Majeshi ya Urusi yalifurushwa toka mjini Kiev huku Ukraine ikiwa haina msaada wowote toka Taifa la nje. Tena wakati huo Urusi ikitumia kikosi chake cha juu kabisa kwenye utaalam wa kivira. Bahati mbaya askati hao, walio wengi waliangamia kwa kuuawa na Askari wa Ukraine, wengine waliuawa na wananchi wa kawaida.
Baada ya mafanikio hayo ya awali ndipo USA na mataifa ya Ulaya yalipoona kuwa kumbe kuna uwezekano wa Uktaine kupambana na Urusi endapo akisaidiwa kwa kupewa silaha.
Kadiri vita inavyoendelea, wataalam wote wa masuala la kivita waliotoa maoni yaowanakubaliana kuwa uwezo wa kivita wa Urusi ulikuwa over-exagerated. Kwa sasa inaonekana wazi kabisa kuwa utaalam wa kivita wa Urusi na Ukraine, huenda Ukraine wapo vizuri zaidi, maana wakiamua kushambulia vusima vya mafuta, wanapiga hapo hapo. Lakini Urusi ina lengo la kupiga ghala la silaha, inaenda kupiga hospitali, wakati hospitali ipo kilometer 5 toka kwenye target.
Urusi kwa sasa anasaidiwa zaidi na ukubwa wa uchumi na hifadhi ya silaha alizozitengeneza kwa miaka mingi, ukilinganisha na Ukraine, lakini kiutaalam wa vita, hana cha pekee dhidi ya Ukraine.
Na vita hii ikiisha, baada ya miaka 10 ijayo, Ukraine itakuwa miongoni mwa mataifa yenye jeshi bora kabisa Duniani.