TANZIA Profesa Honest Ngowi afariki dunia kwenye ajali Mlandizi Pwani. Alikuwa mhadhiri Chuo Kikuu Mzumbe

TANZIA Profesa Honest Ngowi afariki dunia kwenye ajali Mlandizi Pwani. Alikuwa mhadhiri Chuo Kikuu Mzumbe

Juzi nimetoka Mbeya aisee hayo matenka ya mafuta niyokutana nayo barabarani in one day ni zaidi ya mia tano!! Nikajiuliza hivi lile Bomba la mafuta la TAZARA na reli ya TAZARA vina kazi gani?? Na hapo ni njia ya Dar to Mbeya only..
Halafu utakuta mtu kama wewe pia unapinga SGR
 
Juzi nimetoka Mbeya aisee hayo matenka ya mafuta niyokutana nayo barabarani in one day ni zaidi ya mia tano!! Nikajiuliza hivi lile Bomba la mafuta la TAZARA na reli ya TAZARA vina kazi gani?? Na hapo ni njia ya Dar to Mbeya only..
Afadhali,itoke sheria,makonteina,na mizigo mikubwa ,isafirishwe kwa njia ya reli.
 
Rip,I wish haya malori yawe na barabara yao yakupita siku, yanaongoza kwa ajali nyingi za barabarani,mara zikosee njia,mara zifel kupanda mlima,mara contena lianguke kwenye gari ndogo tafran!
 
Habari Wote.

Makamu Mkuu wa Chuo Prof. Lughano Kusiluka anasikitika kutangaza kifo cha Prof. Honest Ngowi na Dereva wake, waliofariki asubuhi ya leo kwa ajali ya gari wakiwa njiani kuja Kampasi Kuu Morogoro.

Tunaomba muwe watulivu wakati Menejiementi inaendelea kufuatilia taarifa kamili ya tukio hili, na kuweka taratibu zingine. Taarifa zaidi zitatolewa rasmi na taratibu zingine za kuwahifadhi wenzetu.

Bwana alitoa na Bwana Ametwaa jina la Bwana lihimidiwe. Poleni Wote kwa msiba huu mzito.

Imetokewa na,

Ofisi ya Mawasiliano

View attachment 2166663
Profesa Honest Ngowi enzi za uhai wake
Profesa Honest Ngowi wa Chuo Kikuu Mzumbe amefariki dunia katika ajali ya gari iliyotokea asubuhi ya leo eneo la Mlandizi, Kibaha mkoani Pwani. Lori iliacha njia na kuilalia gari ya Ngowi. Alitoka kwenye ajali akiwa majeruhi, amefariki akiwa hospitali.

Pia soma > Dkt. Honest Ngowi aichambua sekta ya gesi na kukiri Serikali imejipanga


=======

Professor Honest Prosper Ngowi (PhD Economics) alikuwa mkuu wa idara ya kozi fupi, utafiti na ushauri chuo kikuu cha Mzumbe kampasi ya Dar es Salaam. Pia ni muanzilishi wa kampuni ya ushauri ya ANO. Katika maisha yake amekuwa mtafiti, mshauri na kuchapisha machapisho ya kitaaluma zaidi ya 60, tafiti zaidi ya 70 pia makala zaidi ya 250 kwenye magazeti.

Prof. Ngowi amebobea kwenye uchumi wa maendeleo na biashara hasa kwenye uchumi mkubwa, biashara ya kimataifa, uwekezaji wa kigeni, ujasiriamali, uchumi wa mafuta na gesi na mengineyo. Prof. Ngowi pia amefanya kazi kama msahihishaji wa nje kwenye vyuo mbalimbali ikiwemo chuo kikuu cha Makerere, Udsm, North West University(Afrika kusini) na vingine vingi.
Pole sana kwa Familia yake, pole kwa Wanataaluma Wote, pole kwa Taasisi za Elimu ya Juu zote nchini ( hasa hasa Chuo Kikuu cha Mzumbe ), na pole nyingi mno kwa Watanzania kwa huyu Mwamba wa Tasnia ya Uchumi nchini Tanzania.

Kifo chake Kimenisikitisha Binafsi kwakuwa Marehemu alikuwa ni Mtafsiri na Mchambuzi mahiri wa Masuala ya Kiuchumi na alikuwa hachoshi ama Kumsikiliza au hata Kumsoma katika Gazeti la The Citizen ambako alikuwa na Ukurasa wake Maalum wa Kuchambua Uchumi.

Somo la Uchumi ni gumu ila Marehemu Profesa Ngowi alikuwa akilifanya liwe rahisi Kueleweka na hata Mtu wa Kawaida tu Kulipenda na Kupenda kulifuatilia na Kujifunza mengi. Namfananisha Profesa Ngowi ( Marehemu ) kuwa ni Mtaalam Mahiri wa Uchumi kama walivyo Wachezaji wangu Wapendwa Clatous Chama ( Simba SC ) na Khalid Aucho ( Yanga SC ) ambao huufanya Mpira wa Miguu Kuonekana ni Mchezo rahisi Kuucheza wakati kumbe ni mgumu.

