Umeunena ukweli. Kwanza Urusi inaficha hasara inayoipata. Kuna wakati vyombo vya ndani ya Urusi vilikanusha juu ya idadi ya askari wa Urusi wanaokufa vitani, vikisema kuwa Serikali wanataja idadi ndogo wakati waliokufa ni wengi zaidi. Vyombo vya habari viliongea na kukusanya taarifa kutoka kwa ndugu walioletewa miili ya wapendwa wao, ikawa idadi hiyo ni kubwa kupindukia ile inayotangazwa na Serikali. Wakati wapo pia waliofia vitani ambao hata miili yao haikurejeshwa kwa familia. Kilichofuatia ni wale wanahabari kukamatwa, kufunguliwa mashtaka bandia, na kufungwa jela.
Ukraine ndiyo ipo mstari wa mbele katika kuripoti vifo vya watu wake ili ionewe huruma, na Dunia iuone uovu wa Urusi, lakini Urusi inaficha.
Ukitaka kuujua ukweli, angalia wakati wa ubadilishanaji mateka. Unakuta Ukraine inarudishiwa askari wake 150, na Urusi inarudishiwa asjari wake 150. Shambulio la juzi tu la Kursk, askari zaidi ya 500 wanechukuliwa mateka na Ukraine. Na Ukraine inawahifadhi hao matrka kwenye maeneo yaliyo karibu na maghala ya silaha, ili kama Urusi itaamua kuyashambulia maeneo hayo, iwamalize askari wake yenyewe.
Sasa hivi Ukraine imefikia kutengeneza mpaka fake drones, ambazo moja igharimu chini ya dola 20,000; lakini Urusi inaitungua hiyo drone kwa kombora lenye gharama ya dola milioni 1, yaani mara 50 ya gharama ya drone inayotunguliwa. Na Urusi haiwezi kuacha kuzitungua hizo fake drones kwa sababu Ukraine inachanganya hizo fake drones na attacking drones, na Urusi haina uwezo wa kujua ipo ni halisia na ipi ni fake. Na Ukraine inafanya hivyo ili kuzidi kuigharamisha Urusi, na ikiwezekana ipungukiwe na stock ya makombora. Fikiria sasa Urusi imefikia kuomba msaada wa makombora toka North Korea na Iran. Wakati huo Ukraine ambayo hapo awali ilikuwa haitengenezi makombora, sasa imeanza kuyatengeneza ndani ya nchi yake, huku ikipewa pesa za kugharamia mirasi di kama hiyo na mataifa mbalimbali.