Putin, ameanza kuona gharama za ya Vita. Mara ya kwanza alikuwa anasoma sana Threads za JF akapotoshwa?

Kisago wanachopata NATO huko Ukraine kwani wewe hukioni?
 
Kwahiyo kwa akili yako unaona Putin anapigana na Nchi moja??? Kwa kifupi Putin anapambana na Nchi zote za Ulaya ndio maana imekuwa hivyo, ingekuwa Ukraine pekee sitaki kusema angetumia muda gani.
Akili ni nywele...
Majeshi ya Urusi yalifurushwa toka mjini Kiev huku Ukraine ikiwa haina msaada wowote toka Taifa la nje. Tena wakati huo Urusi ikitumia kikosi chake cha juu kabisa kwenye utaalam wa kivita. Bahati mbaya askati hao, walio wengi waliangamia kwa kuuawa na Askari wa Ukraine, wengine waliuawa na wananchi wa kawaida.

Baada ya mafanikio hayo ya awali ndipo USA na mataifa ya Ulaya yalipoona kuwa kumbe kuna uwezekano wa Ukraine kupambana na Urusi endapo ikisaidiwa kwa kupewa silaha.

Kadiri vita inavyoendelea, wataalam wote wa masuala la kivita waliotoa maoni yao wanakubaliana kuwa uwezo wa kivita wa Urusi ulikuwa over-exagerated. Kwa sasa inaonekana wazi kabisa kuwa utaalam wa kivita wa Urusi na Ukraine, huenda Ukraine wapo vizuri zaidi, maana wakiamua kushambulia depot za mafuta au maghala ya silaha, wanapiga hapo hapo. Lakini Urusi ina lengo la kupiga ghala la silaha, inaenda kupiga hospitali, wakati hospitali ipo kilometer 5 toka kwenye target.

Urusi kwa sasa anasaidiwa zaidi na ukubwa wa uchumi na hifadhi ya silaha alizozitengeneza kwa miaka mingi, ikilinganishwa na Ukraine, lakini kiutaalam katika vita, hana cha pekee zaidi ya Ukraine.

Na vita hii ikiisha, baada ya miaka 10 ijayo, Ukraine bila shaka itakuwa miongoni mwa mataifa yenye jeshi bora kabisa Duniani.
 
Kwahiyo kwa akili yako unaona Putin anapigana na Nchi moja??? Kwa kifupi Putin anapambana na Nchi zote za Ulaya ndio maana imekuwa hivyo, ingekuwa Ukraine pekee sitaki kusema angetumia muda gani.
Akili ni nywele...
Kwahiyo intelijensia yake haikumjulisha kuwa kuna wahuni wataingilia akajihakikishia kuwa ule mkwara mbuzi wake utatosha kuwazua wanyamwezi kupita mlango wa nyuma?

Umemuunga mkono mtoa mada kiaina. Putin alipotoshwa, intelijensia yake ni dhaifu, si kama tulivyoidhania mwanzo.
 
Vipi ndo unamka usingizini.Yaani Ukraine wanakula mabomu halafu wewe unamuamini Putin..Putin mjanja anataka ulimwengu usimuone kuwa mkorofi..mambo ya diplomasia lkn ndani huko itakuwa kawaamuru vijana..waendelee kuichapa Ukraine mpaka isalimu amri.

Yaani wewe upo Mchambawima unakuna na utetezi wa kipuuzi kama huu? Elewa vita siyo lelemama dogo. Putin ameliona hilo. Haijawa ya week ni mwaka wa 2 sasa.
 
Amekwambia kwamba ameshindwa vita?

Juzi tu kasambaratisha mercenaries kama 600 na leo kachinja tena wengine waliokuwa hotelin
Hasara inayotokana na matokeo ya ndani kwenye serikali yake Putin utayajua saa ngapi mrusi mweusi wewe

Wakati wewe ukiona kuchinja wanajeshi wa Ukraine ndio ushindi, kumbe usijue hicho kichinjio kinagharama ipi katika serikali ya Russia na Putin, na kwenye vita mara nyingi mkubwa huwa hasemi ukweli wa jinsi anapigwa, Putin na serikali yake hawawezi kukiri uwingi wa jeshi linaloangamizwa na ka nchi kadoogo ka Ukraine

Ni ujinga kuamini eti Russia haimgharimu chochote hii vita

Nasemaje..! Anayohasara kubwa mno kiasi cha yeye kurudi nyuma kiuchumi tofauti na asingekuwa na vita

Na pia nakuhakikishia kwamba, Putin hatashinda hiyo vita licha kwamba nje mnaona Ukrain kachakazwa
 
Swali ni kwamba ameshindwa vita?
 
Duh!
Hujui chochote kuhusu mpango wa amani wa Istanbul .
Uzuri ni kwamba Putin ashasema eneo lote lililochukuliwa na Russia haitawahi kuwa Ukraine Tena.
Ukraine waliona hilo, ndio maana wakachukua sehemu ya Urusi ya Kursk, ili kama watajadiliana, Warusi wakisema wanashikilia maeneo waliyoteka, na Ukraine watasema hivyo hivyo - mwaga mboga nimwage ugali, la sivyo wote turudishe mboga na ugali mezani tule!
 
Kwahiyo kwa akili yako unaona Putin anapigana na Nchi moja??? Kwa kifupi Putin anapambana na Nchi zote za Ulaya ndio maana imekuwa hivyo, ingekuwa Ukraine pekee sitaki kusema angetumia muda gani.
Akili ni nywele...
Alikua hajui hilo kabla??
 
Kwahiyo kwa akili yako unaona Putin anapigana na Nchi moja??? Kwa kifupi Putin anapambana na Nchi zote za Ulaya ndio maana imekuwa hivyo, ingekuwa Ukraine pekee sitaki kusema angetumia muda gani.
Akili ni nywele...
ndio maana unaambiwa vita ni akili sio manguvu tu
wenzie target yao ilikuwa ni hiyo na wamemchosha kweli kweli na udhaifu wake umeonekana
 
Upo vizuri sn comrade
 
Putin kanyooshwa haswa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…