ya viongozi wa umma ya Zbar, mwenyekiti wa tume ya haki za binadamu na wajumbe 2 watakaoteuliwa na jaji mkuu wa JMT baada ya kupendekezwa na chama cha wanasheria Tanganyika na chama cha wanasheria Zbar. Pia, angalau wajumbe wawili wa uteuzi wawe wanawake, sifa za kuwa mwenyekiti, makamu au mjumbe ziainishwe, nafasi za ujumbe zitangazwe, watu wafanyiwe usaili kisha majina yapelekwe kwa Rais kwa uteuzi

6. Matokeo ya Rais jahojiwe kwenye Mahakama ya juu

7. Wasimamizi wa uchaguzi wazingatie sheria, maadili, weledi, uwazi na ushirikishwaji wa wadau wakati wa kufanya kazi zao. Wasimamizi watakaokiuka taratibu wawajibishwe kwa mujibu wa sheria.

8. Tume ya taifa ya uchaguzi ipewe fedha kwa wakati

9. Itungwe sheria kusimania shughuli za tume ya uchaguzi, pia iwepo sheria moja ya kusimamia chaguzi zote, maafisa wa uchaguzi wanaoengua wagombea bila sababu maalumu wawajibishwe

10. Matumizi ya tehama kwenye uchaguzi yaboreshwe

11. Sharti ya uwepo wa sera ya jinsia liwepo kwenye sheria za vyama vya siasa, pia ushiriki wa wanawake kwenye vyombo vya maamuzi isipungue 40%

12. Sheria zinazokwamisha ushiriki wa wa watu wenye ulemavu kwenye siasa ziangaliwe upya

13. Juhudi za ushirikishwaji wa vijana kwenye siasa ziongezwe

14. Serikali iongeze utoaji wa elimu ya uraia, pia ifundishwe kwenye ngazi zote za elimu, pia mtaala wa elimu uzingatoe elimu ya uraia.

15. Swala la rushwa litamkwe katika katiba ya nchi ili wananchi waelewe

16. Kuanzishwe utaratibu wa mijadaa kila mwaka itakayohusisha viongozi wakubwa wa kitaifa na kisiasa ili kudumisha mshikamano, mahakama iwe ni mamlaka ya mwisho ya kuamua pindi maridhiano yanapokwama

17. Wanahabari waunde chombo cha kusimamia wanahabari na vyombo vyao, vyombo vya umma vitoe muda sawa wa kutangaza habari za wagombea wa vyama vyote kwa usawa, uwepo mchakato wa wazi wa kuwajibisha vyombo vya habari badala ya kufungiwa pekee na mkurugenzi wa habari na mawasiliano

18. Mchakato wa katiba mpya uendelee, hata hivyo mjadala wa kitaifa kuhusu katiba mpya uanze kabla ya kuanza kwa mchakato wa kuandika katiba mpya ili kujadili ajenda muhimu za muungano, mamkala ya Rais, Rushwa, tume ya uchaguzi n.k
 
Attachments

  • FflYQoKXwAI96ly.jpg
    FflYQoKXwAI96ly.jpg
    95.7 KB · Views: 1
  • FflaCeFXkAI8UnM.jpg
    FflaCeFXkAI8UnM.jpg
    607.7 KB · Views: 1
Chadema chama mtu binafsi na anakiendesha Kama biashara maana kamuweka mkwewe pale juu na zaidi hakina watu wenye charisma ya uongozi,hatuwezi kumpa lema wizara,cuf hata sijui Kuna akina nani huko...ccm imesheheni,upinzani hakuna chama kinachounganisha nchi kidini,kikabila na Kanda,hiki kinaungwa mkono na watu wa dini hii kile wa dini ile...wenye akili hawawezi acha mambo ccm itolewe ili mambo yajiendee tu,nchi siyo mbuga za wanyama
Mimi sijaitaja hiyo Chadema kwenye maelezo yangu! By the way, hata hiyo ccm yako yenyewe bado inamilikiwa na watu wachache tu miaka nenda! Huku wakirithishana madaraka kutoka kizazi kimoja, kwenda kingine!

Hivyo bado huna hoja yenye mashiko juu ya Tanzania kuongozwa na serikali ya chama kingine, nje ya ccm.
 
Nimeitaja chadema na cuf,ccm siyo Mali ya mtu binafsi,ccm ni Mali ya Dola,ilikua Mali ya umma tangu ikiwa TAA,TANU
 
Nchii shenzi sana, inakuwaje mtu anajiita Prof. Anajadili sheria inayofanya kazi??
Hivi tunatofauti gani na nyani wa porini?
Tofauti ninayoiona no kwamba watanzania hatuna mikia ndo tofauti tulionayo.
Sheria inatambua vyama vya siasa lkn washenzi wanajadili sheria???? Shit
 
Back
Top Bottom