Putin, ameanza kuona gharama za ya Vita. Mara ya kwanza alikuwa anasoma sana Threads za JF akapotoshwa?

Putin, ameanza kuona gharama za ya Vita. Mara ya kwanza alikuwa anasoma sana Threads za JF akapotoshwa?

Akina Ritz Webabu ChoiceVariable FaizaFoxy walikuwa wanampotosha sana Putin. Akajikuta yeye ni Mwaaaaaaamba. Akasema ana operation ya siku chache kumwondoa Rais wa Ukraine.

Mwaka wa pili sasa.... Nashindwa kuelewa. Putin ni Jasusi mbobevu alidanganywa vipi? Alichemka wapi? Anyway kuanza upya si Ujinga. Akae wayamalize na Ukraine. Vita si lelemama. Watu walitaka kupima nguvu yake. Ameji expose sana. Bora angebaki vile vile ambavyo tulikuwa tunamwogopea. Akina Yericko Nyerere siku hizi wamekata na tamaa kabisa. Nyie msidhani hata mataifa makubwa yanataka vita. Mwenye kujielewa anaepusha mapema.

View attachment 3087753
Unafikiri Ukraine au Putin ndiyo wamechelewesha vita?

Kumbe hata kinachoendelea hukielewi.

Hilo tangazo la Putin ni bonge la strategy ya kisaikolojia.
 
Hasara inayotokanana matokeo ya ndani kwenye serikali yake Putin utayajua saa ngapi mrusi mweusi wewe

Wakati wewe ukiona kuchinja wanajeshi wa Ukraine ndio ushindi, kumbe usijue hicho kichinjio kinagharama ipi katika serikali ya Russia na Putin

Ni ujinga kuamini eti Russia haimgharimu chochote hii vita

Nasemaje..! Anayohasara kubwa mno kiasi cha yeye kurudi nyuma kiuchumi tofauti na asingekuwa na vita

Na pia nakuhakikishia kwamba, Putin hatashinda hiyo vita licha kwamba nje mnaona Ukrain kachakazwa
Umeunena ukweli. Kwanza Urusi inaficha hasara inayoipata. Kuna wakati vyombo vya ndani ya Urusi vilikanusha juu ya idadi ya askari wa Urusi wanaokufa vitani, vikisema kuwa Serikali wanataja idadi ndogo wakati waliokufa ni wengi zaidi. Vyombo vya habari viliongea na kukusanya taarifa kutoka kwa ndugu walioletewa miili ya wapendwa wao, ikawa idadi hiyo ni kubwa kupindukia ile inayotangazwa na Serikali. Wakati wapo pia waliofia vitani ambao hata miili yao haikurejeshwa kwa familia. Kilichofuatia ni wale wanahabari kukamatwa, kufunguliwa mashtaka bandia, na kufungwa jela.

Ukraine ndiyo ipo mstari wa mbele katika kuripoti vifo vya watu wake ili ionewe huruma, na Dunia iuone uovu wa Urusi, lakini Urusi inaficha.

Ukitaka kuujua ukweli, angalia wakati wa ubadilishanaji mateka. Unakuta Ukraine inarudishiwa askari wake 150, na Urusi inarudishiwa asjari wake 150. Shambulio la juzi tu la Kursk, askari zaidi ya 500 wanechukuliwa mateka na Ukraine. Na Ukraine inawahifadhi hao matrka kwenye maeneo yaliyo karibu na maghala ya silaha, ili kama Urusi itaamua kuyashambulia maeneo hayo, iwamalize askari wake yenyewe.

Sasa hivi Ukraine imefikia kutengeneza mpaka fake drones, ambazo moja igharimu chini ya dola 20,000; lakini Urusi inaitungua hiyo drone kwa kombora lenye gharama ya dola milioni 1, yaani mara 50 ya gharama ya drone inayotunguliwa. Na Urusi haiwezi kuacha kuzitungua hizo fake drones kwa sababu Ukraine inachanganya hizo fake drones na attacking drones, na Urusi haina uwezo wa kujua ipo ni halisia na ipi ni fake. Na Ukraine inafanya hivyo ili kuzidi kuigharamisha Urusi, na ikiwezekana ipungukiwe na stock ya makombora. Fikiria sasa Urusi imefikia kuomba msaada wa makombora toka North Korea na Iran. Wakati huo Ukraine ambayo hapo awali ilikuwa haitengenezi makombora, sasa imeanza kuyatengeneza ndani ya nchi yake, huku ikipewa pesa za kugharamia miradi kama hiyo na mataifa mbalimbali.
 
Akina Ritz Webabu ChoiceVariable FaizaFoxy walikuwa wanampotosha sana Putin. Akajikuta yeye ni Mwaaaaaaamba. Akasema ana operation ya siku chache kumwondoa Rais wa Ukraine.

Mwaka wa pili sasa.... Nashindwa kuelewa. Putin ni Jasusi mbobevu alidanganywa vipi? Alichemka wapi? Anyway kuanza upya si Ujinga. Akae wayamalize na Ukraine. Vita si lelemama. Watu walitaka kupima nguvu yake. Ameji expose sana. Bora angebaki vile vile ambavyo tulikuwa tunamwogopea. Akina Yericko Nyerere siku hizi wamekata na tamaa kabisa. Nyie msidhani hata mataifa makubwa yanataka vita. Mwenye kujielewa anaepusha mapema.