Nitamkumbuka hasa kwa tabia yake ya kutokupenda Sifa kama Wanazuoni ( Wanataaluma ) wengine na muda mwingi kuwa mtaratibu, msikilizaji na Mwalimu mahiri aliyeshiba vyema Somo la Uchumi.

Chuo Kikuu cha Mzumbe najua kuwa mmempoteza Mtu Muhimu ( Mhadhiri Mwandamizi ) huyu na najua Pengo lake si rahisi Kuzibika ila hata na Sisi Watanzania wengine tu tena wa Kawaida ( kama Mimi GENTAMYCINE ) tumeguswa na huu Msiba wake.

Namuombea Makazi Mema Mbinguni.
 
Daaah, Mungu wangu..nimelia kwa uchungu sana,
Jana mchana tu nimetoka kwake kutibia Mifugo yake.
Rest in peace Prof😭
Kwahiyo hata malipo yako ilikua bado kupewa, sivyo? Watanzania mnachekesha sana.
 
Tunawasikia tu wakishaondoka.
Kuna watu wenye taaluma kubwa kama hizi,wakiwa hai,hatupati habari zao,sisi wananchi wa kawaida.Tungeomba hapa JF,kuwe na platform,ya kutufahamisha ,Watu muhimu kama hawa,wako wapi,na tutawapata vipi,ili kutupa ushauri wa kuchanganyua changamoto tulizo nazo.
 
Tunawasikia tu wakishaondoka.
Kuna watu wenye taaluma kubwa kama hizi,wakiwa hai,hatupati habari zao,sisi wananchi wa kawaida.Tungeomba hapa JF,kuwe na platform,ya kutufahamisha ,Watu muhimu kama hawa,wako wapi,na tutawapata vipi,ili kutupa ushauri wa kuchanganyua changamoto tulizo nazo.
 
Sasa tuna wasomi wazuri namna hii lkn shida iko wapi mbona nchi zetu hazieleweki.Wanaimplement wapi hii elimu yao?
 
Maroli yakaguliwe sana wengi haean muda ni kukimbizana maizigo bandarini.
 
Acha shobo mtt wa kiume, unaropoka kama umemeza shaha**
Kulikua na haja gani kuja kulia lia hapa kwamba ulimfanyia marehemu kazi? Ili iweje? Tukuonee huruma au? Kijana wa hovyo sana wewe.
 
Kifo Cha Prof Ngowi kimeniuma kama nimempoteza kaka yangu Genius. Yani nilimpenda na kiukweli taifa tumepoteza kichwa. Jambo lakutisha sana uwenda mpaka sasa kama Taifa hatujajuwa umuhimu wa hiz think tank. Usije ukashanga Hit team ya taifa fulani imemmaliza. Why 😭 mtu mmoja aweza kuwa mchawi wa mapinduzi ya uchumi nakuliokoa taifa ktk dhiki na ukimuondoa huwez pata kichwa kama hiko tena.

Nilazima kama Taifa tujuwe tupo ktk mabadiliko makubwa ya uchumi na kama sijakosea huyu Prof was among RC that team. Kubadili fikra za vijana kutoka kuajiriwa na kujiajiri.

Prof Amelala amelala na maujanja yote yakulikomboa Taifa. Kiukweli Mungu ndie anajuwa ila nadiriki kusema Prof hajafa bali ameondoshwa na viumbe tusivyo viona je aligusa nini au alitegewa nini Mungu Mungu ndie anajuwa. Kifo Cha Prof Ngowi kinatukumbusha kumbukizi zakutisha kwenye same barabara Moja Waziri Mkuu Sokoine, Pili Mch Mtikila tatu Mzee Kombe na mwisho😭😭😭.

Tusipo fungua macho tutakuwa vipofu natusipo kuwa vipofu tutakuwa mazezeta... 😭😭😭🤐🤐🤐🤐

Hii barabara inatisha sana wajuvi tujuzen.

Bwana ametoa na Bwana ametwaa jina lake lihimidiwe.
 
Mmefukuza madereva wazuri kwa sababu za kipuuzi za vyeti fake mara sijui dereva naye awe form four wakati mbunge ni darasa la saba, pumbavu kabisa.

Qualification ya driver ni driving license na siyo hawa waliokosa ajira kwenye soko la ajira na kukimbilia udereva, kuendesha Passo yako ni tofauti kabisa na professional driving.

Ukiwa unasafiri jihadhari sana na hizi plate namba za STL, DFP na SU, hakuna madereva humo siku hizi ndio mitambo ya kupeleka watu kuzimu.

Umeongea ujinga sana hao wamefatwa na hiyo contena walikua upande wao kabisaaa...
Acha kuzungumza vitu hujui na kwa watu usowajua
 
Back
Top Bottom