View attachment 3087753
Hawajaitaka Tanzania kuwa mpatanishi maana ni nchi ya amani?
 
Unafikiri Ukraine au Putin ndiyo wamechelewesha vita?

Kumbe hata kinachoendelea hukielewi.

Hilo tangazo la Putin ni bonge la strategy ya kisaikolojia.

Ha ha ha....... Putin akisoma hapa atacheka sana. Kuwa wewe unafaham strategy ambazo yeye hazifahamu kwa miaka yote 2.🤣🤣🤣🤣 Ameacha kusoma kama ambavyo nanyi mmekimbia. Huko Mayahudi na Maarabu yanaendeleaje?
 
Nitarudi kuchangia vita ikiisha.

mpaka kufikia mwakajana, mwezi June, kwa taarifa ya prigozhin, mkuu wa Wagner, ni kwamba Urusi ilikuwa imepoteza askari 120,000. Hii si idadi ndogo, ambayo unaweza kusema kuwa Urusi hai-feel maumivu makali ya hii vita. Fikiria kuwa kwa siku moja, hii vita inaigharmu Urusi kati ya dola milioni 500 na dola bilioni 1. Zidisha kwa idadi ya siku ambayzo vita imekuwa ikiendelea. Kwa nchi kama Urusi ambayo wananchi wake wengi wanaishi kwenye umaskini, hii pesa ingeweza kuwasaidia wananchi wananchi wake kwa kiasi gani!

Wagner PMC chief Yevgeny Prigozhin confirmed that his organization had lost over 20,000 troops killed by May 25, 2023.[76] He went on to claim that overall, the Russian military had lost 120,000 dead in Ukraine by late June. He accused the Ministry of Defence of systematically downplaying Russian losses.[77]
 
Kipi hicho? Maana hizi taarifa kila siku tunadanganyana. Unadhani Putin anatuamini tena kwa haya maneno? Ameamua yeshe sheikh wangu.
1725542634968.png

Maafisa kibao wa NATO wameuwawa chuo cha kijeshi, Poltava, Ukraine
 
Kwahiyo kwa akili yako unaona Putin anapigana na Nchi moja??? Kwa kifupi Putin anapambana na Nchi zote za Ulaya ndio maana imekuwa hivyo, ingekuwa Ukraine pekee sitaki kusema angetumia muda gani.
Akili ni nywele...
Moja kati ya kitu kibaya kabisa kufanya unapokuwa kweny vita au mashindano ni kumdharau mpinzani wako
 
Kwahiyo kwa akili yako unaona Putin anapigana na Nchi moja??? Kwa kifupi Putin anapambana na Nchi zote za Ulaya ndio maana imekuwa hivyo, ingekuwa Ukraine pekee sitaki kusema angetumia muda gani.
Akili ni nywele...
Putin alifanya mahesabu ya vita vibaya. Hakufanya Upembuzi Yakinifu wa Kina kabla ya kuanzisha vita yake hiyo.
Kukurupuka katika kufanya Maamuzi ni Jambo la kawaida kabisa kwa Watawala wenye Itikadi ya Ujamaa/Ukomunisti, tafakuri ya kina huwa wanaifanya baada ya kupata matokeo mabaya yanayoambatana na majuto.
 
Tangu majuzi kati anatuma makombora ya masafa marefu ( Ballistic) zaidi ya 100 kila siku na drones zaidi ya 500.

Cha kushangaza hamalizi vita bali aonekane anapigana.

Soon atalegea...huwezi kupigana vita miaka 5 afu uchumi wako ukabakia salama.
Watu tayari washaondoka na kipande chake cha ardhi.
 
Duh!
Hujui chochote kuhusu mpango wa amani wa Istanbul .
Uzuri ni kwamba Putin ashasema eneo lote lililochukuliwa na Russia haitawahi kuwa Ukraine Tena.
Ukimuuliza maeneo aliyo nayo Russia hayamtoshi kwani?

Na yeye abebe silaha aende front asifurahie vifo vya watoto wa watu.
 
Mbona huwa wanaema kila wakati. Au ww umeanza kufuatilia leo. Urusi tangu siku ya kwanza anaingia anasema wako tayar kwa mazungumzo. Na alishasisitiza, tejea mpango wa amani wa Instanbul.
 
Akina Ritz Webabu ChoiceVariable FaizaFoxy walikuwa wanampotosha sana Putin. Akajikuta yeye ni Mwaaaaaaamba. Akasema ana operation ya siku chache kumwondoa Rais wa Ukraine.

Mwaka wa pili sasa.... Nashindwa kuelewa. Putin ni Jasusi mbobevu alidanganywa vipi? Alichemka wapi? Anyway kuanza upya si Ujinga. Akae wayamalize na Ukraine. Vita si lelemama. Watu walitaka kupima nguvu yake. Ameji expose sana. Bora angebaki vile vile ambavyo tulikuwa tunamwogopea. Akina Yericko Nyerere siku hizi wamekata na tamaa kabisa. Nyie msidhani hata mataifa makubwa yanataka vita. Mwenye kujielewa anaepusha mapema.

View attachment 3087753

Vita yoyote ni ngumu, USA walijua watachukua mwezi mmoja miwili Somalia, Iraq, Syria, Afrighanistan wakaishia kukaa zaidi kibao na waliboondoka hizo nchi zilikuwa katika hali mbaya zaidi.
 
Back
Top Bottom